Mungu Hutumia Njia Zake Zenye Uweza na Hekima Kuviruzuku Vitu Vyote na Kudumisha Kusalia kwa Wanadamu

08/09/2019

Mungu Hutumia Njia Zake Zenye Uweza na Hekima Kuviruzuku Vitu Vyote na Kudumisha Kusalia kwa Wanadamu

Tumetoka kuzungumzia nini? Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua athari hasi katika mazingira ya wanadamu zilizosababishwa na vitu mbalimbali vya asili ambavyo vinaletwa na mambo yote, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, na Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa na vitu vyote vya asili vyenye manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, ikiwa hivyo viumbe mbalimbali vyenye uhai vyote vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vingekuwa vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama,kwa mfano, simba walipaswa kula vitu kama pundamilia na paa, na chui wakubwa wenye milia walipaswa kula vitu kama kondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula, je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Wanadamu wangeweza kula nyasi ambayo kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa wakijaribu kidogo tu, lakini wakiendelea kula kwa muda mrefu, matumbo ya wanadamu hayataweza kustahimili tena na hawatadumu kwa muda mrefu. Na hata kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila na kufurahia vitu hivi alivyokutayarishia Mungu kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Kwa hivyo, machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chochote kingine chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, ilhali kisiri, au pengine muda mrefu uliopita, Mungu alikuwa tayari amekutayarishia hekima Yake. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na katika usimamizi Wake wa wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu wa wajibu kwao wanadamu ambao Anao tangu Awaumbe, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Zake za uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote. Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Hili ni hakika. Je, mna shaka yoyote? (La.) Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha ruzuku ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea, na hakuna chanzo kingine ila Mungu Mwenyewe. Mungu huruzuku mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni mazingira ya msingi kabisa ya watu kuishi, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Kutokana na mitazamo yote, inapofikia utambulisho wa Mungu na hadhi Yake kwa wanadamu, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hili ni sahihi? (Ndiyo.) Yaani, Mungu ni Mtawala, Bwana, na Mpaji wa dunia hii yakinifu ambayo watu wanaweza kuona kwa macho yao na kuhisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulisho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? (Ndiyo.) Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu.

Wanadamu kuweza kuendelea kuishi na kuzaa kwa kawaida ni jambo la muhimu zaidi kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu daima huwapa wanadamu na vitu vyote. Anapeana vitu vyote kwa njia mbalimbali, na chini ya hali za kudumisha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, Anawawezesha wanadamu kuendelea kusonga mbele ili Aweze kudumisha kuwepo kwa kawaida kwa wanadamu. Hivi ndivyo vipengele viwili tunavyowasiliana leo. Vipengele hivi ni vipi? (Kutokana na mtazamo mkubwa, Mungu aliwaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Hicho ni kipengele cha kwanza. Pia, Mungu alitayarisha hivi vitu yakinifu ambavyo wanadamu wanahitaji na wanaweza kuona na kugusa.) Tumewasilisha mada yetu kuu kupitia vipengele hivi viwili. Mada yetu kuu ni gani? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Mnapaswa sasa kuwa na ufahamu fulani wa mbona Niliwasilisha maudhui haya chini ya mada hii. Je, kumekuwa na majadiliano yoyote yasiyohusiana na mada kuu? Hakuna, sivyo? Labda baada ya kusikia mambo haya, wengine wenu hupata ufahamu fulani na kuhisi kwamba maneno haya ni muhimu sana, lakini wengine huenda wakapata tu ufahamu kidogo wa kawaida na kuhisi kwamba maneno haya hayana maana. Haijalishi vile nyinyi mnaelewa hili wakati huu, mnapoendelea kupitia matukio itafika siku ambayo ufahamu wenu utafikia kiwango fulani, yaani, wakati maarifa yenu ya matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe yatafikia kiwango fulani, mtatumia maneno yenu wenyewe ya kiutendaji kuwasilisha ushuhuda wa maana na wa kweli kuhusu matendo ya Mungu.

Ninafikiri ufahamu wenu sasa bado ni sahili na wa kawaida, lakini mnaweza angaa, baada ya kunisikiliza Nikiwasilisha vipengele hivi viwili, kutambua ni mbinu zipi Mungu hutumia kuwapa wanadamu au ni vitu vipi Mungu huwapa wanadamu? Je, mna wazo la msingi na vilevile ufahamu wa msingi? (Ndiyo.) Lakini vipengele hivi viwili Nilivyowasilisha vinahusiana na Biblia? (La.) Vinahusiana na hukumu na kuadibu kwa Mungu katika Enzi ya Ufalme? (La.) Basi kwa nini Niliwasilisha vipengele hivi? Je, ni kwa sababu watu ni lazima wavielewe ili kumjua Mungu? (Ndiyo.) Ni muhimu sana kuvijua na pia ni muhimu sana kuvielewa. Usizuiwe tu kwa Biblia, na usizuiwe tu kwa Mungu kuhukumu na kuadibu wanadamu ili kuelewa kila kitu kuhusu Mungu. Ni nini kusudi la Mimi kusema hili? Ni ili kuwafanya watu wajue kwamba Mungu si Mungu wa watu Wake wateule pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Mawanda ya kazi Yake na matendo Yake ni yapi? Kwa kiwango kidogo zaidi, mawanada ya kazi Yake na matendo Yake yanajumuisha wanadamu wote na vitu vyote vya uumbaji. Kwa kiwango cha juu inajumuisha ulimwengu wote ambao watu hawawezi kuuona. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Wewe unamwona Mungu kitu kidogo Ni jinsi gani kufanya hivyo kungeathiri watu? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp