Ulimwengu wa kiroho ni nini?

10/09/2019

Ulimwengu wa kiroho ni nini?

Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia mbalimbali kubaini asili ya habari kuvihusu. Lakini inapokuja kwa ulimwengu huu mwingine ambao tunauzungumzia leo—ulimwengu wa kiroho ulio nje ya ulimwengu yakinifu—watu hawana hasa mbinu au njia za kujifunzia chochote kuuhusu. Mbona Ninasema hivi? Kwa sababu, katika ulimwengu wa mwanadamu, kila kitu cha ulimwengu yakinifu hakijitengi na uwepo wa kimwili wa mwanadamu, na kwa sababu watu wanahisi kwamba kila kitu katika ulimwengu yakinifu hakitenganishwi na maisha yao ya kimwili na uhai wao wa kimwili, watu wengi wanafahamu tu kuhusu, au kuona, vitu yakinifu mbele ya macho yao, vitu vinavyoonekana kwao. Bali inapokuja katika ulimwengu wa kiroho—yaani, kila kilicho cha ule ulimwengu mwingine—ni haki kusema kuwa watu wengi hawaamini. Kwa sababu watu hawawezi kuuona, wanaamini kuwa hakuna haja ya kuuelewa au kujua kitu chochote kuuhusu, sembuse jinsi ulimwengu wa kiroho ni ulimwengu tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu na kutoka kwa mtazamo wa Mungu, uko wazi—ingawa kwa wanadamu, ni wa siri na umefungwa—kwa hivyo watu huona ikiwa vigumu sana kupata njia ya kuelewa vipengele mbalimbali vya ulimwengu huu. Vipengele tofauti ambavyo nitazungumzia kuhusu ulimwengu wa kiroho vinahusu utawala na ukuu wa Mungu tu. Sifichui miujiza, wala Siwaambii siri zozote mnazotaka kugundua, kwani hili linahusu ukuu wa Mungu, utawala wa Mungu, na riziki ya Mungu, na kwa hivyo Sitazungumzia tu sehemu ambayo ni muhimu nyinyi kuijua.

Kwanza, hebu Niwaulize swali: katika mawazo yenu, ulimwengu wa kiroho ni nini? Kuzungumza kwa ujumla, ni ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu, ambao hauonekani na haushikiki na watu. Lakini kwa fikra zenu, ulimwengu wa kiroho unafaa uwe ulimwengu wa aina gani? Pengine, kwa sababu ya kutoweza kuuona, mnaweza kushindwa kuufikiria. Lakini mtakaposikia hadithi kuuhusu, bado mtafikiri, hamtaweza kujizuia nyinyi wenyewe. Na kwa nini Ninasema hili? Kuna kitu kinachowatokea watu wengi wanapokuwa wachanga: mtu akiwasimulia hadithi ya kuogofya—juu ya mazimwi, na roho—wanaogopeshwa kabisa. Na kwa nini wanaogopeshwa? Ni kwa kuwa wanavifikiria vitu hivyo; hata japo hawawezi kuviona, wanahisi kuwa vipo kila pembe ya chumba chao, vimejificha sehemu fulani, au sehemu fulani yenye giza, na wanaogopa sana kiasi kwamba hawawezi kuthubutu kulala. Hasa wakati wa usiku, hawathubutu kuwa chumbani peke yao, au uani peke yao. Huo ndio ulimwengu wa kiroho wa fikra zenu, na ni ulimwengu ambao watu hudhani unaogofya. Kwa kweli, kila mtu ana fikra fulani, na kila mtu anaweza kuhisi kitu.

Hebu tuanze na ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho ni nini? Hebu Niwape maelezo mafupi na rahisi. Ulimwengu wa kiroho ni sehemu muhimu, ambayo ni tofauti na ulimwengu yakinifu. Na mbona Ninasema kwamba ni muhimu? Tutalizungumzia hili kwa kina. Uwepo wa huu ulimwengu wa kiroho umeungana na ulimwengu yakinifu wa mwanadamu kwa njia isiyoweza kufumbulika. Una jukumu katika mzunguko wa uhai na mauti wa mwanadamu katika utawala wa Mungu juu ya vitu vyote; hili ndilo jukumu lake, na sababu mojawapo inayofanya uwepo wake kuwa muhimu. Kwa sababu ni mahali ambapo hapawezi kutambuliwa kwa milango mitano ya fahamu ya mwanadamu, hakuna anayeweza kubaini kwa hakika kuwepo au kutokuwepo kwake. Shughuli za ulimwengu wa kiroho zimeunganika kikamilifu na uwepo wa mwanadamu, na kwa sababu hiyo mpango wa maisha ya wanadamu pia unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na ulimwengu wa kiroho. Je, hili linahusiana na ukuu wa Mungu? Linahusiana. Nisemapo hili, unaelewa ni kwa nini Ninajadili mada hii; Kwa sababu inahusu ukuu wa Mungu, na utawala Wake. Katika ulimwengu kama huu—ulimwengu ambao hauonekani kwa watu—kila sheria yake ya peponi, amri na mfumo wake wa utawala ni wa juu zaidi kuliko sheria na mifumo ya nchi yoyote katika ulimwengu yakinifu, na hakuna kiumbe aishiye katika ulimwengu huu anaweza kuzivunja au kujitwalia bila haki. Je, hili linahusiana na ukuu na utawala wa Mungu? Katika ulimwengu huu kuna amri wazi za utawala, sheria wazi za mbinguni, na masharti wazi. Katika viwango tofauti na katika mawanda tofauti, wasimamizi huzingatia kikamilifu katika wajibu wao na kufuata sheria na masharti, kwa kuwa wanajua matokeo ya kukiuka sheria ya mbinguni ni yapi, wanafahamu wazi jinsi ambavyo Mungu anaadhibu maovu na kutuza mazuri, na kuhusu jinsi Anavyoviendesha vitu vyote, jinsi Anavyotawala vitu vyote, na zaidi, wanaona wazi ni jinsi gani Mungu anaendesha sheria za mbinguni na masharti Yake. Je, hizi ni tofauti na ulimwengu yakinifu unaokaliwa na wanadamu? Ni tofauti kwa kiasi kikubwa. Ni ulimwengu ambao ni tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu. Kwa kuwa kuna sheria na masharti ya mbinguni, inahusu ukuu wa Mungu, utawala, aidha, tabia ya Mungu ya kile Anacho na alicho. Baada ya kusikia hili, hamhisi kwamba ni muhimu sana Mimi kuzungumzia hii mada? Hamtaki kujifunza siri zilizomo? (Ndiyo, tunataka.) Hiyo ndiyo dhana ya ulimwengu wa kiroho. Japo unapatikana sambamba na ulimwengu yakinifu, na wakati ule ule ukiwa chini ya utawala na ukuu wa Mungu, utawala na ukuu wa Mungu ya huu ulimwengu ni makali zaidi kuliko ulivyo ulimwengu yakinifu. Ikija katika maelezo, tunafaa tuanze na jinsi ulimwengu wa kiroho unawajibikia kazi ya mzunguko wa uhai na mauti ya mwanadamu, kwa kuwa kazi hii ni sehemu kuu ya viumbe wa ulimwengu wa kiroho.

Miongoni mwa wanadamu, Ninawaainisha watu katika aina tatu. Aina ya kwanza ni wasioamini, wale wasio na imani za kidini. Wanaitwa wasioamini. Wengi wa wasioamini wanaamini tu katika pesa, wanatafuta tu maslahi yao wenyewe, wana tamaa ya vitu, na wanaamini katika ulimwengu yakinifu, si katika mzunguko wa uhai na mauti au katika semi za miungu na mapepo. Ninawaainisha kama wasioamini na ni wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni watu mbalimbali wenye imani tofauti na wasioamini. Miongoni mwa wanadamu, Ninawagawa hawa wenye imani katika aina kuu kadhaa: Ya kwanza ni Wayahudi, wa pili ni Wakatoliki, ya tatu ni Wakristo, ya nne ni Waislamu, na ya tano ni wafuasi wa Budha—kuna aina tano. Hizi ndizo aina mbalimbali za watu wenye imani. Aina ya tatu ni wale wanaomwamini Mungu, inayohusiana nanyi. Waumini kama hawa ni wale wanaomfuata Mungu leo. Hawa watu wamegawanyika katika aina mbili. Wateule wa Mungu na watendaji huduma. Hizi aina kuu zimebainishwa wazi. Basi sasa, akilini mwenu mnaweza kutofautisha wazi aina na madaraja ya binadamu, siyo? Ya kwanza ni wasioamini—nimesema wasioamini ni watu gani. Je, wale wanaomwamini Mtu Mzee aliye Angani wanahesabika kama wasioamini? Wengi wa wasioamini wanamwamini yule Mzee aliye Angani; wanaamini kuwa upepo, mvua na radi, na kadhalika vyote vinadhibitiwa na huyu mtu ambaye wanamtegemea kwa upanzi wa mimea na uvunaji wa mazao—lakini wakati imani katika Mungu inatajwa, hawataki kumwamini. Je, hii yaweza kuitwa imani katika Mungu? Watu kama hao wanahesabiwa katika wasioamini. Mnaelewa hili, siyo?—Msifahamu visivyo vikundi hivi. Aina ya pili ni watu wa imani. Aina ya tatu ni wale wanaomfuata Mungu leo. Na kwa nini Nimewagawa wanadamu wote katika aina hizi? (Kwa sababu aina kadhaa za watu wana vituo na hatima tofautitofauti.) Hicho ni kipengele kimoja. Kwa sababu, wakati haya matabaka na aina mbalimbali za watu wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, kila mmoja atakuwa na sehemu tofauti ya kuenda, watapitia sheria ya mzunguko tofauti wa uhai na mauti na hii ndiyo sababu Nimewaainisha wanadamu katika hizi aina kuu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp