Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba
Mkusanyiko wa miongo ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka ishirini na kitu iliyopo katikati ya kuzaliwa na kukomaa hupita kwa muda mfupi tu wa kupepesa jicho, na ingawaje wakati huu katika maisha mtu anachukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika kundi hili la umri wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Wanapozidi kupata uzoefu zaidi, ndipo wanapopiga hatua kwa utaratibu hadi kwenye umri wa miaka ya kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini huanza kuupata uzoefu unaoanza kuota wa maisha na hatima yake, lakini fikira zao kuhusu mambo haya zingali na ukungu mwingi sana akilini mwao. Si mpaka umri wa arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kumwelewa binadamu na ulimwengu, vilivyoumbwa na Mungu, na kung’amua kwamba maisha ya binadamu yanahusu tu, kile ambacho hatima ya binadamu inahusu. Baadhi ya watu, ingawaje wamekuwa wafuasi wa muda mrefu wa Mungu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sikwambii hata unyenyekevu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawaje wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo hoja ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kwenye kipindi cha matendo halisi cha kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wajinga kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao bure bilashi.
Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa kwa sura tatu. Sura ya kwanza ni ujana, miaka ile ya kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kuanzia kuzaliwa hadi kugonga miaka thelathini. Sura ya pili ni ya ukomavu, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi sitini. Na sura ya tatu ni kile kipindi cha uzee wa mtu, kuanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini hivi, mpaka pale mtu anapoondoka ulimwenguni. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha ni finyu na ni yale ya kuiga tu kama kasuku, fikira za wengine yanayokosa hali halisi iliyo ya kweli na ya matendo. Kwenye kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na namna ambavyo mtu anapojipanga katika ulimwengu vyote ni vya juujuu na vinyonge sana. Hiki ndicho kipindi cha mtu cha utoto. Baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo anapofaidi na kupata ufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—kwa kufichika akilini, na ndani kabisa ya moyo wake—huanza kwa utaratibu kushukuru kutoweza kurudishwa nyuma kwa hatima, na kuanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha kuanza kukomaa kwa mtu. Baada ya mtu kusita kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, na kujumlisha mafanikio na makosa ya maisha ya mtu huyo, na anasubiria hukumu ya Muumba kwa maisha ya mtu—hiki ni kipindi cha ukomavu. Tukitilia maanani aina hizi tofauti za kile mtu amepitia na kufaidi ambako watu hupata kwenye vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au karibu na hapo kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na kanuni za sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawaje ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua hoja ya ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, watu wale wanaotaka kazi ya Mungu kuisha haraka, wanaopenda Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama hali Yake halisi na muda si muda kubarikiwa, wanayo hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na ujinga wa kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, kwenye muda wao finyu, kung’amua fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu werevu, wenye akili zao. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na shughuli za kufuatilia: Wale wanaotafuta baraka ni wachoyo na waovu; hawatilii maanani mapenzi yoyote ya Mungu, wala hawatafuti kujua ukuu wa Mungu, wasiwahi kutamani kujinyenyekeza katika utawala huo, wanataka kuishi tu wanavyopenda. Wao ni watovu wa wema; wao ndio wanaofaa kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kutimiza tamanio la Mungu. Watu kama hao huishi kwa nuru, huishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kupongezwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda gani ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka katika udhibiti wa Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka katika huruma Yake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka katika huruma Yake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kijinga, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatapata maana na kuepuka kuwa hapo tu, ndipo watakapopata wokovu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?