Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili ili kutumika kama sadaka ya dhambi kwa wanadamu, akiwaokoa kutoka kwa dhambi. Katika siku za mwisho Mungu amepata mwili tena ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa. Kwa nini Mungu anahitaji kuwa mwili mara mbili ili kufanya kazi ya kumwokoa wanadamu? Na kuna umuhimu gani wa Mungu kuwa mwili mara mbili?

07/06/2019

Jibu:

Ni kwa nini lazima Mungu apate mwili mara mbili kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu? Tunapaswa kuelewa vizuri kwanza: Kuhusu wokovu wa wanadamu, kupata mwili kwa Mungu mara mbili kuna maana ya kina na kubwa. Kwa sababu kazi ya wokovu, haijalishi kama tunazungumza kuhusu ukombozi au hukumu na utakaso katika siku za mwisho, haiwezi kutekelezwa na mwanadamu. Inahitaji Mungu kupata mwili na kutekeleza kazi hiyo Mwenyewe. Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu, yaani, Roho wa Mungu alijivika mwili mtakatifu na usio na dhambi, na alipigiliwa misumari msalabani kutumika kama dhabihu ya dhambi, Akamkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi yake. Ndiyo. Sote tunalifahamu hili. Lakini kuhusu kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, kwa nini Anapata mwili kama Mwana wa Adamu kuonekana na kufanya kazi? Wengi wana wakati mgumu kulielewa hili. Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa amekieleza kipengele hiki cha ukweli na kufichua siri hii, hakuna ambaye angeelewa ukweli huu. Sasa, Hebu tuone hasa kile ambacho Mwenyezi Mungu amesema.

Mwenyezi Mungu asema, “Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu amekuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Ni kwa namna hii tu ndipo Ataweza kuwapa wanadamu njia ya vitendo wanayohitaji kama viumbe. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki ni mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa njia zote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wameainishwa kulingana na aina. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona kwamba katika Enzi ya Neema Mungu alipata mwili mara ya kwanza kufanya kazi ya ukombozi tu, Akitumia usulubisho kama dhabihu ya dhambi kuwakomboa wanadamu kutoka kwa dhambi yao, kumpumzisha mwanadamu kutoka kwa laana na shutuma za sheria. Tulihitaji tu kukiri dhambi zetu na kutubu na dhambi zetu zingesamehewa. Kisha tungefurahia neema na ukweli mwingi. Kisha tungefurahia neema na ukweli mwingi ambao Mungu alitupa. Hii ni kazi ya ukombozi ambayo Bwana Yesu alifanya, na ni maana ya kweli ya kuokolewa kwa imani katika Bwana. Ingawa Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu, bado hatujajipokonya kutoka kwa minyororo ya dhambi, kwani bado tunamiliki asili yetu ya dhambi na tabia ya kishetani. Ingawa tumekiri dhambi zetu kwa Bwana na tumepata msamaha Wake, hatuna ufahamu wa asili yetu ya dhambi, na hata tuna ufahamu mchache wa tabia yetu potovu, hali iliyo mbaya zaidi kuliko dhambi. Tunaweza tu kutambua hiyo dhambi iliyo ndani yetu ambayo ina uhalifu, na ile ambayo inasababisha kushtakiwa kwa dhamiri yetu. Bali tunakosa kutambua dhambi ya kina zaidi, dhambi ya kumpinga Mungu. Kwa mfano, hatufahamu mzizi wa sisi kumpinga Mungu, au jinsi tabia yetu ya kishetani inadhihirishwa, jinsi asili yetu ya kishetani ilitokea, sumu gani za Shetani ziko ndani ya asili yetu, mahali ambapo falsafa za mwanadamu za kishetani na mantiki na sheria za kishetani zinatoka. Kwa hiyo kwa nini mwanadamu hana ufahamu wa mambo haya ya kishetani? Kwa kuwa mwanadamu amesamehewa dhambi zake na Bwana Yesu, mbona asijipokonye kutoka kwa minyororo ya dhambi, na kwa nini anaendelea hata kutenda dhambi hizo hizo? Je, mwanadamu huwa mtakatifu kweli baada ya kusamehewa dhambi zake? Hili kweli ni suala halisi ambalo hakuna mtu katika Enzi ya Neema anaonekana kulielewa. Ingawa katika kumwamini kwetu Bwana, tunasamehewa dhambi zetu, bado sisi hutenda dhambi, humpinga na kumsaliti Mungu bila kufahamu. Sisi waumini tuna ufahamu wa moja kwa moja wa hili. Kwa mfano, hata baada ya kumwamini Bwana, tunaendelea kudanganya, kuwa wa majisifu, kudharau ukweli na kutetea uovu. Sisi bado ni wenye kiburi, waovu, wachoyo na wenye tamaa; tumenaswa bila msaada katika tabia potovu ya Shetani. Wanadamu wengi humfanyia Bwana kazi bila kuchoka, lakini wanafanya hivyo kwa matumaini ya kupewa thawabu na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Wanapofurahia neema ya Bwana wanakuwa na furaha na imara katika imani yao kwa Bwana; lakini punde tu wanapokabiliwa na maafa, au kuna msiba katika familia, wanamwelewa visivyo, wanamlaumu na hata kumkana na kumsaliti Bwana. Mara tu kazi ya Mungu inapokosa kulingana na dhana na njozi zao, wanatenda kama Mafarisayo wanafiki, wakimpinga na kumshutumu Mungu. Tuna uzoefu wa moja kwa moja wa jambo hili. Hiki chote kinathibitisha nini? Hili linaonyesha kwamba ingawa tulikubali wokovu wa Bwana Yesu na tulisamehewa dhambi zetu, hili halimaanishi kwamba tumejisafisha kabisa dhambi na sasa tumetakaswa, sembuse kumaanisha kwamba tumekuwa wa Mungu na tumepatwa na Mungu. Kwa hiyo, wakati Bwana Yesu anarudi tena kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, wengi kutoka kwa ulimwengu wa dini wanakuja kumhukumu, kumshutumu na kumkufuru Mungu, wakimtangaza hadharani kuwa adui yao na wakimpigilia misumari tena msalabani. Je, wale wanaomshutumu na kumpinga Mungu hadharani wanaweza kunyakuliwa katika ufalme wa mbinguni kwa msingi wa dhambi zao kusamehewa tu? Je, Mungu angeweza kuruhusu hizi nguvu za uovu zinazompinga Mungu kuingia katika ufalme wa mbinguni? Je, Mungu angewanyakua hawa wapinga Kristo, hawa wanaochukia ukweli, kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama mnavyoona, ingawa tumesamehewa dhambi zetu kupitia kwa imani yetu kwa Bwana, hatujajisafisha kutoka kwa dhambi kabisa, kujisafisha kutoka kwa ushawishi wa kishetani, na hata kidogo zaidi kupatwa na Mungu na kuwa wa Mungu. Kwa hiyo, ikiwa tunataka kujiondolea dhambi na kupata utakaso, kupatwa kikamilifu na Mungu, lazima tutakaswe na kuokolewa kabisa na kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu.

Tuna maoni rahisi sana ya kazi ya Mungu ya wokovu, kana kwamba mara tu dhambi za mwanadamu ziliposamehewa hakukuwa na matatizo mengine, na chote kilichosalia kilikuwa tu kungoja kunyakuliwa na Bwana kuingia katika ufalme wa mbinguni. Mwanadamu mpotovu ni mjinga na mpuuzi kweli! Dhana na njozi za mwanadamu mpotovu ni za dhihaka kweli! Je, dhambi ndilo tatizo pekee lililowatesa wanadamu baada ya kupotoshwa na Shetani? Kiini cha dhambi ya mwanadamu ni nini? Dhambi ni nini? Kwa nini Mungu anaichukia sana? Kufikia siku hii, hakuna aliye na ufahamu kamili. Mwanadamu amepotoshwa na Shetani kabisa, upotovu wake unafikia kiwango gani? Hakuna anayeelewa vizuri. Uhalisi wa kupotoshwa kwa mwanadamu kabisa ulidhihirishwa wakati wa usulubishaji wa Bwana Yesu. Ukweli kuwa wanadamu wangeweza kumsulubisha Bwana Yesu mwenye huruma, Aliyekuwa ameonyesha ukweli mwingi sana, kunaonyesha kweli kwamba mwanadamu alikuwa amekuwa ukoo wa Shetani, na mtoto wa Shetani, na alikuwa amepoteza ubinadamu wake kabisa, hata hakuwa na kiasi kidogo cha urazini au dhamiri. Nani kati ya wanadamu bado ana ubinadamu wa kawaida? Je, upinzani na uhasama wa mwanadamu kwa Mungu hauonyeshi kwamba mwanadamu amefikia kiwango ambapo ama ni yeye au ni Yeye, ambapo hawezi kupatanishwa na Mungu? Je, tatizo hili linaweza kweli kutatuliwa kwa kusamehewa dhambi zake? Nani anaweza kuhakikisha kwamba kwa kusamehewa dhambi zake, mwanadamu hatampinga Mungu au kumchukulia kuwa adui? Hakuna anayeweza kuhakikisha hili! Dhambi za mwanadamu zinaweza kusamehewa, lakini je, Mungu anaweza kuisamehe asili ya mwanadamu? Asili ambayo inampinga Mungu? Je, Mungu anaweza kusamehe tabia ya kishetani ya mwanadamu inayomjaza? Basi, Mungu huvitatua vipi vitu hivi ambavyo ni vya Shetani? Bila shaka, Mungu hutumia hukumu na kuadibu. Na kwa wale ambao kamwe hawatubu, Mungu atawaangamiza kwa maafa. Ni haki kusema, bila hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa haki, mwanadamu mpotovu hangeshindwa, sembuse kuzama ardhini kwa fedheha kuu. Hii ndiyo sababu kuu kwa nini Mungu lazima apate mwili kufanya kazi ya hukumu. Kuna wengi ambao hushuku na wana dhana kuhusu Mungu kupata mwili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Ni kwa nini? Hili ni kwa sababu wanakosa kuona uhalisi wa upotovu kamili wa mwanadamu. Kwa hiyo, kutokana na hilo, hawana ufahamu hata kidogo wa maana ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. wanakosa kutafuta na kuchunguza njia ya kweli. Kwa namna hii, wangewezaje kukubali na kutii kazi ya Mungu?

Sisi wanadamu hatuwezi kufahamu kina kikubwa cha umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu mara mbili. Kwa hiyo, kuhusu ni kwa nini Mungu amepata mwili mara mbili, na nini maana ya kupata mwili huko mara mbili ni, kwa hali hii ya ukweli, hebu twende kwa vifungu viwili kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu asema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).

Ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba ‘Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, na si binadamu kabisa,’ ni kufuru, kwa kuwa kauli hii haipo kabisa, na hukiuka kanuni ya Yesu kupata mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).

Haijalishi enzi ama mahali ambapo Mungu anapata mwili, kanuni za kazi Yake katika mwili Wake hazibadiliki. Hawezi kuwa Mwili kisha Avuke mwili kwa kufanya kazi; zaidi, hawezi kuwa mwili kisha Akose kufanya kazi katika mwili wa kawaida wa binadamu. Vinginevyo, umuhimu wa Mungu kupata mwili utapotea na kuwa bure, na Neno kuwa mwili itakuwa haina maana. Zaidi ya hayo, Baba tu Aliye mbinguni (Roho) Anajua kuhusu Mungu katika mwili wa Mungu, na sio mwingine, sio hata mwili Mwenyewe ama wajumbe wa mbinguni. Hivyo, kazi ya Mungu katika mwili ni ya kawaida zaidi na bora kueleza Neno kuwa mwili; mwili unamaanisha mwanadamu wa kawaida(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)).

Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu katika ubinadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu. … Kuwa Yeye ana ubinadamu wa kawaida kunathibitisha kuwa Yeye ni Mungu Aliyejidhihirisha katika mwili; ukweli kwamba Anapitia ukuaji wa kawaida wa binadamu unaonyesha zaidi kuwa Yeye ni mwili wa kawaida; zaidi, kazi Yake ni uthibitisho tosha kuwa Yeye ni Neno la Mungu, Roho wa Mungu, kuwa mwili. Mungu Anakuwa mwili kwa sababu ya mahitaji ya kazi; kwa maneno mengine, hii hatua ya kazi inapaswa kufanywa kwa mwili, kufanywa katika ubinadamu wa kawaida. Hili ndilo sharti la ‘Neno kuwa mwili,’ la ‘Neno kuonekana katika mwili,’ na ndio ukweli wa Mungu kupata mwili mara Mbili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).

Kwa nini Ninasema kuwa maana ya kupata mwili haikukamilishwa katika kazi ya Yesu? Ni kwa sababu Neno halikuwa Mwili kikamilifu. Kilichofanywa na Yesu kilikuwa tu sehemu moja ya kazi ya Mungu katika mwili; Alifanya tu kazi ya ukombozi na Hakufanya kazi ya kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, Mungu Amekuwa mwili mara nyingine tena katika siku za mwisho. Hatua hii ya kazi, pia inafanywa katika mwili wa kawaida, ikifanywa na mwanadamu wa kawaida kabisa, ambaye ubinadamu wake haupiti mipaka ya ubinadamu. Kwa maneno mengine, Mungu Amekuwa mwanadamu kamili, na ni mtu ambaye utambulisho wake ni ule wa Mungu, mwanadamu kamili, mwili kamili, Ambaye Anatekeleza kazi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).

Neno la Mwenyezi Mungu limefichua umuhimu na siri ya kupata mwili. Kutokana na kusoma neno la Mwenyezi Mungu tunajua kwamba kupata mwili kunahusu Roho wa Mungu kuvishwa mwili na kugeuka kuwa mtu wa kawaida kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Mungu aliyepata mwili lazima awe na ubinadamu wa kawaida, lazima afanye kazi na kunena ndani ya ubinadamu wa kawaida. Hata anapofanya miujiza, lazima ifanywe ndani ya ubinadamu wa kawaida. Katika sura ya nje, Mungu mwenye mwili anaonekana wa kawaida. Anaonekana kufanya kazi Yake kama mwanadamu wastani, wa kawaida. Kama Hangekuwa na ubinadamu wa kawaida na kufanya kazi katika ubinadamu Wake wa kawaida, Hangekuwa kupata mwili kwa Mungu. Kupata mwili kunamaanisha Roho wa Mungu anapatikana katika mwili. Katika ubinadamu wa kawaida, Anaonyesha ukweli na Anafanya kazi ya Mungu Mwenyewe, Akikomboa na kuwaokoa wanadamu. Huu ndio umuhimu wa kupata mwili. Sasa ni nini umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu mara mbili? Kinachomaanishwa hasa ni kwamba kupata mwili kwa Mungu mara mbili wamekamilisha umuhimu wa kupata mwili, wametimiza kazi ya Neno kuonekana katika mwili na kukamilisha mpango wa usimamizi wa Mungu kuwaokoa wanadamu. Huu ndio umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu mara mbili. Sote tunapaswa kuelewa vizuri kusudi la kupata mwili kwa Mungu mara ya kwanza lilikuwa kufanya kazi ya ukombozi na kutayarisha njia kwa ajili ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa hiyo, kupata mwili kwa Mungu mara ya kwanza hakukamilisha umuhimu wa kupata mwili. kusudi la kupata mwili kwa Mungu mara ya pili ni kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho na kuwapokonya wanadamu kabisa kutoka kwa kukamatwa na Shetani, kuwapumzisha wanadamu kutoka kwa tabia zake za kishetani, kumweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani ili aweze kurudi kwa Mungu na apatwe naye. Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, Ameonyesha ukamilifu wa ukweli kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Amekamilisha kazi yote ya Mungu katika mwili, na Ameonyesha yote ambayo Mungu lazima Aonyesha katika mwili Wake. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo Amekamilisha kazi ya Neno kuonekana katika mwili. Hebu tusome vifungu vingine viwili kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu asema, “Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). “Hatua hii ya kazi hasa inatimiza maana ya ndani ya ‘Neno lakuwa mwili,’ ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya ‘naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,’ na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno ‘Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.’ Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na katika enzi ya mwisho, Yeye anafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumruhusu mwanadamu kuziona njia Zake zote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uelewe mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la jinsi unavyouelewa mwili na Neno. Huu ndio ushuhuda unaopaswa kuwa nao, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kuitamatisha enzi ya Mungu kuwa katika mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)). Kupata mwili kwa Mungu mara mbili kunakamilisha kazi yote ya Mungu katika mwili, yaani, kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kabisa. Kwa hiyo, katika siku za baadaye, Mungu hatapata mwili tena. Hakutakuwa na mara ya tatu au mara ya nne. Kwa sababu kazi ya Mungu katika mwili tayari imekamilishwa kwa ukamilifu. Hiki ndicho kinamaanishwa na kauli kwamba Mungu amepata mwili mara mbili kukamilisha umuhimu wa kupata mwili.

Mungu amepata mwili mara mbili kukamilisha umuhimu wa kupata mwili. Kwa wale ambao bado hawajapitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, hili ni gumu kuelewa. Wale waliopitia tu kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema wanajua kwamba Bwana Yesu ni Mungu aliyepata mwili. Lakini wachache wanafahamu kwamba kazi ya Bwana Yesu ilikuwa ni ukombozi pekee na Hakukamilisha kazi ya Neno kuonekana katika mwili. Ambalo ni kusema, Bwana Yesu hakuonyesha ukamilifu wa ukweli wa wokovu kamili wa wanadamu wa Mungu aliyepata mwili. Kwa hiyo Bwana Yesu akasema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Sasa Bwana Yesu amerudi katika mwili kama Mwana wa Adamu. Yeye ni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Yuko hapa Akifanya kazi ya hukumu akianzia nyumba ya Mungu, hapa Akionyesha ukweli kamili ambao utawatakasa na kuwaokoa wanadamu, ukweli ulio katika “Neno Laonekana katika Mwili.” Mungu mwenye mwili Anazungumza kwa mara ya kwanza katika utambulisho wa Mungu kwa ulimwengu mzima, Akitangaza neno Lake. Anatangaza utondoti wa mpango wa usimamizi wa Mungu kuwaokoa wanadamu, Anaonyesha mapenzi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu wote na hatima ya mwanadamu.

Hebu tuone jinsi Mwenyezi Mungu analieleza hili: “Ni haki kusema kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza tangu uumbaji kwa Mungu kuwahutubia wanadamu wote. Mungu hakuwa amewahi kuzungumza kwa wanadamu walioumbwa kinaganaga hivyo na kwa utaratibu sana. Bila shaka, hiyo pia ilikuwa mara ya kwanza Alipozungumza mengi hivyo, na kwa muda mrefu sana, kwa wanadamu wote. Ilikuwa ya kipekee kabisa. Na zaidi, matamshi haya yalikuwa maneno halisi ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ambapo Aliwafichua watu, akawaongoza, akawahukumu, na kuzungumza nao wazi wazi na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu wajue nyayo Zake, mahali Anapokaa, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, mawazo ya Mungu, na sikitiko Lake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amezungumza kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambapo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu katikati ya maneno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Utangulizi).

Hii ni kwa sababu Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na kuanzia sasa na kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wale wote wasionijua waweze kuyafurahisha macho yao na kuona kwamba kweli, Nimekuja katika ulimwengu wa kibinadamu, Nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, na ‘kukiri’ Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Nawaomba mzingatie kwa makini kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinawakaribia wanadamu tena, kwa wale wote wanaonipinga(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako).

Kuhusu kupata mwili kwa Mungu mara mbili kukamilisha umuhimu wa kupata mwili, kuna wale wasioelewa kabisa, kwa sababu wanakosa uzoefu. Wanaposikia kulihusu, hawaelewi tu. Sasa hebu tuingie katika utondoti wa kazi iliyotekelezwa wakati wa kupata mwili kwa Mungu mara mbili. Wakati wa kupata mwili kwa Mungu mara ya kwanza, Alitekeleza kazi ya ukombozi, Akidhihirisha miujiza mingi: Aliwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano tu na samaki wawili. Alituliza upepo na mawimbi kwa neno moja tu. Alimfufua Lazaro. Pia, Bwana Yesu alifunga na Akajaribiwa jangwani kwa siku arobaini. Alitembea juu ya bahari, n.k. Kwa kuwa mwili wa Bwana Yesu ulifanya miujiza, na Alibadilishwa juu ya mlima, machoni mwetu wanadamu, ingawa Bwana Yesu alipata mwili, bado alikuwa na sifa za ajabu. Alikuwa tofauti kuliko mtu wa wastani, miujiza ilifuata wakati wowote Alipoonekana. Pia, Bwana Yesu alifanya tu hatua moja ya kazi, kazi ya ukombozi. Alionyesha tu ukweli wa kazi ya ukombozi, hasa kudhihirisha tabia ya Mungu ya huruma na upendo. Hakuonyesha ukweli wote wa kazi ya hukumu na wokovu, na Hakuonyesha kwa mwanadamu tabia ya Mungu yenye haki, takatifu na isiyokosewa. Kwa hiyo haiwezi kusemekana kwamba mwenye mwili wa kwanza Alikamilisha maana ya kupata mwili. Kama tu asemavyo Mwenyezi Mungu, “Hatua ya kazi ambayo Yesu alitekeleza ilitimiza tu kiini cha ‘Neno alikuwako kwa Mungu’: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka katika mwili huo. Yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa kupata mwili wa kwanza wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)). Kupata mwili kwa Mungu katika siku za mwisho ni tofauti na kupata mwili wa kwanza. Katika kupata mwili wa pili, Mungu hajafanya miujiza, Yeye si wa ajabu kabisa. Katika sura ya nje Anafanana na mwanadamu wa kawaida, Akifanya kazi Yake na kunena neno Lake kwa uhalisi na kwa kweli miongoni mwa wanadamu. Ameonyesha ukweli kuhukumu, kutakasa na kumkamilisha mwanadamu. Mwenyezi Mungu amefichua siri zote za mpango wa usimamizi wa Mungu, na Amedhihirisha tabia ya Mungu yenye haki na takatifu, chote ambacho Mungu alicho na Anacho, mapenzi ya Mungu, na matakwa Yake kwa wanadamu. Pia, Amehukumu na kufichua asili ya kishetani ya mwanadamu na tabia potovu zinazompinga Mungu, na kwa kufanya hivyo, Alimshinda, Akamkamilisha, Akamfichua na kumwondoa mwanadamu, kila mmoja kwa aina yake mwenyewe. Ukweli wote ambao Mungu anamjalia mwanadamu katika siku za mwisho unaonyeshwa katika ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake, hakuna chochote cha ajabu kuhusu hili. Tunachoona tu ni mwanadamu wa kawaida Akinena neno Lake na kufanya kazi Yake, lakini neno ambalo Kristo ananena lote ni kweli. Lina mamlaka na nguvu, linaweza kutakasa na kumwokoa mwanadamu. Kutoka kwa neno la Kristo, ambalo linahukumu na kufichua ukweli na kiini cha upotovu wa mwanadamu, tunaona jinsi Mungu anapenya kwa kiini cha ndani cha mwanadamu katika kumchunguza, jinsi Mungu anamfahamu mwanadamu kabisa. Mwanadamu pia anakuja kujua tabia ya Mungu yenye haki, takatifu, na isiyokosewa. Kutokana na onyo na kusihi kwa Kristo, tunaona huruma na kujali kwa Mungu kwa mwanadamu. Kutokana na namna nyingi ambazo Kristo ananena na kufanya kazi, tunakuja kukubali uweza na hekima ya Mungu, makusudi ya shauku ambayo Mungu anatumia kufanya kazi kuwaokoa wanadamu, na upendo wa kweli na wokovu wa mwanadamu. Kutokana na namna ambayo Kristo anawatendea watu wote, mambo yote, na vitu vyote, tunakuja kufahamu jinsi raha, hasira, huzuni, na furaha ya Mungu yote ni uhalisi wa mambo ya kujenga, na jinsi yote ni maonyesho ya tabia ya Mungu na madhihirisho ya kawaida ya kiini cha maisha ya Mungu. Kutokana na neno na kazi ya Kristo, tunaona jinsi Mungu ni mkuu na mwenye uwezo mkubwa na vile ni mnyenyekevu na Aliyejificha, tunapata ufahamu wa kweli na maarifa ya tabia ya asili ya Mungu na uso halisi, unaotufanya kuwa na kiu ya ukweli na uchaji kwa Mungu katika mioyo yetu, kumpenda na kumtii kweli Hii ni athari ya neno na kazi ya kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kwetu. Neno na kazi ya kupata mwili kwa Mungu wa pili havimruhusu tu mwanadamu kumwona Mungu akipata mwili lakini pia vinamruhusu kuona ukweli wa Neno la Mungu kuonekana katika mwili. Neno la Mungu linatimiza mambo yote. Mwili huu wa kawaida, wastani ni mfano halisi wa Roho wa ukweli. Mungu mwenye mwili, ni ukweli, njia, na uzima! Yeye ni kuonekana kwa Mungu mmoja halisi wa pekee! Ni kwa kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu tu ndipo umuhimu wa kupata mwili umekamilishwa.

Hebu tusome vifungu vingine viwili vya neno la Mwenyezi Mungu, Ili ufahamu wetu wa ukweli huu na siri uweze kuwa dhahiri hata zaidi. Mwenyezi Mungu asema, “Hatua hii ya kazi hasa inatimiza maana ya ndani ya ‘Neno lakuwa mwili,’ ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya ‘naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,’ na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno ‘Hapo mwanzo kulikuwako na Neno’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)). “Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, ‘Neno kuonekana katika mwili’; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. ‘Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.’ Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu).

Naamini kwamba kila mtu ana ufahamu zaidi kidogo wa jinsi kupata mwili kuwili kwa Mungu kunakamilisha umuhimu wa kupata mwili! Sasa tunajua ukweli kwamba kazi ya Mungu kuwaokoa wanadamu inakamilishwa kupitia kwa kazi ya kupata mwili. Hatua ya kazi ambayo Bwana Yesu alitekeleza ilikuwa kazi ya ukombozi. Ukweli Alioonyesha ulikuwa mchache. kwa hiyo, baada ya kuipitia kazi ya Bwana Yesu, ufahamu wetu wa Mungu bado ulikuwa mchache. Mwenyezi Mungu amekuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na alionyesha ukamilifu wa ukweli wa hukumu yenye haki ya Mungu ya upotovu wa mwanadamu. Hili linamruhusu mwanadamu kuona tabia ya asili ya Mungu na kujua kiini Chake cha haki na takatifu. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho amekamilisha kabisa kazi ya Mungu katika mwili. Ameonyesha ukamilifu wa ukweli ambao Mungu anatakiwa kuonyesha katika mwili, hivyo kutimiza ukweli wa Neno kuonekana katika mwili. Hivi ndivyo jinsi kupata mwili kwa Mungu kuwili kunakamilisha maana ya kupata mwili. Kupata mwili kwa Mungu mara mbili hawawezi kuepukika, na wanajalizana na kukamilishana. Kwa hiyo mtu hawezi kusema kwamba Mungu anaweza tu kupata mwili mara moja, au kwamba Atapata mwili mara tatu au mara nne. Kwa kuwa kupata mwili kwa Mungu mara mbili wameshakamilisha kazi ya Mungu kumwokoa wanadamu, na Wameonyesha ukamilifu wa ukweli wa kuwaokoa wanadamu ambao kupata mwili kwa Mungu kunatakiwa kuonyesha. Hivyo, kupata mwili kwa Mungu mara mbili wamekamilisha maana ya kupata mwili.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp