Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

04/11/2018

Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kujitokeza kwa kila kiumbe kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Wakati huu, moyo Wake ulifaidi sehemu ndogo ya kutosheka, lakini mpango Wake ulikuwa ndio tu umeanza. Punde si punde, siku mpya ilikuwa imewadia—na ukurasa unaofuata ulikuwa upi kwenye mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, kuangaza kwetu kwa macho kunatufikisha kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mpya. Bila shaka, kwa Muumba, bila tashwishi ilikuwa ni siku nyingine nzuri, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa mwanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Ilikuwaje nzuri, ilikuwaje muhimu, na ilikuwaje yenye thamani isiyopimika? Hebu na tuweze kusikiliza matamshi yaliyotamkwa na Muumba….

“Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile” (Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa ardhi kavu na mimea iliyokuwa juu yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa tu rahisi kama kile Alichokuwa tayari Amefanya, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mzuri kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litatimizwa. Mungu aliamuru nuru kujitokeza mbinguni, na nuru hizi hazikuangaza tu kwenye mbingu lakini pia kwenye ardhi, lakini pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na maana ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Nuru kwenye mbingu ni viumbe vilivyo kwenye mbingu vinavyoweza kuonyesha nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mpigo na mara ngapi ambapo vimeamriwa na Mungu, na vinaangaza sehemu mbalimbali zenye vipindi tofauti vya muda kwenye ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya kuzunguka kwa nuru hizi husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa ardhi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia karamu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo nyongeza na saidizi timilifu kwa misimu minne—mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo nuru hizi huhudumu kwa mpangilio maalum kama alama za mara kwa mara na sahihi kwa minajili ya vipimo mbalimbali, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawa ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishaji wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.

Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, miti isiyozaa na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu vitendo vya Muumba vimechangamsha moyo wako na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.

Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza na huvutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kukwepa haya ila kuyaangazia tu macho matendo haya ya kipekee yaliyozaliwa kutokana na utekelezwaji wa mamlaka husika. Nguvu zake za kipekee zafurahisha baada ya kufurahisha, na binadamu anabaki akishangaa na akijawa na furaha, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; nini kingine tena, binadamu amefurahishwa kwa kumtazama alivyo, na kilichozaliwa ndani yake ni heshima, kustahi, na mtagusano wa karibu. Mamlaka na vitendo vya Muumba vinayo athari kwa roho ya binadamu na hutakasa roho ya binadamu na zaidi, kutosheleza roho ya binadamu. Kila mojawapo ya fikira Zake, kila mojawapo ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kiungo muhimu miongoni mwa viumbe vyote, na ni utekelezaji mkuu wenye thamani zaidi wa kuunda ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote.

Hebu tuendelee kusoma Maandiko fungu hadi fungu, tunapoangalia vitendo vingi zaidi vya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp