Kumfafanua Mungu mmoja wa kweli kama Mungu wa utatu ni kumkana na kumkufuru Mungu

24/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Utatu Mtakatifu haupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, vivyo hivyo hakuna dhana ya chombo kitumiwacho kwa pamoja na Baba na Mwana: Roho Mtakatifu. Huu wote ni uongo mkubwa zaidi na haupo kabisa katika dunia hii! Hata hivyo uongo huu una asili yake na haukosi msingi kabisa, kwani akili zenu si punguani, na mawazo yenu hayakosi mantiki. Badala yake, ziko sawa na yenye ubunifu kwa kiasi kikubwa, kwamba haziwezi kuzuiwa hata na Shetani yeyote. La kusikitisha ni kwamba mawazo haya ni uongo mtupu na hayapo kabisa! Hamjaona ukweli halisi haswa; mnabuni na kujiundia dhana, na kuzitengeneza kuwa hadithi ili kuteka imani ya wengine kwa uongo na kupata mamlaka miongoni mwa wanadamu wapumbavu wasio na busara, ili kwamba waamini katika “mafundisho yenu ya kitaaluma” makuu na mashuhuri. Je, huu ni ukweli? Je, hii ndiyo njia ya uzima ambayo wanadamu wanafaa kupokea? Huu ni upuuzi! Hakuna hata neno moja linafaa! Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu? Je, bado mngemrudia? Ningechelewa hata kidogo, inaonekana kwamba mngewarudisha “Baba na Mwana,” Yehova na Yesu kwenda Israeli na mdai kwamba nyinyi wenyewe ni sehemu ya Mungu. Kwa bahati nzuri, sasa ni siku za mwisho. Hatimaye, siku Niliyoitarajia kwa hamu imewadia, na ni baada tu ya kuifanya hatua hii ya kazi kwa mikono Yangu ndipo kumgawanya kwenu Mungu Mwenyewe kumesitishwa. Isingekuwa hivi, mngezidisha, hadi kuwaweka Mashetani wote miongoni mwenu kwenye madhabahu kwa ibada. Hii ndiyo njama yenu! Mbinu yenu ya kumgawanya Mungu! Je, mtaendelea kufanya hivyo sasa? Hebu Niwaulize: Kuna Mungu Wangapi? Ni Mungu Yupi atawaletea wokovu? Je, ni Mungu wa kwanza, wa pili au wa tatu mnayemwomba? Ni nani kati Yao mnayemwamini? Je, ni Baba? Au ni Mwana? Au ni Roho? Niambie ni nani unayemwamini. Ijapokuwa kwa kila neno unasema unamwamini Mungu, mnachokiamini hasa ni akili zenu! Hamna Mungu mioyoni mwenu kabisa! Na bado akilini mwenu mna “Utatu Mtakatifu” kadhaa. Hamkubaliani na hili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Kumjua Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung’amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri kwa masikio, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Hatakosa kuyasifu maarifa yako tu, bali pia atakuadhibu kwa kuwa mwenye dhambi aliyemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na maneno yako yaweza kuwafufua wafu, na kuwaua walio hai, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kuhukumu kwa urahisi, ama kusifu bila mpango, ama kupaka tope bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na watu wowote, ilhali unajitahidi kupata maneno sahihi ya kuelezea ukuu wa wema na neema za Mungu—hili ndilo mshindwa yeyote hujifunza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp