Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

22/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na inapita maarifa ya mwanadamu. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. Mwanadamu ana msamiati finyu tu ambao anaweza kufafanua yote anayojua kuhusu tabia ya Mungu: kubwa, yenye heshima, ya ajabu, isiyoeleweka, kuu, takatifu, yenye haki, yenye hekima, na kadhalika. Maneno mengi sana! Msamiati kama huo finyu hauwezi kuelezea kile kidogo mtu ameshuhudia juu ya tabia ya Mungu. Baadaye, watu wengi waliongeza maneno zaidi ili kueleza vizuri zaidi ari ndani ya mioyo yao: Mungu ni mkuu sana! Mungu ni mtakatifu sana! Mungu ni wa kupendeza sana! Leo, maneno kama haya yamefikia kilele chake, lakini bado mwanadamu hawezi kujieleza wazi wazi. Na kwa hiyo, kwa mwanadamu, Mungu ana majina mengi, lakini Hana jina moja, na hilo ni kwa sababu nafsi ya Mungu ni ya ukarimu sana, na lugha ya mwanadamu haitoshi sana. Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe. Hata hivyo, watu wengi ambao wamepata uzoefu wa kiroho na wamemuona Mungu binafsi bado wanahisi kuwa jina moja maalumu haliwezi kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake—ole wetu, hili linasikitisha, hivyo mwanadamu hamwiti Mungu kwa jina lolote, lakini humwita tu “Mungu.” Moyo wa mwanadamu unaonekana kujawa na upendo, lakini pia unaonekana kuzongwa na ukinzani, kwa maana mwanadamu hajui jinsi ya kumueleza Mungu. Kile Mungu alicho ni cha ukarimu sana, hakuna kabisa njia ya kukieleza. Hakuna jina moja ambalo linaweza kutoa muhtasari wa tabia Ya Mungu, na hakuna jina moja ambalo linaweza kuelezea yote ambayo Mungu anacho na Alicho. Kama mtu ataniuliza, “Ni jina gani hasa unalotumia?” Nitamwambia, “Mungu ni Mungu!” Je, hilo silo jina bora zaidi la Mungu? Je, huko sio kufafanua bora zaidi kuhusu tabia ya Mungu? Basi kwa nini mtumie juhudi nyingi sana kutafuta jina la Mungu? Kwa nini ufikirie sana, kukaa bila kula na kulala, kwa ajili ya jina? Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina. Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu? Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye anakuhitaji wewe, kiumbe, kuamua jina lake? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu. Wewe unaweza kusema tu kuwa mbinguni kuna Mungu, ya kwamba Yeye anaitwa Mungu, na kwamba Yeye mwenyewe ni Mungu mwenye nguvu nyingi, busara tele, wakuinuliwa sana, wa ajabu kuu, mwenye siri kuu, mwenye uweza mkuu sana, na huwezi kusema mengi zaidi; hayo ndiyo yote unayoyajua. Kwa njia hii, je, jina la Yesu tu linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe? Wakati siku za mwisho zitawadia, ingawa ni Mungu ndiye anafanya kazi yake, ni sharti jina lake libadilike, kwa kuwa ni enzi tofauti.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi ingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hii si ya ajabu, na watu wanafikiria hivyo[a] tu kwa sababu ya akili zao rahisi. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kama kazi ya Mungu katika kila enzi ni sawa daima, naye daima anaitwa kwa jina sawa, ni jinsi gani basi mwanadamu atamjua Yeye? Mungu lazima aitwe Yehova, na mbali na Mungu kuitwa Yehova, yeyote ambaye ataitwa jina jingine si Mungu. Ama kwa njia nyingine Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu, na Mungu hawezi kuitwa jina lingine isipokuwa Yesu; na mbali na Yesu, Yehova si Mungu, na wala Mwenyezi Mungu si Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa ni ukweli Mungu ni mwenye uweza, lakini Mungu ni Mungu pamoja na mwanadamu; Sharti aitwe Yesu, kwa kuwa Mungu yu pamoja na mwanadamu. Kufanya hili ni kufuata mafundisho, na kumshurutisha Mungu kwenye eneo fulani. Kwa hivyo, kazi ambayo Mungu hufanya katika kila awamu, jina ambalo Yeye huitwa, na mfano ambao yeye anatwaa, na kila awamu ya kazi yake mpaka leo, havifuati kanuni hata moja, na hayakabiliwi na kikwazo chochote. Yeye ni Yehova lakini pia ni Yesu, na vile vile ni Masihi, na Mwenyezi Mungu. Kazi yake inaweza kubadilika polepole, na kuna mabadiliko sambamba katika jina lake. Hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Yeye kikamilifu, lakini majina yote ambayo Yeye huitwa yanaweza kumwakilisha Yeye, na kazi ambayo Amefanya katika kila enzi inawakilisha tabia yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. Kazi ambayo Yesu Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Neema, na kazi ambayo Yehova Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Yehova Aliwaongoza tu watu wa Israeli na Misri, na mataifa yote nje ya Israeli. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema ya Agano Jipya ilikuwa kazi ya Mungu katika jina la Yesu kwa kuwa Yesu ndiye Aliongoza enzi hii. … Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anafungua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele. Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye afungue njia mpya, sharti aanzishe enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Tanbihi:

a. Nakala ya awali inasoma “ambayo ndiyo.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp