Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?

22/09/2018

Kwa nini ni lazima kupitia kazi ya hukumu katika siku za misho ili kuweza kupata maarifa ya Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli(Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).

“Mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi” (Yohana 14:10).

“Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30).

Maneno Husika ya Mungu:

Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na Alitoka kwa na, na akazidi mawanda ya ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Yake na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Mungu anafanya kazi mpya katika siku za mwisho. Atafichua tabia Yake zaidi, na haitakuwa huruma na upendo wa wakati wa Yesu. Kwa kuwa Ana kazi mpya, kazi hii mpya itaandamana na tabia mpya. Kwa hiyo kama kazi hii ingefanywa na Roho—kama Mungu hangepata mwili, na badala yake Roho angenena moja kwa moja kupitia radi ili mwanadamu hangekuwa na njia ya kuwasiliana na Yeye, je, mwanadamu angejua tabia yake? Kama Roho tu Angefanya kazi, basi mtu hangekuwa na njia yoyote ya kujua tabia Yake. Watu wanaweza tu kuona tabia ya Mungu kwa macho yao wenyewe wakati Anapopata mwili, wakati ambapo Neno laonekana katika mwili, na Anaonyesha tabia Yake yote kupitia mwili. Mungu kweli huishi kati ya wanadamu. Anaonekana; mwanadamu anaweza kweli kujihusisha na tabia Yake na kile Anacho na Alicho; ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumjua kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele kitakatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria Kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. … Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Katika kipindi hiki akimfuata Yesu, Petro alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa Roho Mtakatifu, ufahamu huu haukuwa wazi kabisa, na haya yanaonekana katika maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na hakuwa dhahiri kuyahusu. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa kwa kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno Yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na umbo la ajabu na lisilo la kawaida kwa kweli. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyofichua hulka iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi kwamba alionekana kuwa njiwa anayerukaruka na kuchezacheza, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyechoka sana. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na madai makali Aliyotoa kwa watu yalimfanya aje kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Upendo wa Mungu umeonyeshwa katika kazi Yake: ni baada tu ya kupitia kazi Yake ndipo wanaweza wakagundua upendo Wake, ni katika matukio wanayopitia ya hakika tu ambapo wanaweza kufahamu upendo wa Mungu. Kuna mengi ya kupendeza kumhusu Mungu, lakini bila ya kujihusisha na Yeye kwa hakika watu wengi hawana uwezo wa kuyagundua. Hivi ni kusema, kama Mungu asingefanyika mwili, watu wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, na kama wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, pia wasingeweza kupitia Kazi Yake—na kwa hivyo upendo wao kwa Mungu ungetiwa doa la uongo mwingi na mawazo. Upendo wa Mungu ulio mbinguni si halisi kama upendo wa Mungu ulio ulimwenguni, kwa kuwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliye mbinguni umejengwa katika mawazo yao, bali si kwa yale ambayo wameyaona kwa macho yao, na yale ambayo wameyapitia wao wenyewe. Mungu anapokuja ulimwenguni, watu wanaweza kuyaona matendo Yake halisi na upendo wake, na wanaweza kuona kila kitu katika matendo na tabia Zake za kawaida, ambayo ni mara elfu halisi kuliko ufahamu wa Mungu aliye mbinguni. Bila kujali ni vipi ambavyo watu wanampenda Mungu aliye mbinguni, hakuna kitu halisi kuhusu huu upendo, na umejaa mawazo ya kibinadamu. Haijalishi udogo wa upendo wao kwa Mungu aliye duniani, huu upendo ni halisi; hata kama ni kidogo, ungali ni halisi. Mungu huwafanya watu kumjua kupitia kazi halisi, na kupitia ufahamu huu Anapata upendo wao. Ni kama Petro: kama hangeishi na Yesu, haingewezekana yeye kumwabudu Yesu. Aidha, huu uaminifu ulijengwa kwenye uhusiano wake na Yesu. Ili kumfanya mwanadamu ampende, Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu na kuishi na wanadamu, na yote Anayomfanya mwanadamu kuona na kupitia ni uhalisi wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Kikundi cha watu ambao Mungu mwenye mwili Anataka kupata leo ni wale wanaokubali mapenzi Yake. Watu wanahitaji tu kutii kazi Yake, sio daima kujishughulisha na mawazo ya Mungu aliye mbinguni, waishi ndani ya hali isiyo dhahiri, au kufanya mambo kuwa magumu kwa Mungu mwenye mwili. Wale ambao wanaweza kumtii ni wale wanaoyasikia kabisa maneno Yake na kutii mipango Yake. Watu hawa hawajali kamwe jinsi Mungu mbinguni alivyo kwa kweli au ni kazi ya aina gani Mungu wa mbinguni Anafanya sasa kwa wanadamu, lakini wao humpa Mungu aliye duniani mioyo yao kabisa na kuweka nafsi zao zote mbele Yake. Kamwe hawazingatii usalama wao wenyewe, na hawalalamiki juu ya ukawaida na utendaji wa Mungu katika mwili. Wale wanaomtii Mungu katika mwili wanaweza kukamilishwa na Yeye. Wale wanaomwamini Mungu mbinguni hawatapata kitu. Hii ni kwa sababu si Mungu mbinguni, lakini ni Mungu hapa duniani ndiye Anayetoa ahadi na baraka juu ya watu. Watu hawapaswi daima kumtukuza Mungu aliye mbinguni na kumwona Mungu duniani kama mtu wa wastani. Hii si haki. Mungu mbinguni ni mkuu na wa ajabu na mwenye hekima ya ajabu, lakini hii haipo kabisa. Mungu duniani ni wa wastani sana na asiye na maana; Yeye pia ni wa kawaida sana. Hana mawazo ya ajabu au vitendo vya kimiujiza. Anatenda tu na kuongea kwa njia ya kawaida na ya matendo. Ingawa Hazungumzi kwa njia ya ngurumo au kuita upepo na mvua, Yeye kwa kweli ni mwili wa Mungu aliye mbinguni, na kwa kweli ni Mungu anayeishi kati ya wanadamu. Watu hawapaswi kumtukuza yule wanayeweza kumwelewa na ambaye analingana na mawazo yao wenyewe kama Mungu, au kumwona Yeye ambaye hawawezi kumkubali na kabisa hawawezi kufikiria kama wa chini. Yote haya ni uasi wa watu; yote ni chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp