Ulishuhudia kuwa Bwana amerejea na hufanya kazi Yake ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Hili linaonekana kuwa tofauti na hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe katika Kitabu cha Ufunuo. Kile watu wengi katika dini wanachofikiria ni kwamba hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe imelenga wasioamini walio wa pepo Shetani. Bwana atakapokuja, waumini watachukuliwa kwenda mbinguni, na kisha Atatuma maafa kuwaangamiza wasioamini. Hiyo ndiyo hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe. Unashuhudia mwanzo wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, lakini hatujaona Mungu akileta maafa kuwaangamiza wasioamini. Basi inawezaje kuwa hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe?

07/06/2019

Jibu:

Wale wote ambao wanaelewa Biblia wanajua kuwa hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo ni maono ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Mwenyezi Mungu mwenye mwili Alikuja kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake katika siku za mwisho, Akianza kuwatakasa na kuwaokoa binadamu potovu. Hii inamaanisha hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi imeanza tayari. Hukumu lazima ianzie kutoka nyumba ya Mungu. Mungu kwanza Ataunda kikundi cha washindi kabla ya maafa. Kisha, Mungu ataleta chini maafa makubwa na kuanza kuyazawadia mazuri na kuadhibu maovu, hadi hii enzi ya uovu iangamizwe. Hukumu ya Mungu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi katika siku za mwisho basi itakamilika kabisa. Kisha Mungu Ataonekana kwa uwazi kuanzisha enzi mpya. Sisi sote tunaweza kuliona vizuri sana sasa. Dalili ya maafa makubwa—miezi minne ya damu iliyofuatana—imeonekana tayari. Maafa makubwa yanakaribia. Wakati maafa makubwa yatakuja, yeyote anayempinga Mungu, kumhukumu Mungu, au kumkataa Mungu, na watoto wa ibilisi Shetani wataangamizwa kwenye maafa. Je, si hiyo kwa usahihi hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi? Tunaweza kuona kutoka kwa unabii wa Biblia kuwa kurudi kwa Bwana kumegawanishwa katika hatua mbili za kufika kwa siri na kufika kwa uwazi. Ya kwanza, Bwana Anakuja kama mwizi, kumaanisha Mungu mwenye mwili Anafika kwa siri kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Kusudi kuu ni kukamilisha kikundi cha washindi. Hii inatimiza unabii wa “lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho tayari ilianza wakati Mungu mwenye mwili Alifika kwa siri kuonyesha ukweli na kuhukumu binadamu wote. Sehemu ya kwanza ya kazi ni kuanzisha hukumu katika nyumba ya Mungu. Na hiyo, Mungu huwatakasa na kuwaokoa wale ambao wanasikia sauti Yake na wanaletwa mbele Yake Akiwafanya washindi. Kisha kazi kuu ya Mungu inatimizwa, na maafa makubwa yanaanza. Mungu atatumia maafa kuadhibu na kuangamiza hii dunia nzee. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho hivyo inafika kilele chake. Wakati Mungu huonekana kwa uwazi katika mawingu, kazi Yake ya hukumu itakuwa imekamilika kabisa. Ufalme wa Mungu kisha utaonekana. Hii hivyo inatimiza unabii wa Yerusalemu mpya ikishuka kutoka mbinguni. Kama vile Mwenyezi Mungu alisema, “Hali moja ya kazi ya Mungu ni kuwashinda wanadamu wote na kuwapata watu waliochaguliwa kupitia kwa maneno Yake. Hali nyingine ni kuwashinda wana wote wa uasi kupitia kwa maafa mbalimbali. Hii ni sehemu moja ya kazi kubwa ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio ufalme ulio hapa duniani ambao Mungu anataka unaweza kutimizwa kwa ukamilifu, na hii ni sehemu ya kazi ya Mungu ambayo ni kama dhahabu nzuri(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 17). Maneno ya Mwenyezi Mungu yanajumuisha kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho kwa usahihi kabisa. Tunaweza kuielewa kwa urahisi sana. Hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Kulingana na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, tunaweza pia kuelewa kile ambacho unabii wa Ufunuo kuhusu kufunguliwa kwa vitabu kuhukumu wafu na kufunguliwa kwa kitabu cha uzima kunahusu. Kwa kweli, kufunguliwa kwa vitabu kuhukumu wafu ni hukumu ya Mungu ya wale wote waliomkataa na kumpinga Yeye. Hii hukumu ni laana yao, adhabu yao, maangamizo yao. Na kufunguliwa kwa kitabu cha uzima kunarejelea hukumu inayoanzia katika nyumba ya Mungu, hiyo ni, Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, Akionyesha ukweli kuhukumu na kutakasa wote wale walioletwa mbele ya kiti Chake cha enzi. Hawa wateule wa Mungu wanaokubali hukumu ya Mwenyezi Mungu na wakaletwa mbele Yake wote ni walengwa wa hukumu ya Mungu, utakaso, na wokovu. Hukumu inayoanzia katika nyumba ya Mungu ni ya kukamilisha kikundi hiki cha watu kabla ya maafa. Kikundi hiki cha watu pekee ndio mabikira wenye busara, watu ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima, washindi 144,000 waliotabiriwa na Kitabu cha Ufunuo, watu ambao hatimaye wataingia ufalme wa mbinguni kurithi uzima wa milele. Hii inatimiza kilichotabiriwa katika Ufunuo: “Na nikaangalia, na ona, Mwanakondoo alikuwa amesimama juu ya mlima Sayuni, na pamoja na yeye watu elfu mia moja arobaini na nne, waliokuwa na jina la Baba yake limeandikwa katika mapaji ya nyuso zao. Na nikasikia sauti iliyotoka mbinguni, mithili ya sauti ya maji mengi, na mithili ya sauti ya radi kubwa: na nikasikia sauti yao wapiga vinubi wakipiga hivyo vinubi vyao: Na waliimba kwani ilikuwa wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi, na mbele yao wao wanyama wanne, na wao wazee: na hakuna mwanadamu angeweza kujifunza wimbo huo ila wao elfu mia arobaini na nne, ambao walikuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi(Ufunuo 14:1-5).

Kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kwa ukamilifu inatimiza maono ya hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Kiti kikubwa cheupe cha enzi kinaashiria utakatifu wa Mungu vile vile mamlaka Yake. Basi tunawezaje kujua mamlaka ya Mungu? Sisi sote tunalijua. Mungu aliumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno Lake. Anatumia neno Lake kuongoza, kutakasa, na kuokoa binadamu, kutimiza kila kitu. Neno la Mungu linawakilisha mamlaka Yake. Kama vile tu Neno la Mungu linasema: “Kama Mimi nikisema, litakuwa. Kama Mimi nikiamuru, litasimama imara(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 21). “Kile Nilichosema lazima kihesabiwe, kile kilichohesabiwa lazima kikamilishwe, na hili haliwezi kubadilishwa na yeyote; hili ni thabiti(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1). Kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni kazi ya neno. Mungu hutumia neno Lake kuuongoza ulimwengu mzima, kuongoza binadamu wote. Yeye hutumia neno Lake kuongoza, kuwapa binadamu, na sasa Anatumia neno Lake kuhukumu na kutakasa binadamu. Mwenyezi Mungu anasema, “Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni). “Katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu). “Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli. Kila mtu duniani atasherehekea maneno ya Mungu, ama ni watu wazima au watoto, wanaume, wanawake, wazee, au vijana, watu wote watajinyenyekeza katika maneno ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili).

Onyesho la neno la Mwenyezi Mungu ni kama radi inayopiga kutoka Mashariki moja kwa moja mpaka Magharibi. Linawatakasa na kuwakamilisha wote ambao wanarudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kuwafichua Mafarisayo wanafiki ambao wanachukia ukweli. na vile vile watu wote waovu ambao wanakataa na kumpinga Mungu. Wakati huo, linawabwaga wana wote wa uasi. Kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu duniani katika siku za mwisho inaonyesha kuwa Mungu tayari Ameketi na Anatawala kwenye kiti Chake cha enzi. Hata ingawa hii dunia nzee ya uovu na giza bado ipo kwa sasa, maafa makubwa tofauti ambayo yataangamiza dunia yatafika hivi karibuni. Hakuna nguvu ulimwenguni ambayo inaweza kuangamiza ufalme wa Mungu, na hakuna nguvu ambayo inaweza kukomesha kazi ya Mungu au kuzuia kazi Yake kuendelea. Mungu kutumia mamlaka Yake kufanya kazi Yake ya hukumu duniani ni sawa na kiti Chake cha enzi mbinguni: Ni kitu ambacho hakuna yeyote anaweza kutikisa na hakuna yeyote anaweza kubadilisha. Hiyo ni kweli. Kama tu vile Mwenyezi Mungu anavyosema, “Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19). Haya ndiyo mamlaka na nguvu zinayoonyeshwa na neno la Mungu. Neno la Mungu kutumia mamlaka ulimwenguni ni Kristo akiongoza ulimwenguni. Huyu ni Mungu tayari Akiongoza kwenye kiti Chake cha enzi ulimwenguni. Hii inatosha kuonyesha kuwa ufalme wa Mungu tayari umeshukia ulimwenguni. Huu ni ukweli ambao hakuna yeyote anaweza kana. Tunaweza kuona kuwa mapenzi ya Mungu tayari yamefanywa kwa ukamilifu ulimwenguni, kama yalivyofanywa huko mbinguni. Bwana Yesu alisema, “Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni(Mathayo 6:10). Ufunuo pia kilitabiri: “Naye malaika wa saba akalipiga baragumu; na kukawa na sauti kubwa mbinguni, zikisema, falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele. Na wao wazee ishirini na wanne, ambao waliketi katika viti vyao mbele ya Mungu, walianguka chini kifudifudi, na kumwabudu Mungu, wakisema, Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala(Ufunuo 11:15-17). Haya maneno tayari yamekuwa kweli. Huu wote ni ukweli uliotimizwa na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Haki Yangu, uadhama na hukumu havionyeshi huruma kwa Shetani. Lakini kwa ajili yenu, vipo ili kuwaokoa, lakini ninyi hamwezi tu kuielewa tabia Yangu, wala hamjui kanuni za matendo Yangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 90). Mistari hii ya maneno ya Mungu inarejea matokeo ambayo haki, uadhama na hukumu ya Mungu hufanikishwa ndani ya watu. Matokeo ni gani? Watu wengine hushindwa kuona. “Haki Yangu, uadhama na hukumu havionyeshi huruma kwa Shetani.” Ni nini maana ya maneno haya? Watu wengine husema, “Maana ya maneno haya ni kwamba haki, uadhama, na hukumu ya Mungu huelekezwa kwa Shetani, sio kwa watu.” Je, ufafanuzi huu ni sahihi au si sahihi? Ufafanuzi huu si sahihi, hata ni wa kuchekesha. Hapa, pia unasema, “Lakini kwa ajili yenu, vipo ili kuwaokoa.” Hili linamaanisha nini? “Kwenu” inarejea watu wa Mungu walioteuliwa, wote wanaokubali kazi ya Mungu. Kwa watu wa Mungu walioteuliwa na wote ambao wanamwamini Mungu kweli, haki, uadhama, na hukumu ya Mungu ni kwa ajili ya wokovu wao. Watu wengine huhisi kuwa hili linakinzana, wakisema, “Hayaonyeshi huruma kwa Shetani, lakini ni ya kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo je, haki, uadhama, na hukumu ya Mungu vinaelekezwa kwa Shetani au mwanadamu?” Je, utata huu ni rahisi kutatua? Watu wengine wanaweza kufikiri hivi: “Kati ya watu wote, wengine ni wa Shetani, ibilisi, na wengine ni watu wa Mungu walioteuliwa, walengwa wa wokovu. Kwa hiyo, kwa Shetani, haki, uadhama, na hukumu ya Mungu ni mfichuo, uondoaji, au adhabu. Kwa watu wa Mungu walioteuliwa, kwa wale ambao wanamwamini Mungu kwa kweli, ni vya wokovu, kutakasa, na kukamilisha kabisa.” Je, ufafanuzi huu ni sahihi au la? Ufafanuzi huu ni sahihi. Watu kama hawa wameipata njia. Kwa hiyo sasa, je, ni Shetani au watu wa Mungu walioteuliwa watakaopitia hukumu ya Mungu ya haki, uadhama na ya ghadhabu? Wote lazima waikubali. Si sawa kwa yeyote kutoikubali. Kwa maneno mengine, hakuna mtu anayeweza kuikimbia; huu ni ukweli. Wengine wanaweza kusema, “Mungu hutamka maneno Yake, lakini wasioamini, watu wa dini, na wale ambao ni wa Shetani hawajayasikia wala kuyasoma!” Wasipoyasikia au kuyasoma, je, watakimbia hukumu na kuadibu kwa Mungu? Wanaweza kukimbia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, lakini je, wanaweza kukimbia ghadhabu ya Mungu na maafa yaliyotumwa na Mungu? Wanaweza kuepuka hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi? Hakuna mtu anayeweza kukimbia hilo. Usipokubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, basi lazima ukubali hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi. Kwa hiyo hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi ni nini? Maafa! Kwa hivyo, hukumu ya Mungu ya kiti kikuu cheupe cha enzi katika siku za mwisho tayari imeanza.

Hukumu ya maneno ya Mungu huelekezwa kwa watu wa Mungu walioteuliwa. Hukumu ya ukweli halisi, hukumu na adhabu ya maafa, huelekezwa kwa wasioamini. Kwa hivyo, kuna vipengele viwili vya kazi ya hukumu, ambavyo hutekelezwa kwa wakati mmoja. Hoja hii haiwezi kupuuzwa. Watu wengine husema, “Wateule katika nyumba ya Mungu wanapitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, lakini wasioamini wanakula, kunywa, na kusherehekea, na hawajakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu!” Hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi ni tofauti na hukumu na kuadibu kwa maneno. Hukumu na kuadibu kwa maneno hufanyika kwa kipindi kirefu cha muda, lakini hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi kutakuja baada ya muda mfupi, mara moja. Ni kama tetemeko kubwa la ardhi. Watu wanapokuwa wakila, kunywa, na kujifurahisha, ghafla, ardhi inatetemeka, na tetemeko kubwa la ardhi linatokea. Kila mtu anataka kukimbia lakini hawezi, na anaishia kupondwa hadi kufa. Hukumu na kuadibu kwa ukweli halisi ni kwa haraka, kwa muda mfupi tu, kwa ghafla, na hakuwezi kuzuiwa. Hukumu na kuadibu kwa maneno ni tofauti. Huchukua muda fulani. Aidha, watu wengine hawajala wala kunywa maneno ya Mungu, na watu wengine wameyala na kuyanywa lakini hawajayachukuliwa kwa uzito. Watu wengine wameyachukulia kwa uzito lakini hawajapitia hukumu yao. Kutoipitia hakukubaliki. Mara ya kwanza wanapoyapitia, huenda wasiweze kuyatii, na hawana maarifa au ufahamu, lakini baada ya kipindi fulani cha muda, ufahamu unakuja na baada ya muda mrefu kidogo, wanaelewa zaidi kidogo. Baada ya kupitia kwa muda mrefu zaidi kidogo, wanaweza kuelewa kikamilifu zaidi, na kisha toba halisi na mabadiliko halisi yanaweza kutokea. Huu ndio mchakato wa ufuatiliaji wa ukweli. Kutoka kwa kutoelewa hadi kuelewa, utiifu kutokana na kuelewa na maarifa kutokana na utiifu—mchakato huu huchukua muda mrefu. Ili kufikia matokeo, watu wengine lazima wapitie hilo kwa miaka kumi au ishirini, na watu wengine miaka ishirini hadi thelathini. Na wakati ule ule tunapopitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, wasioamini hufanya nini? Kula, kunywa, kujifurahisha, kulala na kuota! Tutakapokuwa tumepitia hukumu na kuadibu kunakotosha na kutakaswa, na tunaanza kufurahi na kumsifu Mungu, watu wa Mungu wanapokamilishwa na Mungu, maafa ya wasioamini yatakuja. Na maafa yatakapokuja, utakuwa wakati wa kifo chao! Watu wengi sasa wamegundua, “Hii ndiyo hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi! Hukumu na kuadibu kwa maneno ni kwa ndani na kuja kwa maafa na adhabu ya maafa ni ya nje. Wale ambao hawamwamini Mungu na wale wanaompinga Mungu lazima wote wafe katika maafa.” Je, uhusiano wa wakati kati ya hukumu na kuadibu kwa ndani kwa maneno na adhabu ya nje ya maafa ni upi? Yote yanapatana. Maafa ya kila aina pia huwatendekea wasioamini, lakini si makubwa sana, wala hayaainishwi kama maafa ya kuharibu sana. Lakini mara watu wa Mungu watakapofanywa kuwa kamili, kundi la washindi litakapotokea, “puup,” maafa makubwa yatashuka mara moja. Hii ndiyo hukumu na kuadibu kwa maafa ambako hutumiwa kuwaangamiza wasioamini. Hukumu hii na kuadibu huku kumejaa hasira na uadhama!

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp