Uhusiano gani kati ya kila hatua ya kazi ya Mungu na jina Lake

22/09/2018

(1) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Sheria

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na Mungu akasema zaidi kwa Musa, Utawaambia hivi wana wa Israeli, Yehova Mungu wa baba zenu, Mungu wake Ibrahimu, Mungu wake Isaka, na Mungu wake Yakobo, amenituma kwa ninyi: jina langu ni hili milele, na hili ni kumbukumbu yangu kwa vizazi vyote” (Kutoka 3:15).

Maneno Husika ya Mungu:

“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. … Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. … Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Watu wa Israeli wote walimwita Yehova, Bwana wao. Wakati huo, walimwona kama kichwa cha familia zao, na Israeli yote ikawa familia kubwa ambapo kila mtu alimwabudu Bwana wao Yehova. Roho wa Bwana mara nyingi Aliwatokea, naye akanena na kutamka sauti Yake, na kutumia nguzo ya wingu na sauti kuongoza maisha yao. Wakati huo, Roho alitoa mwongozo Wake katika Israeli moja kwa moja, Akizungumza na kutoa sauti Yake kwa watu, na waliona mawingu na kusikia sauti za ngurumo, na kwa njia hii Aliyaongoza maisha yao kwa maelfu kadhaa ya miaka. Kwa hiyo, watu wa Israeli pekee wamekuwa wakimwabudu Yehova daima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Baada ya kuwaumba wanadamu, Yehova hakuwaagiza au kuwaongoza kutoka wakati wa Adamu hadi ule wa Nuhu. Badala yake, baada ya dunia kuharibiwa na gharika tu ndiyo wakati ambapo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa Adamu. Kazi na matamshi Yake huko Israeli yaliwapa watu wote wa Israeli mwongozo walipokuwa wakiishi maisha yao katika nchi yote ya Israeli, na kwa njia hii yakaonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kupuliza pumzi ndani ya mwanadamu, ili aweze kuwa na uhai kutoka Kwake na kuinuka kutoka mavumbini kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini kwamba pia Angeweza kuwachoma wanadamu, na kuwalaani wanadamu, na kutumia fimbo Yake kuwatawala wanadamu. Kwa hivyo, pia waliona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani, na kuzungumza na kufanya kazi miongoni mwa binadamu kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya kazi hiyo ili tu viumbe Wake waweze kujua kwamba mwanadamu alitoka kwa mavumbi yaliyochaguliwa na Yeye, na aidha kwamba mwanadamu alikuwa ameumbwa na Yeye. Siyo haya tu, lakini kazi Aliyoanza huko Israeli ilikusudiwa ili kwamba watu na mataifa (ambao kwa kweli hawakuwa wametengwa na Israeli, lakini badala yake walikuwa wameenea kutoka kwa Waisraeli, ilhali bado walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe wote walioumbwa ulimwenguni waweze kuwa na uwezo wa kumcha Yehova na kumchukulia kuwa mkuu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

(2) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Neema

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Malaika wa BWANA alitokea kwake ndotoni, akisema, Yusufu, wewe mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu mke wako: kwa kuwa alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu. Na atazaa mwana, na wewe utamwita jina lake YESU: kwa sababu atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao” (Mathayo 1:20-21).

“Na malaika akamwambia, Usiwe na woga, Mariamu: kwa kuwa umepata fadhili kwa Mungu. Na, tazama, utashika mimba na kumzaa mwana wa kiume, na utamwita jina lake YESU. Atakuwa mkuu, na ataitwa Mwana wa Aliye juu zaidi: na atapewa kiti cha enzi cha babake Daudi na Bwana Mungu: Na atatawala nyumba ya Yakobo milele; na ufalme wake hautakuwa na kikomo” (Luka 1:30-33).

Maneno Husika ya Mungu:

Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena; badala yake Yeye Aliitwa Yesu, na kutoka hapa Roho Mtakatifu Alianza kazi hasa kwa kutumia jina la Yesu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

“Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. … Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. … “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, Alileta njia ya ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, “Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba.” Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvu ya kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Katika kazi ya Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Na kuhusu tabia Yake, ilikuwa tabia ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Shetani akasema, “Kwa kuwa Unampenda mwanadamu, Lazima Umpende kwakwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Upigiliwe misumari msalabani, kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, kutoka kwa dhambi, na Wewe utajitolea Mwenyewe badala ya wanadamu wote.” Shetani akatoa dau ifuatayo: “Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenye upendo na Mwenye huruma, lazima Umpende mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Ujitoe Mwenyewe msalabani.” Yesu akasema, “Maadamu ni kwa ajili ya wanadamu, basi Niko tayari kutoa Yangu yote.” Baadaye, Alikwenda msalabani bila kujifikiria hata kidogo, na kuwakomboa wanadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walitafuta kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso kwa muda mrefu, na hawakuwahi kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

(3) Umuhimu wa Mungu kuchukua jina la Yehova katika Enzi ya Ufalme

Aya za Biblia za Kurejelea:

Wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Yehova kitalitamka(Isaya 62:2).

Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12).

Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi(Ufunuo 1:8).

Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala(Ufunuo 11:17).

Vitendo vyako ni vikubwa na vya ajabu, Bwana Mungu Mwenyezi; njia zako ni za haki na za kweli, wewe Mfalme wa watakatifu(Ufunuo 15:3).

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 8

Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Wakati ambapo sauti za ngurumo saba zinatoka, kuna wokovu wa wale wanaonipenda Mimi, wanaonitamani kwa mioyo ya kweli. Wale wote ambao ni Wangu na ambao Nimewajaalia na kuwachagua wanaweza kuja chini ya jina Langu. Wanaweza kusikia sauti Yangu, ambayo ni wito wa Mungu. Acha wale walio katika miisho ya dunia waone kwamba Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ni upendo, Mimi ni huruma, Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, na hatimaye Mimi ni hukumu isiyo na huruma.

Acha wote ulimwenguni waone kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe halisi na kamili. Watu wote wanaamini kabisa na hakuna mtu anayethubutu kunipinga tena, kunihukumu au kunikashifu tena. Vinginevyo, watakumbana na laana mara moja na msiba utawafika. Watalia na kusaga meno yao tu na watasababisha uharibifu wao wenyewe.

Wacha watu wote wajue, wachaijulikane hadi katika miisho ya ulimwengu; na kila mtu na ajue: Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Kila mmoja atapiga magoti ili kumwabudu Yeye na hata watoto ambao wamejifunza tu kuzungumza wataita “Mwenyezi Mungu”!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 35

Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp