Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

10/11/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.

Kanisa hulenga kuanzisha kanisa ambalo linapendeza moyo wa Mungu, ili kwamba waumini wanaweza kuhudumu na kuruzuku wenyewe kwa wenyewe katika maneno ya Mungu na upendo wa Mungu, wanaweza kutii na kumwabudu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, na wanaweza kuwa ushuhuda wa kweli kwa Mungu na onyesho la utukufu wa Mungu.

Kanisa linalenga kueneza na kushuhudia kwa injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu, likiwaruhusu watu kuona kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi wa siku za mwisho, na kwamba Yeye ameanza kazi ya “lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17) iliyotabiriwa katika Biblia, ambayo kabisa ni kazi ya Mungu ya kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kikamilifu katika siku za mwisho. Ni kwa kukubali tu ukweli wote unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ambapo mtu anaweza kujiondolea tabia yake ya kishetani, kujikomboa kutoka kwa utumwa wa dhambi, kutakaswa, kuja kumjua Mungu, kumtii Mungu, na kumwabudu Mungu, kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kuokoka majanga makubwa ya siku za mwisho na kuingia katika ufalme wa Mungu–hii tu ndiyo hatima nzuri ya wanadamu. Kueneza na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na hivyo kuleta mbele ya Mungu wale ambao hukiri kwamba kuna Mungu na wanapenda ukweli ili wapate kukubali na kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho–hili ni agizo la Mungu kwa wateule Wake, na malengo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp