Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

04/11/2018

Sasa, hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11: “Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane”? Na hii nafasi iliyokuwa katikati ya nuru na anga ilikuwa nini? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na ardhi na bahari kwenye anga hii, nayo ardhi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na kukawa vivyo hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alitumia matamshi kutimiza mambo haya yote, kuumba uzima wa haya yote.

Kwenye mafungu matatu yaliyo hapo juu, tumejifunza kunatokea matukio matatu makubwa. Matukio haya matatu makubwa yalionekana, na yakaumbwa kuwa hivyo, kupitia kwa matamshi ya Mungu, na ni kwa sababu ya matamshi Yake ndipo, moja baada ya lingine, yaliweza kujitokeza mbele ya macho ya Mungu. Kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba “Mungu huongea, na ikatimizwa; huamuru, na ikawa imara” haya si maneno matupu. Hali hii halisi ya Mungu inathibitishwa wakati ule ambao fikira Zake zinaeleweka, na wakati ambapo Mungu hufungua kinywa Chake kuongea, hali Yake halisi inajionyesha kikamilifu.

Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.” Huku Mungu akiongea, mambo haya yote yaliumbika kufuatia fikira za Mungu, na kwa muda mfupi tu, mseto wa viumbe vidogo vinyonge vyenye maisha vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kusita huku vichwa vyao vikiwa juu kupitia kwenye ardhi, na hata kabla ya kukung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana mikono kusalimiana kwa hamu, kuitikia na kuufurahia ulimwengu. Vilishukuru Muumba kwa maisha aliyovipatia, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa sehemu ya viumbe vyote, na kwamba kila kimojawapo kingejitolea katika maisha yavyo ili viwe vinaonyesha mamlaka ya Muumba. Kama vile matamshi ya Mungu yalivyotamkwa, ardhi ikawa yenye rutuba na kijani, aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu tasa, ambao hakukuwahi kuwepo na chembechembe zozote za maisha, ulifunikwa mara moja na wingi wa nyasi, mimea ya msimu na miti na ilikuwa ikifurika kwa kijani kibichi kingi…. Harufu nzuri ya nyasi na mnukio wa mchanga uliosambazwa kupitia hewani, na mseto wa mimea vyote vilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inanawiri, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilizaliwa na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingepokea matoleo na ustawishaji usiosita wa Muumba, na siku zote ingeendelea kuishi kwa shauku katika kila pembe ya ardhi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na siku zote ingeonyesha nguvu za maisha walizopewa na Muumba …

Maisha ya Muumba ni yale yasiyo ya kawaida, fikira Zake ni zile zisizo za kawaida, na mamlaka Yake ni yale yasiyokuwa ya kawaida, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapofanya matendo; Anatumia tu fikira Zake kutoa amri, na matamshi Yake ili kuagizia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea ya msimu iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yaliwezekana kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.

Wakati Alikuwa aanze kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, na ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika viumbe vyote yalianza kufanyika kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali namna Mungu alivyofanya, au namna Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na ardhi kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na nguvu za maisha ya Muumba zisizo za kawaida na zenye ukubwa. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, lakini mamlaka yanayomiliki nishati kuu na ile isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha viumbe vyote kubadilika, kufufua, kupata nguvu upya, na kuangamia. Kwa sababu ya haya, viumbe vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywa Chake …

Kabla ya viumbe vyote kujitokeza, kwenye akili za Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawa kwenye siku ya tatu mimea aina yote ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kiumbe kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na angeonyesha mamlaka Yake na kuendeleza nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga ili kutayarishia viumbe vyote na mwanadamu ambaye Alinuia kuumba …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp