Swahili Christian Movie "Nuru ya Kweli Yaonekana" | The Good News From God

21/06/2018

Gangqiang ni Mkristo. Aliona namna upendo wa Bwana na huruma Yake kwa binadamu vilivyo vikubwa, na akaamua mara nyingi kwamba angempenda Bwana, kumridhisha Bwana, kutekeleza neno la Bwana, na kuwa na mwenendo wake binafsi kama mtu anayesifiwa na Bwana. Lakini alipotoa athari ya kimatendo kwa neno la Bwana, aligundua kwamba kwake yeye mwenyewe kulikuwa na mambo mengi potovu na ya uasi-ubinafsi, kiburi, udanganifu, na ulaghai na kadhalika. Tabia hizi potovu zilikuwa zinamrudisha nyuma, na hakuwa na nguvu kamwe za kuyatekeleza maneno ya Bwana. Kwa sababu hii, alikuwa na mfadhaiko kabisa, na mara nyingi alimwita Bwana kwa usadizi. Gangqiang baadaye alienda Marekani kufanya kazi na huko akafahamiana na Dada Zhao wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kupitia kwa mawasiliano ya Dada Zhao na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kwa kuyasoma baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, Gangqiang alipata kujua kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari Amerudi, na kwamba Alikuwa ametekeleza kazi ya kuhukumu na kutakasa binadamu, Akimwelekeza binadamu katika njia ya kuitatua asili yake yenye dhambi. Moyo wa Gangqiang ulikuwa umepata nuru, na alikubali kwa furaha kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na akaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu, aliuelewa ukweli fulani, na maisha yake ya huzuni yaliangazwa na maneno ya Mungu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Baadhi ya taarifa katika video hii zinatoka kwa:

NASA

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp