Kutambua Jinsi Hatua Tatu za Kazi Zinavyofanywa na Mungu Mmoja
Leo, mada ya ushirika wetu ni “Kutambua Jinsi Hatua Tatu za Kazi Zinavyofanywa na Mungu Mmoja.” Mada hii ni muhimu, na inahusiana moja kwa moja na mwisho na hatima yetu. Pia inahusiana moja kwa moja na iwapo tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tukimwamini Mungu bali tusijue kazi ya Mungu, hilo linaweza kuwa hatari sana. Tunaweza kupoteza wokovu wa Mungu kwa urahisi, jambo ambalo husababisha mateso ya milele. Hivyo, kwa nini tunasema hivi? Tunajua, miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu, na Alisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Bwana Yesu alionyesha ukweli na kufanya miujiza mingi, ambayo inathibitisha kwamba Bwana Yesu alikuwa Masihi. Lakini katika dini la Kiyahudi, jina la Bwana Yesu halikuwa Masihi, wala Hakuzaliwa katika jumba la kifalme, wala Hakuwaongoza kutoka katika utawala wa Kirumi, kwa hivyo Yeye hakika hakuwa Masihi. Kwa hivyo, bila kujali Bwana Yesu alionyesha ukweli kiasi gani au Alitenda miujiza mingapi, hakuna aliyekiri kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu, na kila mtu aliwafuata viongozi wa dini ya Kiyahudi na kumsulubisha. Matokeo yalikuwa nini? Israeli iliangamizwa kwa karibu miaka elfu mbili. Somo hili la kuumiza lilitokeaje? Watu hawakutafuta kujua kazi ya Mungu, walishikilia fikra na mawazo yao, na kupinga na kulaani kazi ya Mungu. Sasa, Bwana Yesu amerudi kama Mwenyezi Mungu. Alionyesha mamilioni ya maneno ya ukweli, na sasa Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kabisa. Lakini kuna habari gani kuhusu ulimwengu wa kidini? Wanapoona kwamba jina la Mwenyezi Mungu si Yesu, wala Yeye haji juu ya mawingu, wanakataa kukiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na wanawafuata wachungaji na wazee katika kumpinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni sawa na kumsulubisha Mungu tena. Watu wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini kila wakati Mungu anapoonekana ili kufanya kazi na kuwaokoa wanadamu, wale wanaomwamini na kungoja kuonekana Kwake daima humhukumu na kumkataa?” Hii ni kwa sababu watu wamepotoshwa sana na Shetani, kwa hivyo wanachukia sana ukweli, na wao kwa kawaida humpinga Mungu. Sababu nyingine ni kwamba watu hawaijui kazi ya Mungu, na wamejawa na fikra na mawazo kuhusu kazi ya Mungu. Wajua, Mungu alipomaliza kazi Yake katika Enzi ya Sheria, wale waliokuwa katika dini ya Kiyahudi waliamini kwamba kazi ya Mungu ilikuwa imekamilika, na Asingefanya kazi nyingine ya zaidi. Walimngoja Masihi ambaye angewaokoa kutokana na utawala wa Kirumi, lakini hawakukubali kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu, na kwa sababu hiyo, walipoteza wokovu wa Bwana. Mungu alipomaliza kazi ya Enzi ya Neema, waumini wa madhehebu yote walifikiri kwamba kwa kuwa Bwana Yesu aliwakomboa wanadamu, kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika, hakuna kazi mpya itakayofanywa, na Bwana atakaporudi, Atatuleta moja kwa moja katika ufalme wa mbinguni. Leo, maafa makubwa yanapokuwa yakija, watu wengi bado wanangoja ujio wa Bwana juu ya mawingu, na wanakataa kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu, na kwa sababu hiyo, wanashindwa kumpokea Mwokozi na kuanguka katika maafa. Wote wanafikiri kwamba Bwana Yesu Alipomaliza kazi Yake, kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu imekamilika, na hakutakuwa na kazi nyingine. Basi hebu tufikirie hili. Je, kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ni rahisi kweli kama watu wanavyofikiri? Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amefichua fumbo la kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Sote tumeona kwamba baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango wa kutuokoa wenye hatua tatu. Kwanza, Alifanya kazi ya Enzi ya Sheria Akitumia jina Yehova, kisha Akaja na kupata mwili kama Bwana Yesu na kufanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, na katika siku za mwisho, Mungu amekuja tena katika mwili kufanya kazi ya hukumu katika Enzi ya Ufalme Akitumia jina Mwenyezi Mungu. Hatua hizi tatu za kazi ni mpango kamili wa usimamizi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu. Ingawa majina ya Yehova, Bwana Yesu, na Mwenyezi Mungu ni tofauti, na kazi wanayofanya katika kila enzi ni tofauti, hatua hizi tatu zina uhusiano wa karibu, kila moja ikiitegemea ile iliyotangulia, na hatimaye kuishia kuwaokoa kabisa wanadamu na kuwaleta katika enzi mpya. Huu ni uthibitisho kwamba ni Mungu mmoja anayefanya kazi tofauti katika kila enzi. Kwa hivyo, tunawezaje kutambua kwamba hatua hizi tatu za kazi zinafanywa na Mungu mmoja? Kuelewa kipengele hiki cha ukweli ni muhimu katika kupata wokovu na kuingia katika ufalme. Ifuatayo, hebu tushiriki juu ya suala hili kulingana na maneno ya Mungu.
Kwanza, nitasoma kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi). Tunaona kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Ya kwanza ni kazi ya Enzi ya Sheria iliyofanywa na Yehova Mungu zaidi ya miaka 3,000 iliyopita, ya pili ni kazi ya Enzi ya Neema iliyofanywa na Bwana Yesu miaka elfu mbili iliyopita, na hatua ya tatu ni sasa—kazi ya hukumu katika Enzi ya Ufalme inayofanywa na Mwenyezi Mungu mwishoni mwa siku za mwisho. Ingawa maudhui ya hatua hizi tatu ni tofauti, kila hatua huendeleza iliyotangulia na huongeza uketo wa kazi. Hatua hizi pia zinahusiana sana, na hatimaye zitafanikisha wokovu kamili wa wanadamu. Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inatamatisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme, na hatua hii ya kazi huamua hatima ya wanadamu. Tusipoelewa kazi ya Mungu, ni rahisi kukosa nafasi ya mwisho ya kuokolewa na kukamilishwa na Mungu, jambo ambalo litakuwa majuto ya maisha.
Hii inamaanisha kuwa ni muhimu hata zaidi kuelezea hatua tatu za kazi ni nini hasa. Hebu tufikiri, “Kwa nini hatua ya kwanza ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu ilikuwa kufanya kazi ya kutoa sheria?” Kwa sababu mwanzoni, wanadamu walikuwa kama watoto wachanga. Hawakujua jinsi ya kumwabudu Mungu, hawakujua jinsi ya kuishi, na hata kanuni za msingi za maadili, kama vile mauaji na wizi ni dhambi, hazikueleweka. Yehova Mungu alitoa sheria na amri ili kuwafundisha watu jinsi ya kuishi duniani, na Aliwaambia watu wasiue, wasiibe, wasizini, na kadhalika, ili watu wawe na dhana ya msingi kuhusu dhambi, wajue wanayopaswa kufanya na wasiyopaswa kufanya, wajue kushika sheria na kuadhimisha Sabato. Wale walioshika sheria walibarikiwa na Mungu, na wale walioivunja walihukumiwa na walilazimika kutoa sadaka ya kulipia dhambi. Watu walipokiuka sheria na kanuni fulani, hasira na adhabu ya Yehova vilikuja, nao walipigwa mawe au kuteketezwa kwa moto uliotoka mbinguni. Watu wa Israeli walionja utukufu na ghadhabu ya Mungu, pamoja na utunzaji na huruma Yake, na wakasadiki kwamba Yehova Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyeumba mbingu na nchi. Kwa hivyo, wote walimcha Yehova na kutii sheria Yake, waliishi kwa kawaida na kumwabudu Mungu duniani, na waliweza kuishi katika uwepo wa Mungu. Haya ndiyo matokeo yaliyotimizwa na kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Kwa hivyo, je, mwisho wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria ulimaanisha kwamba kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu ilikamilika? Bila shaka, hapana. Ingawa watu katika Enzi ya Sheria walijua dhambi ni nini, jinsi ya kutoa dhabihu na kulipia dhambi, na jinsi ya kumwabudu Mungu, mara nyingi watu walishindwa kushika sheria kutokana na upotovu wa Shetani. Hasa mwishoni mwa Enzi ya Sheria, watu walitenda dhambi mara nyingi zaidi, na hawakuwa na matoleo ya dhambi ya kutosha kuwapatanisha na Mungu. Iwapo kazi ya Mungu ingekoma katika Enzi ya Sheria, watu wangehukumiwa na kuuawa na sheria kwa ajili ya dhambi zao zote, na wanadamu wangeangamizwa kabisa. Kwa hivyo, Yehova Mungu alitumia manabii kuwaambia Waisraeli kwamba Masihi atakuja kama sadaka ya dhambi ili kuwakomboa wanadamu. Unabii ulisema, “Kwani mtoto amezaliwa kwa sababu yetu, sisi tumepewa mwana wa kiume: na mamlaka ya serikali yatakuwa juu ya bega lake: na jina lake litakuwa Wa ajabu, Mshauri, Mungu mwenye nguvu, Baba wa daima, Mfalme yule wa Amani” (Isaya 9:6). “Na Yehova ameweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6). “Wakati utafanya nafsi yake kuwa sadaka ya dhambi” (Isaya 53:10). Baada ya hayo, kama Alivyoahidi, Mungu alikuja na kupata mwili kama Bwana Yesu ili kufanya kazi ya kuwakomboa wanadamu. Alipokuwa akiishi miongoni mwa watu, Bwana Yesu alionyesha ukweli, Akawafundisha watu kuungama dhambi zao na kutubu, kumpenda Bwana kwa moyo wao wote, nafsi na akili zao zote, kuwapenda jirani zao kama wanavyojipeda wenyewe, kumwabudu Mungu katika roho na ukweli, na kadhalika. Ukweli huu ulikamilisha kabisa sheria na kuwapa watu njia mpya ya utendaji. Pia Aliponya wagonjwa, Alitoa pepo, Alisamehe dhambi za watu, Akawapa baraka na neema, na hatimaye Akasulubishwa kama mwili usiokuwa na dhambi. Alichukua dhambi za kila mtu na kuwakomboa wanadamu. Baada ya hapo, watu hawakuhitaji tena kutoa matoleo ya dhabihu walipotenda dhambi. Ilimradi waliomba na kutubu, walisamehewa na kufurahia baraka na neema za Mungu. Watu walipitia tabia ya Mungu ya huruma na upendo, na uhusiano kati ya watu na Mungu ulikuwa wa karibu zaidi. Ni wazi kwamba kazi ya Bwana Yesu ilitimiza kikamilifu unabii wa Agano la Kale. Iliwaokoa watu kutokana na minyororo ya sheria, ikamaliza Enzi ya Sheria, na kuwaleta wanadamu katika Enzi ya Neema. Hii inathibitisha kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwokozi na ujio wa Masihi. Ukweli ulioonyeshwa na Bwana Yesu na kazi Yake ya ukombozi ni onyesho la tabia ya Mungu na yote ambayo Mungu anayo na Aliyo, na unafichua kikamilifu mamlaka na uwezo wa kipekee wa Mungu, jambo ambalo linathibitisha kwamba Bwana Yesu ndiye Mungu mwenye mwili na kwamba Bwana Yesu na Yehova ni Roho mmoja na Mungu mmoja. Ni kama tu Bwana Yesu alivyosema, “Mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya Mimi”” (Yohana 14:10). “Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30). Kazi ya ukombozi na kazi ya Enzi ya Sheria ni hatua mbili tofauti za kazi zilizofanywa katika enzi tofauti na Mungu mmoja. Kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yanavyosema: “Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. … Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akaendeleza kazi ya Yehova na, aidha, Akatekeleza kazi Yake, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe. Walifanya kazi katika awamu mbili zinazotofautiana. Awamu moja ilifanyika katika hekalu, na hiyo nyingine ilifanyika nje ya hekalu. Awamu moja ilikuwa ya kuongoza maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa sheria, na awamu nyingine ilikuwa ya kutoa kafara ya dhambi. Awamu hizi mbili za kazi bila shaka zilikuwa tofauti; huu ni mgawanyiko wa enzi ya zamani na enzi mpya, na hakuna kosa kusema kuwa hizo ni enzi mbili! Maeneo ya kazi yao yalikuwa tofauti, na kiini cha kazi yao kilikuwa tofauti, na lengo la kazi yao lilikuwa tofauti. Kwa hivyo, enzi hizi zinaweza kugawanywa kwa awamu mbili: Agano la Kale na Jipya, ambayo ni kusema, enzi mpya na ya zamani. … Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anazindua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). Enzi ya Neema ilidumu miaka elfu mbili, na karibu waumini wote walifikiri kwamba Bwana Yesu aliposulubishwa ili kuwakomboa wanadamu, kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika, na Bwana atakaporudi katika siku za mwisho, Atawainua waaminifu moja kwa moja hadi mbinguni. Hivyo, hivi ndivyo ilivyo kwa kweli? Ni kweli kwamba waumini wamesamehewa dhambi zao, lakini asili ya watu yenye dhambi bado haijatatuliwa. Bado tunadhibitiwa na asili zetu za dhambi, mara nyingi sisi husema uongo na kutenda dhambi bila hiari, sisi hupigania umaarufu na faida, tuna wivu, tuna kiburi, sisi hujidai na sisi ni waasi, hatuna uwezo wa kuvumilia, hatuwezi kujizoeza kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda, na ni vigumu hata zaidi kumpenda na kumtii Bwana. Kwa miaka elfu mbili, waumini wote wameishi wakiwa wamenaswa katika mzunguko huu wa kutenda dhambi mchana na kuungama usiku, na tunapitia kwa kina mateso ya kuishi katika dhambi. Huu ni ukweli usiopingika. Je, wale wanaoishi katika dhambi namna hii wameokolewa? Je, wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni? Bwana Yesu alisema, “Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34-35). “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45). “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). Mungu ni mwenye haki na ni mtakatifu. Anawezaje kuruhusu watu ambao mara nyingi hutenda dhambi na kumpinga kuingia katika ufalme Wake? Kwa hivyo, Bwana Yesu alipomaliza kazi ya ukombozi, Alisema kwamba Atakuja tena kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na kuwaleta watu katika ufalme. Ni kama tu Bwana Yesu alivyotabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12-13). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17). “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:48). Katika siku za mwisho, Bwana Yesu alirudi katika mwili kama alivyoahidi, kama Mwenyezi Mungu ili kuonyesha ukweli wote unaohitajika kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu na kufanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu, jambo ambalo linasuluhisha kabisa asili ya dhambi ya watu na kuwaruhusu waokolewe kikamilifu na Mungu. Hii inatuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ni “Roho wa ukweli,” na Yeye ni Bwana Yesu anayeonekana na kufanya kazi katika siku za mwisho.
Hebu tuangalie baadhi ya vifungu vya maneno ya Mwenyezi Mungu ili kueleza mambo wazi zaidi. Mwenyezi Mungu anasema, “Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu. Bila shaka, kupata mwili huku hakufanyiki kivyake, bali ni hatua ya tatu ya kazi baada ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kila hatua mpya ya kazi ya Mungu kila mara huleta mwanzo mpya na enzi mpya. Vivyo hivyo kuna mabadiliko yanayokubaliana katika tabia ya Mungu, katika njia Yake ya kufanya kazi, katika sehemu Yake ya kufanya kazi, na katika jina Lake. Ndiyo maana basi ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi ya Mungu katika enzi mpya. Lakini licha ya jinsi anapingwa na mwanadamu, Mungu huendelea kufanya kazi Yake, na daima Yeye huwa Akiongoza wanadamu wote kuendelea mbele. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).
“Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).
“Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). Maneno ya Mwenyezi Mungu yako wazi sana. Kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ilisamehe tu dhambi za watu, lakini haikuondoa asili ya dhambi ya watu au kuwaokoa kabisa watu kutokana na dhambi, kwa hivyo kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu haijakamilika. Kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi iliandalia njia kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kazi ya kuwahukumu, kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu inayofanywa na Mwenyezi Mungu ndiyo hatua ya mwisho ya mpango wa usimamizi wa Mungu, na pia ndiyo hatua muhimu zaidi. Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli, ambao unafichua mafumbo yote katika Biblia pamoja na mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu, pamoja na madhumuni ya mpango wa usimamizi wa Mungu, ukweli wa ndani wa hatua tatu za kazi, fumbo la kupata mwili, jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa watu, mwisho na hatima ya watu wa aina zote, jinsi ufalme wa Kristo utakavyotimizwa duniani, na kadhalika. Mwenyezi Mungu pia anafichua na kuhukumu chanzo cha dhambi ya watu na upinzani wao dhidi ya Mungu, ambacho ni asili za kishetani na tabia za kishetani zilizo ndani ya watu. Pia Anaonyesha vipengele vyote vya ukweli ambavyo watu lazima watekeleze na kuingia katika imani katika Mungu, kama vile maoni wanayofaa kuwa nayo katika kumwamini Mungu, jinsi ya kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, jinsi ya kuwa mtu mwaminifu, jinsi ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na jinsi ya kufikia utiifu kwa Mungu, kumpenda Mungu, n.k. Watu lazima waingie katika uhalisi wa ukweli huu wote ili kuacha kabisa upotovu na kuokolewa kikamilifu na Mungu. Kwa wateule wengi wa Mungu, hukumu, kuadibu, upogoaji, ushughulikiaji, majaribio, na usafishaji ulio katika neno la Mungu umewaruhusu kuelewa polepole na kuchukia tabia na asili zao za kishetani, kutambua kwamba tabia ya Mungu ni takatifu, ni yenye haki, na haiwezi kukosewa, kuwapa hofu ya Mungu mioyoni mwao na toba ya kweli, tabia zao potovu kutakaswa na kubadilishwa, na kupata utiifu wa kweli kwa Mungu. Bila kujali wanakumbana na mateso, dhiki, majaribio, au usafishaji gani, wanaweza kumfuata Mwenyezi Mungu kwa uthabiti, kueneza na kushuhudia injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu, na kutoa shuhuda mzuri wa kumshinda Shetani. Ushuhuda wa uzoefu wao umechapishwa mtandaoni, na hutoa ushuhuda kwa ulimwengu mzima wa kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Watu hawa ndio washindi ambao Mungu atawakamilisha kabla ya maafa makubwa, na wao ni malimbuko, jambo ambalo linatimiza kikamilifu unabii katika Ufunuo, “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo” (Ufunuo 14:4). Na pia ni kama Mwenyezi Mungu asemavyo. “Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, lile linalomiliki mamlaka ya Mungu na lililo na ushuhuda wa Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu). Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli na kukamilisha kazi nzuri sana, jambo ambalo linafichua kikamilifu mamlaka na uwezo wa kipekee wa Mungu, na hii inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Roho mmoja na Mungu mmoja. Kwa hivyo, sasa, hebu tutulie na kufikiri: Isipokuwa Mungu, ni nani awezaye kuonyesha ukweli na kufunua fumbo la mpango wa usimamizi wa Mungu? Ni nani awezaye kufichua chanzo cha dhambi ya watu na upinzani wao dhidi ya Mungu? Isipokuwa Mungu, ni nani awezaye kuhukumu upotovu wa watu na kuwaokoa kabisa wanadamu kutoka dhambini? Ni nani anayeweza kuonyesha tabia ya Mungu takatifu na yenye haki isiyovumilia kosa lolote? Ukweli unathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa vitendo mwenye mwili, Mungu mmoja wa kweli mbaye ndiye mwanzo na mwisho wa vitu vyote!
Kwa hivyo, je, sasa kila mtu anaelewa vizuri? Hatua tatu za kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme ni hatua tatu tofauti za kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu katika enzi tofauti. Kazi ya sheria iliwafundisha wanadamu dhambi ni nini, kazi ya ukombozi ilikomboa dhambi zao, na kazi ya hukumu inawaruhusu kuondoa dhambi. Hatua hizi tatu za kazi zinahusiana sana, kila moja ikitegemea ile iliyotangulia, na hatimaye, watu wanaokolewa kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani na kuletwa katika ufalme wa Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu hutumia kuwasimamia na kuwaokoa wanadamu. Kuanzia mwanzo hadi mwisho, unafanywa na Mungu mmoja. Ingawa jina la Mungu ni tofauti, na mbinu na kazi Yake ni tofauti, asili ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, na tabia ya Mungu ni sawa, na havibadiliki kamwe. Tukiangalia maneno yaliyonenwa na Yehova Mungu katika Enzi ya Sheria, maneno ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, na ya Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme, maneno haya yote ni ukweli. Maneno hayo ni maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu na kile Mungu anacho na alicho, yanatoka kwenye chanzo kimoja, na ni sauti na maneno ya Roho mmoja. Huu ni uthibitisho kwamba hatua tatu za kazi zinafanywa na Mungu mmoja. Ni kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yanavyosema. “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). “Yeye ni Mungu, aliye mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu; lakini pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia Angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoka kutoka dhambi. Leo, pia Anaweza kuwashinda wanadamu ambao hawamjui na kuwafanya wawe chini ya miliki Yake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?