Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti

04/11/2018

Maandiko yanasema, “Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri” (Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa hewani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu …

Kama vile maneno ya Mungu yalivyotamkwa, maisha mapya mazuri, kila mojawapo ikiwa na umbo tofauti, kwa ghafla vilipata uhai miongoni mwa matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikijitikisatikisa kwa minajili ya kupata nafasi, kuruka, kurukaruka kwa furaha…. Samaki wa maumbo na ukubwa wote waliweza kuogelea majini; samakigamba wa kila aina waliweza kukua kwenye michanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za mwani kuanza kukua kwa haraka, ikiyumbayumba kutokana na msongo wa maisha mbalimbali ya majini, yasiyosita, na yanayosihi yale maji tulivu, ni kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki wako! Kwani hutawahi kuwa pekee tena! Kuanzia muda ule ambao viumbe mbalimbali vilivyo na uhai viliumbwa na Mungu na kuonekana majini, kila maisha mapya yalileta nguvu kwenye maji yaliyokuwa tulivu kwa muda mrefu, na kuweza kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia hapo kwenda mbele, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kutangamana pamoja, na havikuweka umbali kati yao. Yale maji yalikuwepo kwa minajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakipatia uhai kila maisha yaliyokuwa karibu na kumbatio lake, na kila maisha yalikuwepo kwa minajili ya maji kwa sababu ya uhai wake. Kila moja ilipatia uhai mwenzake, na wakati uo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitolea ushuhuda wa miujiza na ukubwa wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizoshindwa za mamlaka ya Muumba …

Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti

Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia maisha yalivyoanza kujaza mbingu. Mmoja baada ya mwingine, ndege, wakubwa na wadogo, walipaa kwenye mbingu kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye neema. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na mbinu walizopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa mbinu walizokuwa nazo wakapaa katikati ya mbingu na ardhi, kotekote kwenye mbuga na misitu…. Walikuwa ndio wapenzi wa hewani, walikuwa ndio wapenzi wa viumbe vyote. Hivi punde ndio wangekuwa kiunganishi kati ya mbingu na ardhi, na wangepitisha ujumbe kwa viumbe vyote…. Waliimba, wakawa wanapaapaa kwa furaha kotekote, walileta vifijo, vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia kuimba kwao kwa uwazi, kuvutia, na kutumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kusifu Muumba kwa maisha aliyowapa. Walicheza kwa uchangamfu ili kuonyesha utimilifu na miujiza ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia agano la mamlaka ya Muumba kupitia kwenye maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa …

Licha ya kama vilikuwa majini, au mbinguni, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hivi hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Havikuwahi kuthubutu kwenda nje ya mipaka viliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaana, na kutii kwa umakinifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa kufahamu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na amri na maagizo ya mbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao wenyewe maalum, na wakashukuru maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti viumbe vyote kwa kimya ambacho hakikumiliki matumizi yoyote ya lugha, na iliyokuwa tofauti na mwanadamu. Utiliaji mkazo wa mamlaka Yake kwa njia hii maalum ulimshawishi binadamu kupata maarifa mapya, na kuufanya ufasiri mpya wa mamlaka ya kipekee ya Mungu. Hapa, lazima Niwaambie kwamba kwenye siku hii mpya, ule utiliaji mkazo wa mamlaka ya Muumba ulionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.

Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya fungu hili la maandiko: “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama viumbe vyote Alivyokuwa ameumba vikiumbika na kusimama wima kwa sababu ya matamshi Yake, na kwa utaratibu vikianza kubadilika. Wakati huu, Mungu alikuwa ametosheka na mambo mbalimbali Aliyoyaumba kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Wewe unaona nini hapa? Kinawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepangilia na kushauri, kukamilisha shabaha Alizokuwa ameweka wazi ili kuzikamilisha. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, Hakujutia chochote, lakini Alitosheka. Ni nini maana ya Yeye kutojutia chochote? Tunaelezewa kwamba Mpango wa Mungu ni mtimilifu, kwamba nguvu na hekima Zake ni timilifu, na hiyo ni kutokana tu na mamlaka Yake kwamba utimilifu kama huo unaweza kukamilishwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kukamilika na kuwa timilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho timilifu, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia utimilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa kizuri, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu akaona kwamba ni vizuri,” kila kitu Alichoumba kikachukua mfumo wa kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa mahali maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu. Vilevile, wajibu wao miongoni mwa viumbe vyote na safari ambayo lazima waabiri kwenye usimamizi wa Mungu wa viumbe vyote, ulikuwa tayari umeamriwa na Mungu, na usingebadilishwa. Hii ilikuwa sheria ya mbinguni iliyotolewa na Muumba kwa viumbe vyote.

“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” matamshi haya mepesi, yasiyopongezwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ndiyo matamshi ya sheria ya mbinguni na maelekezo ya mbinguni kwa viumbe vyote kutoka kwa Mungu. Ni mfano mwingine halisi wa mamlaka ya Muumba, mfano ambao ni wa kimatendo zaidi na unaojitokeza zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote pia vilizaa, vikawepo na vikaangamia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itabatilishwa na Muumba! Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp