Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo? Ni nini asili yao?

24/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Naye akaanza kuzungumza nao kwa kutumia mifano. Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu, naye akalizingira kwa ugo, naye akachimba mahala pa shinikizo ya zabibu, naye akaunda mnara, naye akalipanga kwa wakulima, na kuenda katika nchi ya mbali. Na kwa majira yake akamtuma mtumishi kwa wakulima wale, ili aweze kupata matunda ya shamba hilo la mizabibu kutoka kwa wakulima. Nao wakamkamata, na kumpiga, na kumtoa humo bila chochote. Na tena akamtuma mtumishi mwingine; nao wakamtupia mawe, na kumjeruhi kichwani, na kumwondoa humo kwa aibu. Na tena akamtuma mwingine; nao wakamwua, na wengine wengi; wakiwapiga wengine, na kuwaua wengine. Kwa sababu alikuwa na mwana mmoja, aliyempenda sana, alimtuma pia kwao mwisho, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wakulima hao waliambiana, Huyu ndiye mrithi; njooni, acha tumwue, na urithi wake utakuwa wetu. Nao wakamchukua, na kumwua, na kumtupa nje ya shamba la mizabibu. Bwana wa shamba hilo la mizabibu atafanyaje basi? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, naye atawapa wengine lile shamba la mizabibu” (Marka 12:1-9).

“Ole wenu, ninyi waandishi na Mafarisayo, wazandiki! … Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu?” (Mathayo 23:29-33).

Maneno Husika ya Mungu:

Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kuhusu uaminifu wako hadharani, bali tumia matendo yako halisi ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. …

Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo watakaoonekana katika siku za mwisho, na watu kuwa wanaowadanganya wanadamu. Makristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na mtu wa aina hii. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?

kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi” wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[1] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[2] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Tanbihi:

1. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

2. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp