Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanaamini kuwa Bwana Yesu kusema “Imekwisha(Yohana 19:30) msalabani ni ushahidi kwamba kazi ya Mungu ya wokovu tayari imekamilika kabisa. Na bado unashuhudia kwamba Bwana amerejea katika mwili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu ili kuwaokoa wanadamu kabisa. Kwa hiyo ni kwa njia gani hasa mtu anafaa kuelewa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu? Hatuko dhahiri juu ya kipengele hiki cha ukweli, kwa hiyo tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.

07/06/2019

Jibu:

Wakati Bwana Yesu alisema msalabani “Imekwisha(Yohana 19:30), Alikuwa anazungumzia hasa kuhusu nini? Je, Alimaanisha kwamba kazi ya ukombozi ilikuwa imekwisha, au alikuwa Akimaanisha kwamba kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kikamilifu ilikuwa imekwisha? Je, watu wa wakati ule hakika wangejua? Inaweza kusemwa kwamba hakuna aliyejua. Kile Bwana Yesu alichosema yalikuwa ni maneno: “Imekwisha.” Hakusema kwamba kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ilikuwa imekwisha. Wanadamu hawawezi kwa hakika kuelewa kile Bwana Yesu alichokuwa akimaanisha Aliposema, “Imekwisha.” Je, mtu yeyote anawezaje kuthubutu kuelezea maneno ya Bwana kulingana na mawazo yake mwenyewe? Kwa nini kuthubutu kutafsiri kiholela maneno haya “Imekwisha”? Hiki sio kingine ila kuwekelea bila kufikiria mawazo ya kibinafsi juu ya maneno ya Bwana Yesu. Hebu tafakari haya, ikiwa Bwana Yesu alisema “Imekwisha” inamanisha kwamba kazi ya Mungu ya kuokoa wanadamu wote imekamilika kabisa, basi kwa nini Bwana alitoa unabii, na kusema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Tunaelewaje hili? Pia, kama ilivyorekodiwa katika Injili ya Yohana, Sura ya 12, Mstari wa 47-48, “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho.” Maneno ya Bwana Yesu yanatwambia wazi kwamba Bwana atarudi kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Pia kuna unabii wa Biblia: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Kulingana na kile ambacho mchungaji na mzee husema, ikiwa kusulubiwa kwa Bwana Yesu kulikamilisha kazi yote ya kumwokoa mwanadamu, basi ni vipi unabii wa Bwana Yesu, “Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote,” je, maneno haya yangekuwaje ukweli? Je, si unabii wa Bwana Yesu kwamba Angerejea kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ungekosa kutimia? Kwa hivyo, yale mchungaji na mzee husema kweli hayalingani na maneno ya Bwana Yesu na hayalingani na uhalisi wa kazi ya Mungu. Sote tunapaswa kujua kwamba kile Bwana Yesu alichofanya ilikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kile tu tunapaswa kufanya ni kukubali Bwana Yesu, kukiri na kutubu mbele Yake, na dhambi zetu zitasamehewa. Kisha sisi tunastahili kuomba kwa Bwana, na kufurahia neema ambayo Bwana ametawaza. Bila kujali dhambi, hatutahukumiwa na sheria tena. Haya ndiyo matokeo ya kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kauli ile “wokovu kupitia Imani” ambayo sisi husema kila mara. Kutokana na matokeo yaliyopatikana na kazi ya Bwana Yesu tunaona hata thibitisho kubwa zaidi kwamba kazi ya Bwana Yesu ilikuwa ile ya ukombozi pekee. Hakuna vile ilikuwa ya kuhukumu, kutakasa, na kuwakamilisha watu wa siku za mwisho. Ingawa imani yetu katika Bwana Yesu inasamehe dhambi zetu, na hatutendi dhambi zilizo wazi, na huwa na tabia nzuri kweli, lakini hatujajitenga kabisa kutoka kwa dhambi na kuwa safi, na kuokolewa kikamilifu, ni kweli? Je, mara kwa mara sisi husema uongo na kutenda dhambi? Je, bado sisi hutenda kwa tamaa na tuna mawazo maovu? Je, sisi bado huwaonea wivu wengine, na kuwachukia wengine? Je, mioyo yetu imejawa na majivuno na hila? Je, bado tunaiga mitindo ya kidunia, na kushikilia utajiri, na kutamani utukufu? Watu wengine wanapokamatwa na kuhukumiwa na serekali ya Kikomunisti ya China, hata humlaumu Mungu. Wao hata hutoa taarifa zilizoandikwa ambazo humkana Mungu, na kumsaliti Mungu. Hasa kuhusu kuonyesha ukweli na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, watu hutoa hukumu juu ya kazi ya Mungu na kuilaani kulingana na mawazo yao na matamanio. Je, si huu ni ukweli? Katika imani yetu katika Bwana, hivyo, tunapata tu msamaha wa dhambi. Lakini ndani yetu inabaki asili ya Shetani na tabia ya Shetani. Hiki ndicho chanzo chetu cha kutenda dhambi na kupinga Mungu. Ikiwa asili ya ndani yetu ya dhambi haitatatuliwa, basi tutampinga Mungu, tutamsaliti Mungu, na kumfikiria Mungu kama adui. Je, unaweza kusema kwamba mtu kama huyu anastahili kuingia katika ufalme wa mbinguni? Ni lazima liwe wazi sasa kwamba kwa kusema “Imekwisha,” Bwana Yesu alimaanisha kwamba ni kazi ya Mungu ya ukombozi pekee ilikuwa imekamilika. Kwa hakika, Yeye hakuwa akisema kwamba kazi yote ya kuokoa mwanadamu ilikuwa imekamilika. Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho alikuja kuonyesha ukweli wote, na kufanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Kuja huku ni kwa kuwatakasa watu kikamilifu, na kuwaokoa kabisa, kutatua tatizo la kimsingi la dhambi ndani ya watu, kuwaruhusu watu kuwa huru kutoka kwa dhambi na kupata utakaso, kupata wokovu kamili na kuingia katika ufalme wa Mungu. Acha tusome vifungu vingine vichache vya maneno ya Mwenyezi Mungu, ili sote tuweze kuelewa kwa uwazi kabisa.

Mwenyezi Mungu anasema, “Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho).

Ni lazima ujue aina ya watu ambao Ninataka; wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea).

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. … Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Mwenyezi Mungu hunena wazi kuhusu umuhimu na matokeo yanayopatikana kwa kazi ya hukumu wakati wa siku za mwisho. Hili linaturuhusu kuwa na uhakika kwamba kazi ya hukumu ya Mungu wakati wa siku za mwisho ndiyo kazi ambayo hutakasa kikamilifu na kumwokoa wanadamu. Kazi ya ukombozi ambayo Bwana Yesu aliifanya inafungua njia kwa kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Mwenyezi Mungu hufanya kazi ya hukumu na utakaso juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, kikamilifu Akiwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi na kuwaleta katika ufalme wa Mungu. Je, si Mungu kufanya kazi kwa njia hii ni kwa utendaji sana? Tukikubali tu kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, na kutoikubali kazi ya Mungu ya hukumu na kazi ya kutakasa ya siku za mwisho, tutaweza kustahili kuuingia ufalme wa Mungu? Yaonekana kwamba imani kwa Mungu inatuhitaji kuifahamu kazi ya Mungu. Ilhali watu wengi wa kidini wanayo imani ya wokovu kupitia kwa imani pekee. Wanasadiki kwamba imani kwa Bwana huleta msamaha wa dhambi, huku ukisuluhisha matatizo yote, kumsadiki Bwana wenye rehema na upendo husamehe dhambi yoyote ambayo mtu angeweza kutenda. Atawainua wote hadi katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja. Wao hivyo basi hukataa kuikubali kazi ya hukumu ya siku za mwisho ya Mwenyezi Mungu. Tatizo hili ni lipi? Mtu aina hii anaifahamu kazi ya Mungu? Je, wao wanaifahamu tabia ya Mungu yenye haki? Ungesema kwamba Mungu angeweza kuruhusu mtu mwenye aina ya shetani anayeasi dhidi Yake na kumpinga Yeye kuingia ndani ya ufalme Wake? Asingemruhusu! Mtu aina hii kuingia ndani ya ufalme wa Mungu kutasababisha matokeo gani? Hebu tuuchukulie mfano. Kama wana wa Israeli waliomsadiki Yehova Mungu wangeletwa ndani ya ufalme wa Mungu, unafikiria nini kingefanyika? Hawakuweza hata kukubali hata Mungu mwenye mwili, Bwana Yesu, na pia walifanya kila waliloweza kumshutumu Bwana Yesu, na kumsulubisha Bwana Yesu msalabani. Aina hii ya kishetani inayompinga kabisa Mungu kwa njia hii, kama wangeingia ndani ya ufalme wa Mungu, wangeendelea kumpinga Mungu? Je, wangeasi? Je, wangejaribu kunyanganya nguvu za Mungu? Je, kwa nini Bwana Yesu hakuenda katika sinagogi kuhubiri? Ni kwa sababu makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wa imani ya Kiyahudi walikuwa waovu sana. Walikuwa na uwezo wa lolote. Sote tunajua kwamba baada ya Bwana Yesu kukamatwa na wao, Alipigwa, kusutwa, na kutemewa mate. Hata Alipeanwa kwa serikali ya Kirumi kusulubiwa. Bwana Yesu tayari alijua kuwa walikuwa wa namna ile ya nyoka hivyo Yeye hakuenda katika sinagogi kuhubiri. Katika siku za mwisho Bwana Yesu amerudi. Kwa nini Haendi katika makanisa kuhubiri? Ni kwa sababu viongozi katika makanisa wote ni wakatili sana. Kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili angeenda katika makanisa, hakika wangeiita polisi. Wao hakika wangempeleka Mwenyezi Mungu kwa serekali ya CCP. Je, si huo ndio ukweli? Je, sasa tutathubutu kwenda katika makanisa kushuhudia hadharani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Ukiwashuhudia kuhusu Mwenyezi Mungu, wao hakika watakuhusuru na kukudunisha, na hata wakupeleke kwa Ofisi ya Usalama wa Umma. Kwa sababu hizi, kanisa la leo ni sawa na jinsi sinagogi za dini ya Kiyahudi zilikuwa. Kwote ni mahali ambapo humfukuza Mungu, humkataa Mungu, na kuhukumu Mungu. Je, iko hivi kweli? Hii inaenda kuonyesha kiwango ambacho mwanadamu ni mpotovu. Wamechoshwa na ukweli, na huchukia ukweli. Wote hukataa kufika kwa Mungu, na wote wamekuwa wa aina ya Shetani na kumpinga Mungu. Kama Mungu hangekuwa mwili wakati wa siku za mwisho kuonyesha ukweli, kuhukumu watu, na kuwatakasa watu, jamii ya wanadamu wangeangamizwa na Mungu kwa sababu walimpinga Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Sasa kuna watu wengine ambao wanaonyesha kwamba jambo la mwisho Bwana Yesu alilolisema msalabani lilikuwa, “Imekwisha(Yohana 19:30). Na kisha wanasema: “Bwana Yesu alipotumika kama dhabihu ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu, Yeye aliifanikisha kazi ya Mungu ya wokovu. Tumesamehewa dhambi zetu kwa sababu tunamwamini Bwana Yesu. Pia tumedhibitishwa kuwa wenye haki kupitia imani pekee na kwa hivyo tutaweza kuingia ufalme wa mbinguni. Tunapaswa tu kungojea kunyakuliwa na Bwana.” Au wanasema: “Kila kitu ki tayari, tunahitaji tu kunyakuliwa.” Je, kauli hii imethibitishwa? Hapana, haijadhibitishwa. Tunaweza tu kuthibitisha kwamba dhambi zetu zimesamehewa, siyo? Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba dhambi zetu zimesamehewa? Bila kujali ni dhambi ya aina gani ambayo umetenda, unahitaji tu kuomba na kuikubali dhambi yako na utahisi furaha, amani, na nafsi yako itawekwa huru kutoka kwa utumwa wa dhambi. Mtu anahisi kuwa huru kabisa anapokuwa huru kutokana na dhambi! Huu ni ukweli. Hivyo tunaweza kusema kwamba dhabihu ya dhambi ni kweli kabisa na ni kitu ambacho wote wamwaminio Bwana Yesu wanaweza kukithibitisha kupitia kwa uzoefu wao. Lakini Bwana Yesu hakusema, “Kwa kumwamini Bwana Yesu, utapata wokovu na kuwekwa huru kabisa kutokana na dhambi. Ukimwamini Bwana Yesu, utasifiwa na Mungu na utaingia katika ufalme wa mbinguni.” Bwana Yesu hakulisema hili na hakuna ushahidi kwa hilo. Kwa nini hakuna ushahidi? Dhambi za mwanadamu zimesamehewa, lakini, je, tabia yake ya ndani ya kishetani na asili yake yenye dhambi zinaweza kusamehewa? Hapana. Je, Bwana Yesu aliwahi kusema “Baada ya dhambi zako kusamehewa unaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni”? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema “Unahitaji tu kuniamini Mimi na kutakuwa na nafasi yako katika ufalme wa mbinguni”? Bwana hajasema hivyo kamwe. Je, Bwana Yesu alisema nini? “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Hivyo “afanyaye mapenzi ya Baba Yangu aliye mbinguni” yanamaanisha nini? Yanamaanisha unapaswa kufanya mapenzi ya Mungu, kufuata njia ya Mungu, kuweka katika vitendo njia ya ukweli, yaani, neno la Mungu. Mtu lazima daima alifanye lolote ambalo Mungu anamhitaji alifanye, na lazima ashikilie kila kitu ambacho Mungu anadai afanye, kila kitu ambacho Mungu anadai atii, na kila kitu ambacho Mungu anadai afuate kwa uaminifu, na hapo tu ndipo anapoweza kuingia ufalme wa mbinguni. Lakini ni watu wangapi waliweza kutimiza mahitaji ya Mungu katika Enzi ya Neema? Hakuna hata mmoja. Hivyo tunaweza kusema kwamba kazi ya Enzi ya Neema ilikuwa hatua ya kazi ya ukombozi. Imetabiriwa katika Biblia kwamba Bwana atakaporudi, Ataitenda hatua ya kazi ya hukumu na kuadibu ili kuwatakasa wale wote ambao wanakuja mbele za Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu ataianzisha hatua ya kazi ya utakaso, kazi ya kuwatenga wote kulingana na aina yao wenyewe, katika siku za mwisho kabla ya Yeye kuikamilisha enzi. Na yote ambayo Bwana Yesu aliyatabiri kuhusu kutenganisha ngano kutoka kwa magugu, kondoo kutoka kwa mbuzi, wanawali wa busara kutoka kwa wanawali wajinga, na watumishi wema kutoka kwa watumishi waovu—yote haya yatatimia. Katika siku za mwisho, Mungu ataianzisha hatua ya kazi ya kuwahukumu watu na kuwatakasa watu, jinsi ilivyotabiriwa katika Biblia. Kwa mfano: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17), “Ninyi mnaohifadhiwa na nguvu zake Mungu kupitia imani hadi kwa wokovu ambao uko tayari kufichuliwa katika muda wa mwisho” (1 Petro 1:5), “Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15), “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi(Ufunuo 3:3), na “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12). Unabii huu wote unairejea kazi itakayotendwa Bwana atakaporudi. Hili linathibitisha kwamba kuanzia Enzi ya Sheria hadi wakati wa kurudi kwa Bwana ili kuitimiza enzi, kuna hatua tatu za kazi. Hili ni kweli, na linaweza kuonekana katika unabii wa Biblia. Kazi ya Enzi ya Neema ilikuwa kazi ya ukombozi—bila shaka haikuwa kazi ya kutakasa ili kuiangamiza asili yenye dhambi ya wanadamu. Hapajawa na amwaminiye Bwana Yesu ambaye asili yake ya dhambi imeondoshwa kabisa, hakuna hata mtu mmoja ambaye hajatenda dhambi tena baada ya kusamehewa, hata mmoja ambaye ameyafanikisha mabadiliko kamili ya tabia yake, hata mmoja ambaye amemjua Mungu kwa kweli. Huu ndio ukweli wa mambo. Wakati wa Enzi ya Neema, wanadamu walimwamini Mungu kwa miaka elfu mbili, lakini matatizo matano ya kimsingi yalibaki hayajasuluhishwa: Kwanza, tatizo la asili ya kishetani ya wanadamu yenye dhambi haikusuluhishwa; pili, tatizo la wanadamu kudhihirisha tabia zao za kishetani mara kwa mara lilibaki halijasuluhishwa; tatu, tatizo la mabadiliko ya tabia ya maisha ya kila mtu halikusuluhishwa; nne, tatizo la jinsi wanadamu wanapaswa kumjua na kumtii Mungu halikusuluhishwa kikamilifu; tano, aidha, tatizo la jinsi wanadamu wanaweza kupata utakaso halikusuluhishwa kabisa. Haya matatizo matano ya kimsingi yalibaki bila kusuluhishwa, kuthibitisha kwamba kazi ya Mungu ya Enzi ya Neema ilikuwa tu hatua moja ya kazi ya ukombozi—na sio hatua ya mwisho ya kazi ya ukombozi wa wanadamu. Kazi ya Enzi ya Neema iliitayarisha njia tu, iliijenga misingi, kwa ajili ya kazi ya ukombozi ya siku za mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Kuokolewa kunamaanisha nini hasa? Watu katika dini huamini kwamba kwa sababu maneno ya mwisho ya Bwana Yesu msalabani yalikuwa “Imekwisha(Yohana 19:30), mradi una imani katika Bwana Yesu na dhambi zako zimesamehewa, hii inamaanisha umeokoka. Watu katika dini huelewa vibaya kile Mungu amesema kwa sababu hawajui kazi ya Mungu. Je, Bwana Yesu alikuwa akiashiria nini Aliposema “Imekwisha”? Alikuwa akiashiria ukamilisho wa kazi ya Mungu ya ukombozi, na hakika sio kuashiria kumaliza mpango wa Mungu wa usimamizi. Kwa hivyo, ni ukweli kwamba ni rahisi zaidi kwa wale ambao hawajui kazi ya Mungu kuelewa visivyo kile ambacho Amesema, na rahisi zaidi kwao kuhukumu kazi ya Mungu. Kwa hivyo wokovu ni nini hata hivyo? Je, kusamehewa dhambi ni wokovu wa kweli? La, kunaweka tu msingi kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho, kunaanzisha msingi. Kazi ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu kwa uhalisi ni kazi ya siku za mwisho. Kazi ya siku za mwisho inaanzishwa kwa msingi wa sadaka ya dhambi katika Enzi ya Neema. Ni kwa sababu tu kuna sadaka ya dhambi ndiyo dhambi za mwanadamu zinasamehewa na wanadamu wana sifa zinazostahili kuja mbele ya Mungu kupokea kazi Yake. Ni kwa hukumu na kuadibu kwa siku za mwisho tu, majaribu na usafishaji, ambapo mwanadamu anaokolewa kwa kweli na kuwekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kutoka kwa udhibiti wa asili ya kishetani. Ni kazi ya siku za mwisho pekee inayoweza kubadili tabia ya mwanadamu ambayo imepotoshwa na Shetani, na kuweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwa ushawishi wa Shetani, na kufikia lengo la kumfanya mwanadamu kumgeukia Mungu kikamilifu. Kwa hivyo, iwapo katika kumwamini Mungu mwanadamu hapitii kazi ya Mungu katika siku za mwisho, basi hawezi kufikia wokovu kwa kweli. …

Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Baada ya dhambi za mwanadamu kusamehewa, chanzo cha kutenda dhambi kwa mwanadamu, yaani, asili yake ya kishetani haijaondolewa. Mwanadamu akiendelea kama kawaida kumpinga Mungu na kumsaliti Mungu, hili si kosa dhidi ya tabia ya Mungu? Iwapo Mungu angemuinua katika ufalme Wake mwanadamu ambaye bado anaweza kumpinga na kumsaliti, hili halingeashiria kwamba Mungu amejidanganya? Mwanadamu huyu mpotovu bado anaweza kumpinga Mungu na bado anaweza kumtundika Kristo msalabani mara nyingine tena. Iwapo mwanadamu kama huyu ni mwanadamu ambaye ameokoka, basi hakuna njia ya kuelezea utakatifu wa Mungu na haki, haina maana. Ufalme wa Mungu ungeruhusu vipi kuwepo kwa mwanadamu ambaye humpinga Mungu? Hilo haliwezekani kwa sababu tabia ya Mungu haivumilii kosa la mwanadamu. Kwa hivyo, ukisema: “Mwanadamu ambaye amepokea sadaka ya dhambi ameokolewa, na anaweza kuingia ufalme wa Mungu,” maneno kama hayo hayafai.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp