Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 14

07/06/2020

Kila hatua ya kazi ya Roho Mtakatifu inahitaji ushuhuda sawia kutoka kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi ni vita kati ya Mungu na Shetani, na mlengwa katika vita hivi ni Shetani, huku atakayekamilishwa na kazi hii ni mwanadamu. Kazi ya Mungu kuzaa au kutozaa matunda inategemea na jinsi ushuhuda wa mwanadamu ulivyo. Huu ushuhuda ndio Mungu anaohitaji kutoka kwa wale wanaomfuata; ni ushuhuda unaofanywa mbele ya Shetani, na unaothibitisha athari za kazi Yake. Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kikamilifu, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na huo ushuhuda ndio matendo ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu iwe au isiwe na athari inayohitajika, au pawepo ama pasiwepo ushuhuda wa kweli, ni mambo ambayo yameunganishwa na ushuhuda wa mwanadamu. Wakati kazi itakapokwisha, yaani, wakati usimamizi wa kazi ya Mungu utakapofikia kikomo, Mwanadamu atahitajika kuwa na ushuhuda wa hali ya juu, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho wake, matendo na kuingia kwa mwanadamu vitafikia kilele chake. Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kuzingatia sheria na amri, na alihitajika kuwa mpole na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na zaidi bado anahitajika kumpenda Mungu katika mateso. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia toka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji ya mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa hali hii, umbo la usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa juu kuliko tabia yake inavyoweza kufikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo ambapo wanadamu wataanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ndipo kazi ya Mungu itafikia kikomo, wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili abadilishe tabia zake hautakuwepo, na wanadamu wote wataishi kwenye nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu. Aidha Mungu hatamwekea matakwa mwanadamu, na patakuwepo na ushirikiano mwema zaidi kati ya mwanadamu na Mungu, mojawapo ikiwa maisha ya mwanadamu na Mungu pamoja, maisha ambayo yatafuatia baada ya usimamizi wa Mungu kukamilishwa, na baada ya mwanadamu kuokolewa toka katika mafumbato ya Shetani. Wale ambao hawatafuata kwa ukaribu nyayo za Mungu hawatakuwa na uwezo wa kufikia maisha hayo. Watakuwa wamejishusha ndani ya giza, ambapo watalia na kusaga meno; hao ndio watu wanaoamini katika Mungu lakini hawamfuati Yeye, wanaoamini katika Mungu lakini hawatii kazi Yake yote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp