Mfano wa Kondoo Aliyepotea
Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.
Kifungu hiki ni fumbo—ni hisia gani watu wanapata kutokana fumbo hili? Namna ya kujieleza—fumbo—lilitumika hapa ni mbinu za lugha katika lugha ya binadamu, na kwa hivi ni kitu kilicho ndani ya mawanda ya maarifa ya binadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba hakikuambatana na Alichokuwa Mungu, lakini Mwana wa Adamu alipoonyesha kifungu hiki katika Enzi ya Neema, kilionekana cha kufariji, chenye uzuri, na kilicho karibu kwa watu. Mungu alipokuwa mwili, Alipoonekana katika umbo la binadamu, Alitumia sitiari inayofaa sana kuonyesha sauti ya roho Yake katika ubinadamu. Sauti hii iliwakilisha sauti binafsi ya Mungu na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa binadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mwelekeo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya binadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliwaelezea au “kuwatafsiria” binadamu lugha Yake ya maana sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuelewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Angeweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuongea na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu waweze kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili wangeweza kuuona moyo Wake. Mnaona nini katika hili? Kwamba hakuna kuzuiliwa katika maneno na vitendo vya Mungu? Namna watu wanavyoona, hakuna njia ambayo Mungu angetumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia aina hii ya sitiari ili watu waweze kuhisi ule uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mwelekeo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha muda. Mfano huu uliwazindua watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhemsha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kukisoma kifungu cha mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kuwaokoa binadamu na wanaelewa uzito wa mwanadamu katika moyo Wake.
Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika dondoo hii: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Haya yalikuwa maneno binafsi ya Bwana Yesu, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, yaonekana alikuwa Bwana Yesu akiongea, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndiyo maana Akasema: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Watu wakati huo walimtambua tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na mtu huyu waliyeona mbele ya macho yao alikuwa ametumwa tu na Yeye, na hakuweza kuwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kusema hivyo vilevile, ili waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi ule uhalali na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na ufiche wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika ulimwengu wa kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu walichohitaji, Alijua ni nini watu walikuwa na wasiwasi kuhusu, na kile kilichowakanganya, hivyo Akaongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile ambacho Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini usahihi wao na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano mgumu sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu kufanya kazi katika mwili kulikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili shaka na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na kutochangamka kwao. Yaweza kusemekana kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na mwanadamu, na kuhisi mashindano yao akishindana dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikuwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kushinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile Alicho nacho na kile Alicho, kupitia kiini Chake binafsi halisi. Haikuwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile Alicho nacho na kile Alicho, na upendo na hekima Yake. Aliwapata watu Aliowataka, kushinda utambulisho na hadhi Aliyostahili, na “kurudi” kwa kiti Chake cha enzi.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?