Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

10/09/2019

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, akithibitisha majina yao, anwani, umri, na uzoefu wao wote. Kila kitu walichofanya walipokuwa hai kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni.

Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa mahali ambapo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi ambazo wamezitenda, pia ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—hili ni tukio la kwanza ambalo linatokea katika hatua hii ya pili. Kwa sababu ya mambo mabaya waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, watakapozaliwa tena katika mwili mpya huenda hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini.… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la. Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo linaogopesha? (Linaogopesha.) Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na fikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi, siyo?. Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri zaidi au vibaya kuliko jinsi wangesishi kama nguruwe? (Vizuri zaidi.) Je, mtu atakuwa wa faraja zaidi kama mtu angezaliwa kama paka? Angekuwa mnyama sawa tu, na kuwa paka ingekuwa rahisi zaidi kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa sababu paka huweza kuupitisha muda wao mwingi kulala. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito. Hivyo basi, iwapo mtu atapata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo ni sawa na adhabu nzito. Kuwa mbwa kungekuwa ni afadhali kidogo kuliko kuja kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Baadhi ya mbwa, baada ya kuwa kipenzi kwa miaka mingi, wanaweza kuelewa mengi ya yale bwana wao wanasema! Wakati mwingine na mahitaji yake na bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi. Je, mbwa basi hapati maisha ya furaha? Hivyo basi, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu hupata mwili kuwa mnyama, pia wa aina gani.

Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa kumekamilika mzunguko mmoja wa uhai na mauti. Tangu siku mtu anapowasili katika ulimwengu wa kiroho hadi mwisho wa adhabu yake, ama hadi anapozaliwa upya kama mnyama mara nyingi na anajitayarisha kuzaliwa upya kama mwanadamu, huu ni mchakato mzima.

Na wale waliokamilisha adhabu yao, na hawajapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Hili linaweza kurudiwa mara ngapi? Kwa hili kuna mipaka ya wakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kwa wakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za wakati, na vipimo vyake ni vipi? Vinalingana na ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu unahitaji kutoka kwa roho, na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao wana nafasi maalum katika ulimwengu huu. “Maalum” inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili. Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, na hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za wakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kuzaliwa katika mwili mpya, na hizi sheria na desturi zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho. Sasa mnaelewa, naam?

Kwa nafsi yoyote, kuzaliwa kwake katika mwili mpya, nafasi yake ni ipi katika haya maisha, atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Watu wa kila aina huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni. Katika maisha haya Wakati uleule, watu wengine, wamekuja kuchukua madeni yao: Walitapeliwa vitu vingi sana, na pesa nyingi sana katika maisha yao yaliyopita, na kwa hiyo, baada ya kuwasili katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapa haki na kuwapa fursa ya kukusanya madeni yao katika maisha haya. Watu wengine wamekuja kulipa deni la shukrani: katika maisha yao yaliyopita—kabla hawajafa—mtu alikuwa mkarimu kwao, na katika maisha haya wamepatiwa fursa nzuri kupata mwili ili kwamba waweze kuzaliwa upya ili kulipa upya deni hili la shukrani. Wakati uleule, wengine wamezaliwa upya katika haya maisha ili kudai uhai. Na wanadai uhai wa nani? Uhai wa mtu aliyewaua katika maisha yao yaliyopita. Kwa ujumla, maisha ya sasa ya kila mtu yana uhusiano mkubwa na maisha yao yaliyopita, yameungana kwa njia isiyoachana. Yaani, maisha ya sasa ya kila mtu yanaathiriwa pakubwa na maisha yao yaliyopita. Kwa mfano, kabla ya kufariki, Zhang alimtapeli Li kiwango kikubwa cha pesa. Je, Zhang ana deni la Li? Kwa kuwa analo, ni kawaida kwamba Li anapaswa kuchukua deni lake kutoka kwa Zhang? Hivyo basi baada ya wao kufa, kuna deni kati yao ambalo linatakiwa kulipwa. Wakati wanapata mwili mpya na Zhang anakuwa mwanadamu, je, Li anapataje deni hili kutoka kwake? Mbinu moja ni kwamba Li anapata deni lake kwa kuzaliwa upya kama mwana wa Zhang, Zhang anapata pesa nyingi, na zinaliwa na Li. Haijalishi Zhang anapata pesa nyingi kiasi gani, mwana wa Li anazitumia ovyo. Haijalishi Zhang anapata kiasi gani cha pesa, katu hazitoshi, wakati uleule, mwanawe, kwa namna fulani daima anazitumia pesa za babake kupitia njia na mbinu mbalimbali. Zhang anachanganyikiwa: “Kwa nini mwanangu daima amekuwa kisirani? Mbona wana wa watu wengine ni wema sana? Ni kwa nini mwanangu hana lengo, ni kwa nini hana maana na hana uwezo wa kuchuma pesa zozote, kwa nini daima ninapaswa kumsaidia? Kwa kuwa ni lazima nimsaidie, nitamsaidia, ila kwa nini hata nimpe pesa kiasi gani, daima anataka zaidi? Ni kwa nini asifanye kazi halali, lakini atafanya chochote—kuzurura, kula, kunywa, kuzini, na kucheza kamari? Nini kinaendelea?” Halafu Zhang anafikiria kidogo: “Inaweza kuwa ni kwa sababu nilikuwa na deni lake katika maisha ya zamani. Sawa basi, nitalilipa! Haya hayataisha hadi nilipe kikamilifu!” Inaweza kufika siku ambayo Li anafidia deni lake, na akiwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, itafika siku ambayo atajitambua: “Sijafanya kitu kizuri hata kimoja katika hii nusu ya kwanza ya maisha yangu! Nimefuja pesa zote alizozipata baba—ninapaswa kuwa mtu mwema! Nitajikakamua: nitakuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na anayeishi ipasavyo, na sitamletea babangu huzuni tena!” Kwa nini anafikiria hivi? Mbona anageuka kuwa mwema ghafla? Kuna sababu ya hili? Ni sababu gani? (Kwa sababu Li amepokea deni lake; Zhang amelipa deni lake.) Katika hili, kuna chanzo na matokeo. Kisa kilianza zamani sana, kabla hawa wawili hawajazaliwa, na hiki kisa cha maisha yao ya zamani kimeletwa katika maisha yao ya sasa, na hakuna anayeweza kumlaumu mwingine. Haijalishi Zhang alimfundisha nini mwanake, mwanake hakumsikiliza, na hakufanya kazi halali hata ya siku—lakini siku ambayo deni lilipwa, hapakuwa na haja ya kumfundisha; mwanake alielewa kiasili. Huu ni mfano rahisi. Kuna mifano mingine mingi kama huu? (Ndiyo.) Na unawafunza watu kitu gani? (Wanapaswa kuwa wema na hawapaswi kutenda maovu.) Kwamba hawapaswi kutenda maovu, na kutakuwa na adhabu kwa maovu yao! Wengi wa wasioamini, hutenda maovu mengi na utendaji maovu wao umekutwa na adhabu, sawa? Je, hii adhabu ni ya kinasibu? Kila linalokutwa na adhabu lina asili na sababu. Unadhani hakuna litakalotendeka baada ya kumlaghai mtu pesa? Unadhani baada ya kuwatapeli pesa zao hakutakuwa na matokeo kwako baada ya kuchukua pesa zao? Hilo halitawezekana, na kutakuwa na athari! Bila kujali yeye ni nani, au kama anaamini ama haamini kuwa kuna Mungu, kila mtu ni lazima atawajibikia mienendo yake na kubeba matokeo ya matendo yake. Kwa kurejelea huu mfano rahisi—Zhang kuadhibiwa, na Li kulipwa—je hii si haki? Watu wakifanya vitu kama hivyo, kuna aina hiyo ya matokeo. Haitenganishwi na utawala wa ulimwengu wa kiroho. Licha ya kuwa wasioamini, wale wasiomwamini Mungu, uwepo wao uko chini ya amri za peponi na sheria ambazo haziwezi kuepukika na yeyote na hakuna mtu anayeweza kuuepuka ukweli huu.

Wale ambao hawana imani huamini kuwa kila kitu ambacho kinaweza kuonekana kipo, ilhali kila kitu kisichoonekana, au ambacho kiko mbali sana na watu, hakipo. Wanapenda kuamini kuwa hakuna “mzunguko wa uhai na mauti,” na hakuna “adhabu,” na kwa hiyo wanatenda dhambi na kufanya maovu bila majuto—ambayo baadaye wataadhibiwa kwayo, au watapata miili kama mnyama. Wengi wa watu mbalimbali miongoni mwa Wasioamini wanapatikana katika mzunguko huu. Ni kwa sababu hawajui kuwa ulimwengu wa kiroho ni mkali katika kuviendesha viumbe hai wote. Ikiwa unaamini au la, huu ukweli upo, na hakuna mtu hata mmoja au chombo chochote kinaweza kuepuka mawanda ya ambacho kinaonwa na macho ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja au chombo kinachoweza kuepuka sheria na mipaka ya sheria za peponi na amri za Mungu. Na hivyo basi mfano huu rahisi unamwambia kila mtu kwamba haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu, haikubaliwi kutenda dhambi na kufanya maovu, na kuna matokeo. Wakati mtu aliyemlaghai mwingine pesa anaadhibiwa hivyo, hiyo adhabu ni ya haki. Mienendo inayoonekana ya kawaida kama hii inaadhibiwa na ulimwengu wa kiroho, inaadhibiwa na amri na sheria za mbinguni za Mungu, na vivyo hivyo uhalifu mkubwa na matendo maovu—ubakaji na unyang’anyi, ulaghai na udanganyifu, wizi na ujambazi, mauaji na uchomaji, na kadhalika—yanapitia adhabu za aina zenye ukali wa viwango mbalimbali. Na hizi adhabu zenye ukali wa viwango mbalimbali zinajumuisha nini? Baadhi yake zinatumia muda kufikisha kiwango cha ukali, na nyingine hufikiwa kwa mbinu mbalimbali, na nyingi hufikiwa kupitia mahali mtu aendapo akipata mwili. Kwa mfano, watu wengine wana maneno machafu. Kuwa na “maneno machafu” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwaapiza wengine mara kwa mara, na kutumia lugha chafu, lugha inayowalaani watu wengine. Lugha yenye nia mbaya inaashiria nini? Inaashiria kuwa mtu ana roho mbaya. Lugha yenye nia mbaya inayowalaani watu wengine mara nyingi inatoka vinywani mwa watu kama hao, na lugha yenye nia mbaya kama hiyo mara nyingi inaandamana na matokeo makali. Baada ya hawa watu kufa na kupokea adhabu stahili, wanaweza kuzaliwa kama mabubu. Watu wengine ni wajanja sana wakiwa hai, mara kwa mara wanawatumia watu wengine kwa manufaa yao, njama zao huwa zimepangwa barabara, na wanafanya mengi yanayowadhuru wengine. Wakizaliwa upya, wanaweza kuwa wazimu au punguani. Watu wengine mara nyingi huwachungulia watu wengine wakiwa faraghani; macho yao huona mengi ambayo hawakutakiwa kuona, na hujua mengi ambayo hawakupaswa kujua, hivyo basi wazaliwapo upya, wanaweza kuwa vipofu. Watu wengine ni hodari sana wakiwa hai, wanapigana mara kwa mara, na kufanya mengi ambayo ni maovu, na kwa hiyo wanapozaliwa upya, wanaweza kuwa vilema au wakakosa mkono, vinginevyo wanaweza kuwa vibyongo, au wenye shingo iliyopinda, huenda wakatembea wakichechemea, au wakawa na mguu mmoja mfupi kuliko mwingine, na kadhalika. Katika hali hii, wanapewa adhabu mbalimbali kutegemea kiwango cha maovu waliyotenda walipokuwa hai. Mwasemaje, kuhusu ni kwa nini watu huwa na makengeza? Je, kuna watu wengi wa hivyo? Kuna wengi wao siku hizi. Watu wengine wana makengeza kwa sababu waliyatumia macho yao sana katika maisha yao yaliyopita, walifanya mambo mengi mabaya, na kwa hiyo wazaliwapo katika haya maisha macho yao hupata makengeza, na katika hali mbaya, hata huwa vipofu. Haya ni malipo! Watu wengine wanaelewana vizuri na wengine kabla hawajafa, wanafanya mambo mengi mazuri kwa wapendwa wao, marafiki, wenza, au watu wanaohusiana nao. Wanatoa hisani na matunzo kwa wengine, au kuwasaidia kifedha, wengine wanawaheshimu sana, na watu kama hao warudipo katika ulimwengu wa kiroho hawaadhibiwi. Kwa asiyeamini kukosa kuadhibiwa kwa njia yoyote inamaanisha alikuwa mtu mzuri sana. Badala ya kuamini katika uwepo wa Mungu, wanaamini tu katika Mzee aliye Angani. Wanaamini tu kuwa kuna roho juu yao akitazama yote wafanyayo—hayo tu ndiyo wanaamini. Na matokeo ni kwamba wanakuwa na mwenendo mzuri zaidi. Hawa watu ni wenye huruma na wakarimu, na mwishowe wakirudi katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapokea vizuri sana na watapata mwili na kuzaliwa upya mapema. Wanapozaliwa tena, watafikia katika familia za aina gani? Japo familia yake haitakuwa ya kitajiri, itakuwa tulivu, kutakuwa na maelewano miongoni mwa wanafamilia, watakuwa na siku mwanana, za kupendeza, kila mmoja atafurahia, na watakuwa na maisha mazuri. Naye atakapokuwa mtu mzima, atakuwa na familia kubwa na jamaa wengi, watoto wake watakuwa na vipawa na kufanikiwa, na familia yake watakuwa na bahati nzuri—na matokeo kama hayo yanahusiana kwa kiasi kikubwa na maisha ya zamani ya mtu. Yaani, mahali mtu huenda baada ya kufa na kupata mwili, wawe wanaume au wanawake, wito wao ni upi, watapitia nini maishani, vikwazo vyao, watapata baraka gani, watakutana na nani, ni nini kitawatokea—hakuna awezaye kulitabiri hili, kuliepuka, au kujificha kutokana nalo. Yaani, baada ya maisha yako kupangwa, kitakachokutokea, hata ujaribu namna gani kukikwepa, hata ukitumia mbinu gani kukiepuka, huna njia ya kuvuruga mkondo wa maisha uliopangiwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Kwani upatapo mwili, majaaliwa yako tayari huwa yameishapangwa, ikiwa yatakuwa mazuri au mabaya, kila mtu anapaswa kuyakubali yalivyo, na anapaswa kusonga mbele; hili ni jambo ambalo hakuna mtu aishiye katika maisha haya anaweza kuliepuka, na huu ndio uhalisia. Sawa, umeyaelewa haya yote, naam?

Baada ya kulielewa hili, mnaona kwamba Mungu ana uangalizi unaolipiza sana na mkali pamoja na utawala kwa mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini? Kwanza, Mungu ameweka sheria mbalimbali za mbinguni, amri, na mifumo katika milki ya kiroho, na baada ya kutangazwa kwa hizi sheria za mbinguni, amri na mifumo, ambazo zinatekelezwa kabisa, kama zilivyopangwa na Mungu, na viumbe wenye nyadhifa rasmi mbalimbali katika ulimwengu wa kiroho, na hakuna anayethubutu kuzikiuka. Na kwa hivyo, katika Mzunguko wa uhai na mauti wa wanadamu katika dunia ya mwanadamu, mtu awe amepata mwili kama mwanadamu au mnyama, kuna sheria kwa yote mawili. Kwa kuwa sheria hizi zinatoka kwa Mungu, hakuna anayethubutu kuzivunja, wala hakuna awezaye kuzivunja. Ni kwa sababu tu ya huo ukuu wa Mungu, na kwa sababu kuna sheria hizo, ndiyo ulimwengu yakinifu uonekanao kwa mwanadamu ni wa kawaida na wenye mpangilio; ni kwa sababu tu ya ukuu wa Mungu ndipo mwanadamu anaweza kuishi kwa amani pamoja na ulimwengu mwingine ambao hauonekani kabisa kwa mwanadamu, na kuweza kuishi nao kwa amani—vitu ambavyo vyote haviwezi kutenganishwa na mamlaka ya Mungu. Baada ya maisha ya mtu ya kimwili kufa, roho bado huwa na uhai, basi ni nini kingetendeka ikiwa roho ingekosa utawala wa Mungu? Roho ingezurura kila mahali, ikiingia kila sehemu, na hata kudhuru viumbe hai katika ulimwengu wa wanadamu. Madhara hayo hayangekuwa tu kwa mwanadamu bali pia kwa mimea na wanyama—ila wa kwanza kudhuriwa wangekuwa watu. Kama hili lingetukia—roho kama hiyo ingekosa uendeshaji, na kuwadhuru watu kwa hakika, na kufanya mambo maovu kwa hakika—basi pia kungekuwa na ushughulikiaji ufaao wa roho hii katika ulimwengu wa kiroho: Ikiwa mambo yangekuwa mabaya, roho haingeendelea kuwepo, ingeangamizwa; ikiwezekana, ingewekwa mahali fulani halafu ipatiwe mwili. Yaani, utawala wa ulimwengu wa kiroho kwa roho mbalimbali umepangiliwa, na kutekelezwa kulingana na hatua na sheria. Ni kwa sababu tu ya utawala huo ndiyo ulimwengu yakinifu wa mwanadamu haujatumbukia kwenye machafuko, ndiyo mwanadamu wa ulimwengu wa kuonekana ana akili ya kawaida, urazini wa kawaida, na maisha ya kimwili yenye mpangilio. Ni baada tu ya mwanadamu kuwa na maisha ya kawaida ndiyo wale wanaoishi katika mwili wanaweza kuendelea kufanikiwa na kuzaana katika vizazi vyote.

… Ikija kwa wasioamini, je, kanuni iongozayo matendo ya Mungu ni ile ya kutuza mazuri na kuadhibu mabaya? Kuna upekee wowote? (La.) Je, mnaona kwamba kuna kanuni katika matendo ya Mungu? Wasioamini kwa hakika hawamwamini Mungu, hawatii mipango ya Mungu, na hawafahamu ukuu wa Mungu, na hawamtambui Mungu hata kidogo. Zito zaidi, wanamkufuru Mungu, na kumlaani, na ni mahasimu wa wale wanaomwamini Mungu. Japo watu hawa wana mwelekeo huo kwa Mungu, bado uongozi wa Mungu kwao hauachani na kanuni Zake; Anawaongoza kwa njia ya utaratibu kulingana na kanuni Zake na tabia Yake. Je, Mungu anauchukuliaje uhasama wao? Kama ujinga! Na kwa hiyo Amewasababisha hawa watu—wengi wa wasioamini—wakati mmoja kuwahi kupata mwili kama wanyama. Basi wasioamini ni nini machoni mwa Mungu? Wao ni mifugo. Mungu anaongoza mifugo na kwa watu kama hao Ana kanuni sawa. Hata kwa utawala wa Mungu kwa watu hawa, tabia Yake kwao, bado inaweza kuonekana, kama inavyowezekana sheria Zake kama chanzo cha utawala Wake juu ya vitu vyote. Hivyo basi, unaona mamlaka ya Mungu katika kanuni ambazo kwazo Anawaongoza wasioamini ambao Nimezungumzia hivi punde? Je, mnaona tabia ya haki ya Mungu? (Tunaona.) Yaani, haijalishi Anashughulikia kitu gani kati ya vitu vyote Anavyoshughulikia, Mungu anatenda kulingana na kanuni na tabia Yake. Hiki ndicho kiini cha Mungu. Hangeweza kujitenga kiholela na amri au sheria za mbinguni Alizozipanga kwa sababu Anamwona mtu wa aina hii kama mfugo. Mungu anatenda kulingana na kanuni, bila kuzivuruga hata kidogo, matendo Yake hayaathiriwi na jambo lolote, na haijalishi Anafanya nini, yote ni kulingana na kanuni Zake mwenyewe. Hili ni kwa sababu Mungu ana kiini cha Mungu Mwenyewe, ambacho ni kipengele cha kiini Chake ambacho hakimo kwenye kiumbe yeyote. Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili. Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu.

Kifo cha kiumbe hai—kuondokewa na uhai wa kimwili—kinaashiria kwamba kiumbe hai huyu ametoka katika ulimwengu yakinifu hadi ulimwengu wa kiroho, ilhali kuzaliwa kimwili kunaashiria kwamba kiumbe hai ametoka ulimwengu wa kiroho na kuja ulimwengu yakinifu kuanza kufanya kazi yake, kuchukua nafasi yake. Iwe ni kuondoka au kuwasili kwa kiumbe, vyote havitenganishwi na kazi ya ulimwengu wa kiroho. Mtu akija katika ulimwengu yakinifu, mipango kabambe na fafanuzi huwa tayari imetengenezwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho kuhusu atakwenda katika familia gani, atafikia enzi gani, atawasili saa ngapi, na nafasi yake. Hivyo basi, maisha yote ya mtu huyu—mambo afanyayo, na njia azichukuazo—yanasonga kulingana na mipango ya ulimwengu wa kiroho, bila hitilafu hata kidogo. Wakati ambapo maisha ya kiroho yanaisha, wakati huo, na namna na mahali ambapo yanaishia, ni wazi na yanaonekana katika ulimwengu wa kiroho. Mungu anatawala ulimwengu yakinifu, na Anatawala ulimwengu wa kiroho, na Hawezi kuchelewesha mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti wa roho, wala Hawezi kufanya makosa katika mpangilio wa mzunguko wa uhai na mauti wa roho. Kila msimamizi katika nyadhifa rasmi katika ulimwengu wa kiroho anafanya majukumu yake na kufanya ambacho anapaswa kufanya, kulingana na maelezo na sheria za Mungu. Na kwa hiyo, katika ulimwengu wa wanadamu, kila tukio la kuonekana lishuhudiwalo na binadamu lina utaratibu, na halina vurugu yoyote. Haya yote ni kwa sababu ya utawala uliopangiliwa wa Mungu juu ya vitu vyote, hali kadhalika kwa sababu mamlaka ya Mungu yanatawala kila kitu, na kila kitu Anachokitawala kinajumuisha ulimwengu yakinifu ambamo mwanadamu anaishi, aidha, ulimwengu wa kiroho usioonekana nyuma ya mwanadamu. Na kwa hiyo, ikiwa mwanadamu anataka kuwa na maisha mazuri, na anataka kuishi katika mazingira mazuri, hali kadhalika kupewa ulimwengu yakinifu mzima, mwanadamu sharti pia apatiwe ulimwengu wa kiroho, ambao hauwezi kuonekana kwa yeyote, ambao unaongoza kila kiumbe hai kwa niaba ya mwanadamu, na ambao una utaratibu. Basi, inaposemwa kwamba Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote, je, hatujakuza ufahamu na uelewa wetu wa “vitu vyote”? (Ndiyo.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ulimwengu wa kiroho ni nini?

Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp