Mtu anawezaje kwa kweli kuwa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi?

17/02/2020

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27).

“Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho” (Ufunuo 2:7).

“Usitoe machozi: tazama, Simba wa kabila ya Yuda, Shina lake Daudi, ameweza kukifungua hicho kitabu, na kuzitoa muhiri saba zilizoko” (Ufunuo 5:5).

“Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1: 8).

Maneno Husika ya Mungu:

Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu. Bila shaka, kupata mwili huku hakufanyiki kivyake, bali ni hatua ya tatu ya kazi baada ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kila hatua mpya ya kazi ya Mungu kila mara huleta mwanzo mpya na enzi mpya. Vivyo hivyo kuna mabadiliko yanayokubaliana katika tabia ya Mungu, katika njia Yake ya kufanya kazi, katika sehemu Yake ya kufanya kazi, na katika jina Lake. Ndiyo maana basi ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi ya Mungu katika enzi mpya. Lakini licha ya jinsi anapingwa na mwanadamu, Mungu huendelea kufanya kazi Yake, na daima Yeye huwa Akiongoza wanadamu wote kuendelea mbele. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita. Kazi ya hatua hii inafanywa kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Neema. Ikiwa hatua hizi mbili za kazi hazikuhusiana, kwa nini basi kusulubiwa hakurudiwi katika hatua hii? Kwa nini Sibebi dhambi za mwanadamu, lakini badala yake Naja kumhukumu na kumwadibu mwanadamu moja kwa moja? Ikiwa kazi Yangu ya kumhukumu na kumwadibu mwanadamu na kuja Kwangu saa hii si kwa njia ya Roho Mtakatifu na hakukufuata kusulubiwa, basi Nisingekuwa na sifa zinazostahili kumhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kazi katika hatua inajenga kabisa juu ya kazi katika hatua iliyotangulia. Hiyo ndiyo maana ni kazi kama hii tu ndiyo inaweza kumleta mwanadamu katika wokovu hatua kwa hatua. Yesu pamoja na Mimi tunatoka kwa Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizo nazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; Miili Yetu ina maumbo tofauti, lakini hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji tofauti ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndiyo maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukielewa leo hii si kama kile cha wakati uliopita; ni hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na kwamba hawakuzaliwa katika familia moja, sembuse katika kipindi kimoja, hata hivyo Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, haipingiki kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni miili ya nyama ya Mungu, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja na hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Wayahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba Wao ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi za nje za miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini sura ya nje ya miili Yao na kuzaliwa Kwao hakufanani. Mambo haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu Yao, maana, kimsingi, Wao ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi Zao zote zinaongoza Roho Zao, ambazo zinawapa kazi tofauti katika nyakati tofauti, na miili Yao kwa ukoo tofauti. Roho wa Yehova si baba wa Roho wa Yesu na Roho wa Yesu si mwana wa Roho wa Yehova: Ni Roho moja. Vile vile Kama vile Mungu mwenye mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Mungu anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu; na hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, hii si kudura ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili inaonekana kwa wanadamu kuwa tofauti kabisa na ile ya kwanza, kiasi kwamba kazi hizi mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, na hakuna chochote katika kazi ya kwanza kinachoweza kuonekana wakati huu. Japo kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili ni tofauti na ile ya kwanza, hili halithibitishi kuwa chanzo Chao si kimoja na sawa. Iwapo chanzo Chao ni kimoja inategemea aina ya kazi iliyofanywa na miili na si katika maumbo Yao ya nje. Katika hatua tatu za kazi Yake, Mungu Amekuwa mwili mara mbili, na mara zote kazi ya Mungu kuwa mwili inaanzisha enzi mpya, inaanzisha kazi mpya; kuwa mwili kwa mara ya kwanza na pili kunakamilishana. Macho ya wanadamu hayawezi kugundua kuwa hii miili miwili kwa kweli imetokana na chanzo kimoja. Ni wazi kwamba hili liko nje ya uwezo wa macho ya wanadamu au akili za wanadamu. Ila katika kiini Chao, ni miili sawa, kwani kazi Yao inatokana na Roho mmoja. Iwapo hii miili miwili inatokana na chanzo kimoja haiwezi kuamuliwa kutokana na enzi na sehemu Ilipozaliwa, au vigezo vingine kama hivyo, ila kwa kazi ya uungu iliyoonyeshwa Nayo. Kupata mwili wa pili hakufanyi kazi yoyote iliyofanywa na Yesu, kwani kazi ya Mungu haifuati makubaliano, lakini kila wakati inafungua njia mpya. Kupata mwili wa pili hakulengi kuongeza au kuimarisha maono ya kupata mwili wa kwanza katika akili za watu, ila kuutimiza na kuukamilisha, kuongeza kina cha wanadamu kumwelewa Mungu, kuvunja sheria zote ambazo zipo katika mioyo ya watu, na kufuta picha za uongo kuhusu Mungu mioyoni mwao. Ni wazi kuwa hakuna hatua yoyote ya kazi ya Mungu mwenyewe inaweza kumpa mwanadamu ufahamu kamili wa Mungu; kila mojawapo inatoa kwa sehemu tu, si ufahamu mzima. Japo Mungu Ameonyesha tabia Yake kikamilifu, kwa sababu ya upungufu wa ufahamu wa wanadamu, ufahamu wake kuhusu Mungu si kamili. Haiwezekani, kutumia lugha ya wanadamu, kueleza tabia nzima ya Mungu; basi hatua moja tu ya kazi Yake itamwelezaje Mungu kikamilifu? Anafanya kazi katika mwili kwa kujisetiri katika ubinadamu Wake wa kawaida, na mtu anaweza kumjua tu kupitia kwa maonyesho ya uungu Wake, si kupitia kwa umbo Lake la kimwili. Mungu Anakuja katika mwili kumruhusu mwanadamu Amjue kupitia kazi Zake mbalimbali, na hakuna hatua mbili za kazi Yake zinafanana. Ni kwa njia hii tu mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu kamili wa kazi ya Mungu katika mwili, si kwa kujifunga katika kipengele kimoja tu. Japo kazi ya hii miili miwili iliyopatikana ni tofauti, kiini cha hii miili, na chanzo cha kazi Yao vinafanana; ni kwamba tu Ipo ili kutekeleza hatua mbili tofauti za kazi, na inatokea katika enzi mbili tofauti. Licha ya jambo lolote, miili ya Mungu katika mwili inashiriki kiini kimoja na asili moja—huu ni ukweli ambao hauwezi kupingwa na yeyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp