Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi huwahubiria waumini kwamba mahubiri yoyote yanayosema kwamba Bwana amekuja katika mwili ni uongo. Wao hutegemeza hili aya za Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Sasa hatuna habari tunavyofaa kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa uongo, hivyo tafadhali jibu swali hili.

07/06/2019

Jibu:

Bwana Yesu kweli alitabiri kwamba kungekuwa na Kristo wa uongo na manabii wa uongo katika siku za mwisho. Huu ni ukweli. Lakini Bwana Yesu pia alitabiri wazi mara nyingi kwamba Atarudi. Hakika tunaamini hivyo? Wakati wa kuchunguza unabii wa Bwana Yesu kurudi, watu wengi huupa kipaumbele wasiwasi wao wa Kristo wa uongo na manabii wa uongo. na kutotilia maanani jinsi ya kukaribisha kuwasili kwa bwana harusi, na jinsi ya kusikia sauti ya bwana harusi. Suala ni lipi hapa? Je, si hili ni jambo la kula kwa hofu ya kusongwa, ya kuwa mwenye busara katika umaskini na kuwa mjinga utajirini? Kwa kweli, bila kujali jinsi watu tunavyojihadhari dhidi ya Makristo wa uongo na manabii wa uongo, kama tusipokaribisha kurudi kwa Bwana, na hatuwezi kuelekwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, sisi ni mabikira wapumbavu ambao wanaondolewa na kuachwa na Mungu, na imani yetu katika Bwana ni ya kushindwa kabisa! Cha msingi kuhusu kama au la tunaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana ni kama au la tuna uwezo wa kusikia sauti ya Mungu. Mradi tunatambua kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima, hatutakuwa na ugumu katika kutambua sauti ya Mungu. Kama hatuwezi kutambua ukweli, na tunalenga tu juu ya ishara na maajabu ya Mungu, basi hakika tutadanganywa na Makristo wa uongo na manabii wa uongo. Kama hatutatafuta na kuchunguza njia ya kweli, basi kamwe hatutaweza kusikia sauti ya Mungu. Je, si tunasubiri kifo, na kuleta maangamizo yetu wenyewe? Tunaamini kuwa kwa maneno ya Bwana, kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Wale ambao kweli wana ubongo, na ubora wa tabia, na wanaweza kusikia sauti ya Mungu hawatadanganywa na Makristo wa uongo na manabii wa uongo. Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo hawana ukweli, na hawawezi kufanya kazi ya Mungu. Hiki si kitu tunachohitaji kuwa na wasiwasi nacho. Ni wale tu ambao wamechanganyikiwa na hawana akili wanaoweza kudanganywa na Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Wanawali werevu hawatadanganywa na Kristo wa uongo na manabii wa uongo, kwa sababu wana utunzaji wa Mungu na ulinzi. Wakati Mungu alipomuumba mwanadamu, wanawali werevu walipewa roho za binadamu na walikuwa na uwezo wa kusikia sauti ya Mungu. Na kwa hivyo kondoo wa Mungu husikia sauti Yake, ambayo imeamuliwa na Mungu. Ni wanawali wapumbavu tu Ambao hujishughulisha kwa kuhadhari dhidi ya Kristo wa uongo na manabii wa uongo, na kutelekezwa kutafuta na kuchunguza kurudi kwa Bwana. Kama tunataka kukaribisha kurudi kwa Bwana, na kutodanganywa na Kristo wa uongo na manabii wa uongo, basi ni lazima kuelewa jinsi Kristo wa uongo huwadanganya watu. Kwa kweli, Bwana Yesu tayari ametuambia kuhusu matendo ya Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Bwana Yesu alisema, “Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:24). Maneno ya Bwana Yesu yatuonyesha kwamba Kristo wa uongo na manabii wa uongo hasa hutegemea kufanya miujiza na maajabu ili kuwadanganya watu wa Mungu waliochaguliwa. Hili ndilo dhihirisho kuu la udanganyifu wa Kristo wa uongo kwa watu. Katika hili, ni lazima tuelewe kwa nini Kristo wa uongo hutumia ishara na miujiza kuwadanganya watu. Zaidi ya yote, ni kwa sababu Kristo wa uongo na manabii wa uongo hawana ukweli kabisa. Katika asili na kiini, wao ni pepo waovu sana. Na hivyo ni lazima wategemee ishara na maajabu kuwadanganya watu. Kama Kristo wa uongo na manabii wa uongo wangekuwa na ukweli, hawangetumia ishara na maajabu kuwadanganya watu. Liangalie jambo hilo kwa njia hii, Kristo wa uongo na manabii wa uongo hufanya ishara na maajabu kwa sababu hicho tu ndicho kitu wanachoweza kufanya. Kama hatuwezi kuona hili, basi itakuwa ni rahisi sana kwao kutudanganya. Kristo pekee ndiye ukweli, njia na uzima. Yule anayeweza kueleza ukweli, na kuonyesha watu njia, na kuwapa uzima ni Yule ambaye ni Kristo. Wale ambao wanajiita Kristo, lakini hawawezi kueleza ukweli, hakika ni Makristo wa uongo; wao ni bandia. Hii ndiyo kanuni ya msingi ya kuwatambua Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Wale wote ambao wanatafuta na kuchunguza njia ya kweli wanapaswa kuzingatia kanuni hii kuitafuta na kuihakikisha sauti ya Mungu. Na katika hili wao hawafanyi kosa.

Mwenyezi Mungu tayari ameweka wazi matendo ya Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Hebu tusome kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema, hatua ya kwanza katika kazi ya ukombozi, na sasa kwa kuwa Mungu Amemkomboa mwanadamu kutoka msalabani, Hatekelezi kazi hiyo kamwe. Ikiwa katika siku za mwisho ‘Mungu’ sawa na Yesu Angeonekana, Ambaye Anaponya wagonjwa, Anafukuza mapepo na Anayesulubiwa kwa ajili ya wanadamu, ‘Mungu’ huyo, japo Analingana na maelezo ya Mungu katika Biblia, na rahisi kwa mwanadamu kukubali, Hangeweza, katika kiini chake, kuwa mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu, bali na roho mwovu. Kwani ni kanuni ya kazi ya Mungu kutorudia Alichokikamilisha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu). “Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo). “Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanatuambia wazi kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe hazeeki, na kamwe hafanyi kazi ya aina moja. Hii ni kama tu wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi: Aliikaribisha Enzi ya Neema, na kuihitimisha Enzi ya Sheria. Alifanya hatua moja ya kazi ya ukombozi, na kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi. Ili kazi Yake iwe ya kufaa, Alitekeleza ishara na maajabu kadha. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amekuja, Ameikaribisha Enzi ya Ufalme, na kuihitimisha Enzi ya Neema. Lakini Yeye huwa harudii kazi iliyofanywa na Bwana Yesu. Badala yake, katika msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Yeye hufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Yeye huonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu, Ili kutatua chanzo cha dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya kishetani, na kumwokoa mwanadamu kabisa kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ili kwamba mwanadamu hatimaye apatwe na Mungu. Na Kristo wa uongo? Wote ni pepo wabaya ambao humwigiza Kristo. Hawana uwezo wa kufanya kazi ya kukaribisha enzi mpya na kuhitimisha enzi nzee. Wanaweza tu kumwigiza Bwana Yesu na kufanya baadhi ya ishara rahisi na maajabu kuwadanganya wale ambao wamevurugika na wasioweza kung’amua. Lakini hawana uwezo wa kuiga yale Bwana Yesu alifanya kama kufufua wafu na kulisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, au kukemea upepo na bahari. Hayo yako nje ya uwezo wao. Katika kiini, Kristo wa uongo ni waovu, hao ni pepo wabaya, na hawana ukweli kabisa. Na hivyo, ni lazima wategemee ishara na maajabu ili kuwadanganya watu. La sivyo wao huwadanganya na kuwaasa watu kwa kuiga sauti ya maneno ya Mungu na maneno sahili ambayo wakati fulani yalizungumzwa na Mungu.

Kuhusiana na ukweli kuhusu jinsi ya kujua tofauti kati wa Kristo ya kweli na Kristo wa uongo hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaweza kuona wazi kwamba Kristo ni Mungu aliyepata mwili, Yeye ni Roho wa Mungu aliyepata katika mwili. Hivyo ni kusema, yote ambayo Mungu anamiliki, ikiwa ni pamoja na kile Mungu anacho na alicho, tabia ya Mungu, na hekima ya Mungu vyote vimeonekana katika mwili Wake. Ndiyo. Kristo ana kiini cha uungu, na ni mfano halisi wa ukweli. Yeye ana uwezo wa kuonyesha ukweli wa kumruzuku mwanadamu, na kumtunza mwanadamu, siku zote, katika maeneo yote. Ni Kristo tu ndiye anayeweza kufanya kazi ya kuwakomboa watu na kuwaokoa wanadamu. Hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuiga haya, wala hawawezi kukana jambo hilo. Wengi wa Kristo wa uongo, wakati huo huo, wamepagawa na pepo wachafu. Wao wana kiburi kikubwa na dhihaka. Katika kiini, wao ni pepo wachafu na mashetani. Hivyo, bila kujali ni ishara gani na maajabu gani wao hufanya, au jinsi wanavyotafsiri Biblia vibaya, au wanavyozungumza juu ya elimu ya kina na nadharia, hawafanyi lolote ila kuwadanganya watu, na kuwadhuru, na kuwaleta katika maangamizi. Hakuna wanalolifanya ambalo linaadilisha watu. Kila wanachofanya ni kuleta giza daima kwa nyoyo za watu, wanawaacha bila njia ya kutembea, ili wamezwe hatimaye na Shetani. Inaweza kuonekana kwamba Kristo wote wa uongo na manabii wa uongo ni kupata mwili kwa Shetani, ni pepo wabaya ambao wamekuja kuipinga na kuivuruga kazi ya Mungu. Bila kujali ni watu wangapi wanaowadanganya, kuwadhuru, au kuwaleta katika maangamizi, hivi karibuni wataanguka, na kujiangamiza wenyewe, maana hawana hata chembe ya ukweli. Kama kweli tunaelewa ukweli kuhusu jinsi ya kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Kristo wa uongo, basi hakuna jinsi tunaweza kukataa kuisikia sauti ya Mungu au kukaribisha kuonekana kwa Mungu kwa hofu ya kudanganywa na Makristo wa uongo.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tangu Mwenyezi Mungu alipoanza kuonyesha ukweli ili kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, mwanadamu tayari ameingia katika Enzi ya Ufalme na Enzi ya Ufalme imeanza. Ikiwa imani yetu katika Mungu imesalia imekwama katika Enzi ya Neema, basi tumeachwa nyuma na kutengwa na kazi ya Mungu. Wakati Bwana atawasili kisiri ili kufanya kazi Yake ya hukumu ambayo inaanzia kwa nyumba ya Mungu, bila shaka kutakuwa na Makristo wengi wa uongo na watu wadanganyifu ambao watatokea wakati ule ule wakifuatilia kazi ya Mungu na kuivuruga. Kwa hivyo, Makristo wa uongo wanapoonekana, Mungu kwa hakika tayari amekuja na kuwasili kisiri. Ni vile tu hatulijui. Kwa wakati huu, tunapaswa kutafuta na kuchunguza kwa bidii kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini sasa bado kuna watu wengi ambao, kuhusiana na kuja kwa Bwana kwa mara ya pili, wangali wanachukulia kukinga dhidi ya Makristo wa uongo kuwa ndilo jambo lenye umuhimu mkubwa zaidi, badala ya kuzingatia jinsi ya kuwa wanawali werevu na kusikiliza sauti ya Mungu kuhusu jinsi ya kupokea kuja kwa Bwana kwa mara ya pili. Badala yake, wanashikilia dhana na fikra zao, wakifikiri kuwa ushuhuda wote wa kurudi kwa Bwana Yesu kupitia kupata mwili ni uongo. Je, si wao hasa ndio wanawali wajinga ambao Bwana Yesu alizungumzia kuhusu? Je, huku sio kushutumu Bwana Yesu aliyerudi? Je, watu hawa hata huamini katika kurudi kwa Bwana Yesu? Je, si huku ni kukana kurudi kwa Bwana Yesu kwa mara ya pili?

Jinsi mtu anavyotofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo kunaonyesha kwa hakika iwapo ana ukweli au hana ukweli, na ndiyo njia bora zaidi ya kuonyesha iwapo yeye ni mwanamwali mwerevu au mjinga. Watu wengine hutumia kifungu hiki cha maandiko kama msingi wa kuhukumu na kushutumu Kristo mwenye mwili na kukana kuwasili kwa Kristo. Watu hawa wamejionyesha wenyewe kuwa wajinga. Ili kutofautisha baina ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo, ni lazima kwanza mtu awe na ufahamu wa kiini cha Kristo. Kila mmoja anajua kwamba Bwana Yesu ndiye Kristo katika mwili na Kristo ni Mungu mwenye mwili, yaani, Mungu akiwa mbinguni akifanyika mwili kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Kristo ni Roho wa Mungu mwenye mwili na ana kiini cha uungu. Uweza na hekima ya Mungu, tabia ya Mungu, na miliki na nafsi ya Mungu ambayo Roho wa Mungu anayo yote yamejidhihirisha ndani ya Kristo. Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Hivyo tunaweza kuwa na uhakika kuwa Kristo sio Mungu asiye yakini, sio wa kubuni wala asiye halisi. Kristo ni halisi na wa vitendo; Anaweza kutegemewa na kuaminiwa na mwanadamu. Kristo ndiye Mungu wa vitendo ambaye anaweza kufuatwa na kujulikana. Ni kama tu Bwana Yesu kuishi waziwazi miongoni mwa wanadamu, akifanya kazi na kumuongoza mwanadamu, na kumchunga mwanadamu. Kwa maana sasa tunajua kiini cha Kristo, kutofautisha baina ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo kunakuwa rahisi sana. Hebu tuone kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Wakati Bwana Yesu alipokuja katika ile Enzi ya Neema, Alisema: “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai(Yohana 14:6). Bwana Yesu alionyesha ukweli mwingi, alionyesha tabia ambayo hasa ni rehema na huruma, na kukamilisha kazi ya Mungu ya kukomboa wanadamu wote. Kazi ya Bwana Yesu, matamshi na tabia Aliyoonyesha inathibitisha kikamilifu kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Katika zile siku za mwisho, Mwenyezi Mungu alikuja na kusema: “Maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia….(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 12). Mwenyezi Mungu alionyesha maneno milioni kadhaa na kufungua kitabu, akionyesha tabia ambayo hasa ni ya haki na kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Kazi ya Mwenyezi Mungu ya kuhukumu na kutakasa, na kuokoa wanadamu waliopotoka kwa mara nyingine tena inathibitisha kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Bwana Yesu alikuwa ametabiri zamani kuwa Atarudi kufanya kazi ya hukumu katika zile siku za mwisho, na kwamba Atafanya hivyo katika mwili kama Mwana wa Adamu, akija kwa ulimwengu wa mwanadamu akiwa na sura ya Mwana wa Adamu na kuzungumza na makanisa. Kazi ya Mwenyezi Mungu imetimiza unabii wa kuja kwa Bwana Yesu kwa mara ya pili. Hili limetuwezesha kuona kuwa Kristo wa kweli katika mwili anaweza kuja kuonyesha ukweli na tabia ya Mungu, na anaweza kufanya kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho na anaweza kushinda, kuokoa, na kumtakasa mwanadamu, na vile vile kufanya mapenzi ya Mungu na kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Ukweli wote Anaoonyesha utashinda kwa hakika na kwa ukamilifu wanadamu wote wapotovu, na unaweza kuleta wale wote wanaomwamini Mungu kwa kweli mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Kristo bila shaka atakamilisha kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Hilo ni hakika.

Makristo wa uongo ni mapepo waovu wanaojifanya kuwa Makristo. Ni wadanganyifu. Makristo wengi wa uongo wamepagawa na roho waovu. Hata kama hawajapagawa na roho waovu, wao ni mapepo wabaya wenye kiburi kingi sana na wasio na akili. Hio ndio sababu wao hujifanya kuwa Makristo. Kujifanya kuwa Kristo ni kutenda dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu na bila shaka watalaaniwa. Kwa sababu kiini cha Makristo wa uongo ni mapepo waovu, Makristo wa uongo hawana ukweli wowote na kimsingi wao ni mapepo wabaya. Kwa hivyo, kila kitu kinachosemwa na Makristo wa uongo ni uongo na dhana zenye udanganyifu, zisizoweza kuwahakikishia watu. Hakuna chochote kinachosemwa au kufanywa na Makristo wa uongo kinaweza kustahimili uchunguzi wa makini, na zaidi hawawezi kujaribu kukiweka kwenye mtandao ili kuonekana na kuchunguzwa na wanadamu wote. Hii ni kwa sababu Makristo wa uongo na mapepo waovu ni miliki ya giza na uovu, na hawawezi kustahimili mwangaza wa mchana. Wanaweza tu kutegemea kufanya ishara na maajabu rahisi ili kuwadanganya wale watu wajinga na wapumbavu katika pembe zenye giza kila mahali. Hivyo, tunaweza kuwa na uhakika kuwa yeyote anayedai kuwa Kristo lakini hutegemea tu ishara na maajabu rahisi ili kuwadanganya watu ni Makristo wa uongo. Ukweli wote unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, umewekwa kwenye mtandao, ukionekana na wanadamu wote. Wale wote ambao humwamini Mungu kwa kweli na hupenda ukweli wote wanatafuta na kuchunguza njia ya kweli, mmoja kwa mmoja wakirudi mbele ya kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu ili kukubali hukumu, utakaso, na kufanywa kamili na maneno ya Mungu. Huu ni ukweli unakubalika. Kile kinachosemwa na kufanywa na Makristo wa uongo ni tofauti kabisa na kile cha Kristo katika mwili. Ni rahisi sana kutambuliwa na watu ambao huelewa ukweli. Kwa hivyo, kutofautisha Kristo wa kweli na Makristo wa uongo kwa kuzingatia kanuni ya Kristo kuwa ukweli, njia, na uzima ndiyo njia sahihi zaidi. Bwana Yesu aliwahi kusema mara moja kuwa kondoo wa Mungu husikiliza sauti ya Mungu. Wanawali werevu wanaweza kusikia sauti ya Mungu, na wanawali werevu wataweza kugundua ukweli katika sauti ya Bwana harusi, wagundue tabia ya Mungu katika neno la Mungu, wagundue alicho nacho Mungu na alicho, na waweze kuona nia za Mungu, na hivyo wataweza kukubali kazi ya Mungu na warudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ni kwa nini wanawali wajinga hawawezi kusikia sauti ya Bwana harusi? Wanawali wajinga ni wajinga kwa sababu hawawezi kutambua ukweli ni nini. Hawawezi kutofautisha sauti ya Mungu na wanajua tu kufuata kanuni. Kwa hivyo watafichuliwa na kuondolewa na kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Wale ambao tunaupata uzoefu wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho wote huuona ukweli mmoja waziwazi: Wakati Mungu ameitenda hatua mpya ya kazi, Shetani na kila aina ya pepo waovu hufuatia muda mfupi baadaye ili kuiga na kujisingizia kazi ya Mungu ili kuwadanganya watu. Bwana Yesu aliponya na aliwafukuza pepo, naye Shetani na pepo waovu waliponya na kuwafukuza pepo kwa kuiga. Roho Mtakatifu aliwapa watu lugha, kisha pepo waovu wakawachezea watu hadi wakazungumza kile kiitwacho “lugha” ambazo mtu yeyote hangeweza kuzifahamu. Hata hivyo, ingawa pepo waovu watafanya kila njia ili kuwapatia wanadamu mahitaji mbalimbali wayatakayo na ingawa watatekeleza baadhi ya matendo yapitayo akili za kibinadamu ili kuwadanganya watu, Shetani na pepo waovu hawana ukweli hata kidogo. Hivyo, hawataweza hata kidogo kuwapa watu ukweli. Kutokana na hoja hii, mnaweza kumtofautisha Kristo wa kweli na wale wa uongo.

Wakati ambapo Mungu mwenye mwili alianza kazi wakati huu, kwanza Alibaki mnyenyekevu na kujificha kwa muda mrefu, Akingoja hadi neno lilipofika kiwango cha juu ambapo watu walishindwa. Hapo tu ndipo Roho Mtakatifu alimshuhudia Kristo. Kristo hajawahi kumwambia yeyote kwamba Yeye ni Kristo akiwa katika uwepo wake, Hajawahi kutumia nafasi Yake kama Kristo kuwakemea watu. Amebaki mnyenyekevu na kujificha, akijishughulisha na kuwapa watu na yale ambayo maisha yao yanadai, katika kuonyesha ukweli, katika kutatua shida zinazohusiana na kubadili tabia ya mwanadamu. Kristo hajawahi kuringa, daima Amebaki mnyenyekevu na kujificha. Hiki ni kitu ambacho kwacho hakuna kiumbe anaweza kulingana nacho. Kristo hajawahi kutumia nafasi Yake kuwafanya watu wamtii na kumfuata. Badala yake, Anaonyesha ukweli ili kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu na kumwokoa mwanadamu ili mwanadamu apate maarifa ya Mungu, kumtii Mungu na kupatwa na Mungu. Kutoka kwa hili, unaweza kuona kwamba Mungu kweli ni wa heshima. Huku Roho wa Mungu akipata mwili, Yeye huitenda kazi Yake kwa njia ya kunyenyekea na kufichika. Yeye huyapitia Mwenyewe maumivu na mateso yote ambayo mwanadamu huyapitia, bila lalamiko lolote. Kama Kristo, Yeye hajawahi kuringa au kujisifu Mwenyewe, na bila shaka Yeye hajawahi kujishushia hadhi wala kuishikilia kauli. Yeye hutoa kabisa heshima na utakatifu wa Mungu. Hili huifichua asili ya maisha ya Mungu yenye heshima isiyolinganishika, na kwamba Yeye ni mfano halisi wa upendo. Kazi itekelezwayo na Makristo wa uongo na pepo waovu ni kinyume hasa cha kazi itekelezwayo na Kristo. Pepo waovu daima ni wepesi kudai kwamba wao wenyewe ni Kristo. Wanadai kwamba usipowasikiliza, basi hutaweza kuuingia ufalme. Wao hulitenda kila wawezalo ili watu wawaone, hujisifu, huringa, hujitukuza, au kuitenda baadhi ya miujiza ili kuwadanganya watu. Baada ya watu kudanganywa hadi kukubali, watazirai, kwa sababu hawajapewa ukweli kwa muda mrefu sana. Kuna mifano mingi sana ya haya, kwa sababu Makristo wa uongo sio ukweli, njia, au uzima. Hivyo, hawana njia. Wale wanaowafuata wataaibishwa karibuni, na wakijaribu kubadilika wakati huo, watakuwa wamechelewa sana. Hivyo, jambo muhimu sana ni kuamua kwamba Kristo peke yake ndiye ukweli, njia na uzima. Makristo wa uongo hawana ukweli wowote kabisa. Pepo waovu mbalimbali hawana ukweli wowote kabisa. Bila kujali wayasemayo ni mengi kiasi gani, bila kujali ni vitabu vingapi wataviandika, hakutakuwa na ukweli hata mmoja katika chochote kati ya hayo. Hili ni halisi. Kristo peke yake ndiye Awezaye kuuonyesha ukweli. Kuyatofautisha mambo katika msingi wa hoja hii ndilo jambo muhimu zaidi. Licha ya hayo, Kristo hajawahi kuwalazimisha watu wamkubali au kumkiri Yeye. Wale wanaomwamini Yeye watakuja kuuona ukweli wazi zaidi na zaidi, na njia itaangazwa zaidi na zaidi. Hili huthibitisha kwamba Kristo peke yake ndiye Awezaye kumwokoa mwanadamu, kwa sababu Kristo ndiye ukweli. Makristo wa uongo wanaweza tu kuyasema mambo machache ambayo humwiga Yeye, maneno ambayo yanaupotosha ukweli. Hakuna ukweli kabisa ndani ya maneno haya. Yatamwelekeza tu mwanadamu kwenye giza, kumletea maafa, na kazi ya pepo waovu. Bila shaka hutaokolewa ukifuata Makristo wa uongo, utapotoshwa tu zaidi na zaidi na Shetani. Utakuwa mwenye ganzi na mjinga zaidi na zaidi kiasi cha kufikia maangamizi yako. Wale wanaowafuata Makristo wa uongo ni kama mwanadamu kipofu anayeingia katika mashua ya wezi—wanachagua kuangamia kwao kabisa!

Kimetoholewa kutoka katika Utangulizi wa Kuchangua Matukio ya Ulaghai wa Makristo wa Uongo na Wapinga Kristo

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp