Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

22/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani yake; na kifo na kuzimu zikawatoa waliofariki ambao walikuwa ndani zao: na kila mtu alihukumiwa kulingana na vitendo vyake. Na kifo na kuzimu zikarushwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili. Na yeyote ambaye hakupatikana ameandikwa ndani ya kitabu cha uzima alirushwa katika ziwa la moto” (Ufunuo 20:11-15).

Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Maneno Husika ya Mungu:

“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale, siku za mwisho zitakapowadia, Mungu ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha, Mungu ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote wakipiga magoti ardhini, Atafichua dhambi za kila mwanadamu na hivyo kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na yanatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na yametungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Nasema, kwa vyovyote vile hata picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, bado ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, mwanadamu amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima iwe ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa, na lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia; vinginevyo itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa, kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na mwenye uadhama Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa lazima wawe wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kustaajabisha sana na la kusisimua mno.… Kila mtu hudhani kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu isiyo ya kawaida. Je, unajua, hata hivyo, kwamba Mungu alianza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu kitambo sana na wakati huu wote wewe bado uko katika hali ya kutotambua? Kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu inaanza rasmi, tayari umewadia wakati ambapo Mungu kuzifanya upya mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo tu ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshahitimika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia dunia nzima, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Yeye huendesha usimamizi Wake kwa hatua zilizopimwa na kulingana na mpango Wake kwa kimya, na bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake hukaribia, moja baada ya nyingine, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, na baada yake kiti Chake cha enzi mara moja hushuka kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima! Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho huja kati yetu. Yeye ni hekima, Yeye ni haki na uadhama, na Yeye huja kwa ukimya kati yetu, akiwa na mamlaka na akiwa amejawa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote ambacho yuko karibu kufanya. Maisha ya mwanadamu yanaendelea kama awali moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu huishi kati yetu, mwanadamu kama watu wengine, kama mmoja wa wafuasi wasio na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi ya hayo, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia iko hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya Uchina tu, au kwa idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, Ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kutegemeza kwa kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo Lake la nje au sababu nyinginezo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza.

Umetoholewa kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale wanaotii ukweli na kunyenyekea kwa kazi ya Mungu watakuja chini ya jina la Mungu mwenye mwili wa pili—Mwenyezi. Wataweza kukubali uelekezi binafsi wa Mungu, na watapata ukweli zaidi na wa juu zaidi na watapokea maisha ya kweli ya mwanadamu. Wataona maono ambayo watu wa zamani hawajawahi kuona kamwe: “Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16). Maono haya ni maonyesho ya tabia kamilifu ya Mungu, na maonyesho ya aina hii ya tabia Yake nzima pia ndiyo maonyesho ya kazi ya Mungu Anapopata mwili mara hii. Katika mibubujiko ya kuadibu na hukumu, Mwana wa Adamu Anaonyesha tabia Yake ya asili kupitia kuzungumza kwa maneno, Akiwaruhusu wale wote wanaokubali kuadibu Kwake na hukumu kuuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, uso ulio mfano wa kuaminika wa Mwana wa Adamu Alivyooneka na Yohana. (Bila shaka, yote haya hayatawaonekania wote wasioikubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.) Uso wa kweli wa Mungu hauwezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu, na hivyo Mungu Hutumia maonyesho ya tabia Yake asili kuuonyesha uso Wake wa kweli kwa mwanadamu. Ambayo ni kusema wote ambao wamepitia tabia asili ya Mwana wa Adamu wameuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi na Hawezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu. Mara tu mwanadamu amepitia kila hatua ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, basi atapata kujua maana kamili ya maneno ya Yohana alipozungumza kuhusu Mwana wa Adamu kati ya vinara vya taa: “Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp