Mungu alimtumia Musa kufanya kazi ya Enzi ya Sheria, hivyo kwa nini Mungu hawatumii watu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini badala yake Analazimika kupata mwili ili kuifanya Mwenyewe? Kuna tofauti gani muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na watu ambao Mungu huwatumia?

07/06/2019

Jibu:

Ni kwa nini lazima Mungu apate mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho? ni swali ambalo wengi walio na kiu ya ukweli na wanatafuta kuonekana kwa Mungu wanalijali sana. Pia ni swali linalohusiana na kama tunaweza kunyakuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuelewa kipengele hiki cha ukweli. Ni kwa nini lazima Mungu ajipatie mwili ili kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho badala ya kumtumia mwanadamu kuifanya kazi Yake? Hili linaamuliwa na hali ya kazi ya hukumu. Kwa sababu kazi ya hukumu ni onyesho la Mungu la ukweli na onyesho la tabia Yake yenye haki ili kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu. Hebu tusome vifungu vichache kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu.

Sababu ya Mungu kuhitajika bado kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, ingawa Bwana Yesu aliwakomboa wanadamu

Mwenyezi Mungu asema, “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona kwamba Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inajumuisha kuonyesha vipengele vingi vya ukweli, kuonyesha tabia ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, kufichua siri zote, kuhukumu asili ya kishetani ya mwanadamu ya kumpinga Mungu na kumsaliti Mungu, kufichua na kuchangua maneno na mwenendo wa mwanadamu, na kufichua kiini kitakatifu na chenye haki cha Mungu na tabia isiyokosewa kwa wanadamu wote. Wakati wateule wa Mungu wanapitia hukumu kwa maneno ya Mungu, ni kana kwamba wako uso kwa uso na Mungu, wakifichuliwa na kuhukumiwa naye. Wakati Mungu anamhukumu mwanadamu, lazima amruhusu kuona dhihirisho la tabia Yake yenye haki, kana kwamba kuona kiini kitakatifu cha Mungu, kana kwamba kuona nuru kuu inayorushwa kutoka mbinguni, na kuona neno la Mungu ni kama upanga mkali ukatao kuwili unaoingia ndani ya moyo na roho ya mtu, ukimsababisha kuvumilia maumivu yasiyoelezeka. Ni kwa njia hii tu ndio mwanadamu anaweza kupata kutambua kiini chake potovu na ukweli wa upotovu wake, ahisi fedheha nzito, aone aibu, na asujudu mbele za Mungu kwa toba ya kweli, na kisha ataweza kukubali ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu, aachane kabisa na ushawishi wa Shetani, na aokolewe na kukamilishwa na Mungu. Kazi kama hii ya hukumu, utakaso, na wokovu wa mwanadamu inaweza tu kufanywa na Mungu mwenye Mwenyewe.

Baada ya kupitia hukumu kwa neno la Mwenyezi Mungu, sote tumehisi jinsi utakatifu na tabia yenye haki ya Mungu ni visivyokosewa na wanadamu. Kila herufi ya neno la Mungu ina uadhama na ghadhabu, kila neno hugonga hadi kiini cha mioyo yetu, likifichua kabisa asili yetu ya kishetani ya kumpinga Mungu na kumsaliti Mungu, pamoja na vitu vya tabia ya upotovu vilivyozikwa ndani kabisa mwa mioyo yetu ambavyo hata sisi wenyewe hatuwezi kuviona, likituruhusu kutambua vile asili yetu na kina chetu vimejaa kiburi, kujidai, ubinafsi, na udanganyifu, jinsi tunavyoishi kulingana na vitu hivi, kama pepo walio hai wakizurura duniani, wasiokuwa na hata kiasi kidogo cha ubinadamu. Mungu analiona hili kuwa la kuchukiza sana na la karaha. Tunahisi kufedheheshwa na kunyanyaswa na majuto. Tunaona ubaya na uovu wetu wenyewe na tunajua hatustahili kuishi mbele za Mungu, kwa hiyo tunasujudu sakafuni, tukiwa radhi kupokea wokovu wa Mungu. Katika kupitia hukumu kwa neno la Mwenyezi Mungu, tunashuhudia kweli kuonekana kwa Mungu. Tunaona kwamba utakatifu wa Mungu hauwezi kuchafuliwa na haki Yake ni isiyokosewa. Tunatambua makusudi yenye ari na upendo halisi ambao Mungu anajitahidi nao kumwokoa mwanadamu na tunaona ukweli na kiini cha upotovu wetu mikononi mwa Shetani. Hivyo, ndani ya mioyo yetu, tunaanza kuhisi kumcha Mungu na tunakubali kwa furaha ukweli na kutii mpango wa Mungu kwa ajili yetu. Kwa namna hii, tabia yetu potovu inatakaswa polepole. Mabadiliko tuliyofikia leo ni matokeo ya kupata mwili kwa Mungu kufanya kazi ya hukumu. Kwa hiyo mwaona, ni wakati ambao kupata mwili kwa Mungu anaonyesha ukweli tu, Anaonyesha tabia yenye haki ya Mungu na chote ambacho Anacho na Alicho kutekeleza kazi ya hukumu, wakati huo tu ndipo mwanadamu anaona kuonekana kwa nuru ya kweli, kuonekana kwa Mungu, na anaanza kuwa na ufahamu wa kweli kuhusu Mungu. Ni namna hii pekee ndipo tunaweza kuona kwamba ni Mungu tu anaweza kututakasa na kutuokoa. Isipokuwa Kristo, hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Hebu tusome kifungu kingine cha neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu asema, “Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. … Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa).

Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu tunaona waziwazi kwamba kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho lazima ifanywe kwa njia ya kuonyesha ukweli, tabia ya Mungu, na uweza na hekima ya Mungu kumshinda, kumtakasa, na kumkamilisha mwanadamu. Mungu anaonekana Mwenyewe kuifanya kazi hii ya hukumu katika siku za mwisho. Kazi hii inaashiria mwanzo wa enzi moja na mwisho wa enzi nyingine. Kazi hii lazima ifanywe na kupata mwili kwa Mungu, hakuna mwanadamu anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Ni kwa nini watu wengi wanaamini kwamba Mungu anapaswa kuwatumia wanadamu kuifanya kazi Yake yote, badala ya kupata mwili ili kuifanya kazi hiyo Mwenyewe? Hili haliaminiki! Je, wanadamu wanakaribisha ujio wa Mungu kweli? Kwa nini kila mara kuna watu wengi sana wanaotumaini kwamba Mungu atawatumia wanadamu kuifanya kazi Yake? Hili ni kwa sababu wanadamu hufanya kazi kwa mujibu wa dhana zao, wao hufanya mambo tu jinsi watu wanavyofikiri yanapaswa kufanywa, kwa hiyo wanadamu huwaabudu wanadamu wengine kwa urahisi, huwakweza na kuwafuata, Lakini njia ya Mungu ya kufanya kazi huwa haipatani kamwe na dhana za mwanadamu, Hafanyi mambo jinsi mwanadamu anavyofikiri yanapaswa kufanywa. Kwa hivyo mwanadamu huona ugumu kulingana na Mungu. Kiini cha Mungu ni ukweli, njia, na uzima. Tabia ya Mungu ni takatifu, yenye haki na isiyokosewa. Mwanadamu mpotovu, hata hivyo, amepotoshwa kabisa na Shetani, na amejaa tabia ya kishetani, na yeye huona ugumu kulingana na Mungu. Kwa hiyo, mwanadamu huona ugumu kukubali kazi ya kupata mwili kwa Mungu na hataki kusoma na kuchunguza, badala yake anamwabudu mwanadamu na kuweka imani isiyoweza kutambua katika kazi yake, akiikubali na kuifuata kana kwamba ni kazi ya Mungu. Tatizo ni lipi hapa? Ungesema, wanadamu hawana habari hata kidogo kuhusu nini maana ya kumwamini Mungu na kupitia kazi Yake, kwa hiyo, kazi ya Mungu katika siku za mwisho lazima iwe na maonyesho ya ukweli na kupata mwili ili kutatua matatizo yote ya wanadamu wapotovu. Kuhusu swali lenu la kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kuifanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, bado linahitaji jibu? Kiini cha mwanadamu ni mwanadamu, mwanadamu hamiliki kiini cha uungu, kwa hiyo mwanadamu hawezi kuonyesha ukweli, kuonyesha tabia ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na hawezi kuifanya kazi ya kuwaokoa wanadamu. Licha ya kuwa, wanadamu wote wamepotoshwa na Shetani na wana asili ya dhambi, hivyo wana sifa gani za kustahili kuwahukumu wanadamu wengine? Kwa kuwa mwanadamu mchafu na mpotovu hana uwezo wa kujitakasa na kujiokoa, anatarajia vipi kuwatakasa na kuwaokoa wengine? Wanadamu kama hao wangekabiliana na fedheha tu wakati watu wengine wangekataa kukubali hukumu yao. Mungu pekee ndiye mwenye haki na mtakatifu, na Mungu pekee ndiye ukweli, njia, na uzima. Kwa hiyo, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho lazima itekelezwe na kupata mwili Kwake. Hakuna mtu anayeweza kuifanya kazi kama hii, huu ni ukweli.

Sasa kwa nini Mungu alimtumia mwanadamu kuifanya kazi Yake katika Enzi ya Sheria? Hii ni kwa sababu kazi ya Enzi ya Sheria na ile ya hukumu ya siku za mwisho zina hali tofauti. Katika Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa upya, walikuwa wamepotoshwa na Shetani kwa kiwango kidogo tu. Kazi ya Yehova Mungu ilijumuisha hasa kutangaza rasmi sheria na amri kutoa mwongozo kwa mwanadamu wa mwanzo kuhusu namna ya kuishi duniani. Hatua hii ya kazi haikulenga kuibadilisha tabia ya mwanadamu, haikuhitaji kuonyesha ukweli mwingi zaidi. Mungu alihitaji tu kumtumia mwanadamu kuwasilisha kwa Waisraeli sheria Alizokuwa Ameunda, ili Waisraeli wangejua namna ya kuzitii sheria, kumwabudu Yehova, na kuishi maisha ya kawaida duniani. Baada ya kufanya hivyo, hatua hiyo ya kazi ilikamilishwa hivyo. Kwa hiyo, Mungu angemtumia Musa kuikamilisha kazi ya Enzi ya Sheria, Hakuhitaji kupata mwili ili kuitekeleza kazi hiyo Mwenyewe. Kinyume chake, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inalenga kuwaokoa wanadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani kwa hali kubwa. Kutoa vifungu vichache vya neno la Mungu na kutangaza rasmi sheria chache hakutatosha kamwe katika hali hii. Kiasi kikubwa cha ukweli lazima kionyeshwe. Tabia ya Mungu ya asili, chote ambacho Mungu anacho na Alicho lazima vionyeshwe kabisa, ukweli, njia, na uzima lazima vifunguliwe kwa ajili ya wanadamu wote, kana kwamba Mungu angejifichua Mwenyewe uso kwa uso na wanadamu, Akimruhusu mwanadamu kuelewa ukweli na kumjua Mungu, na kwa kufanya hivyo, Anawatakasa, Anawaokoa na kuwakamilisha wanadamu kabisa. Mungu lazima afanye hili Mwenyewe binafsi kwa njia ya kupata mwili, hakuna mwanadamu anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Mungu anaweza kuwatumia manabii kutoa vifungu vichache vya neno Lake, lakini Mungu hawaruhusu manabii kuonyesha tabia ya Mungu ya asili, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, au kuonyesha ukweli wote, kwa sababu mwanadamu hastahili kufanya hivyo. Kama Mungu angemtumia mwanadamu kuonyesha tabia na ukweli Wake wote, kuna uwezekano wa kumwaibisha Mungu, kwa sababu mwanadamu ana tabia potovu, ana uwezekano wa kuzisaliti dhana na njozi zake mwenyewe, lazima kuwe na uchafu katika kazi yake, ambalo lingemfedhehesha Mungu na kuathiri matokeo ya jumla ya kazi ya Mungu. Pia, mwanadamu anafaa kuchukua chote ambacho anacho na alicho kwa ajili ya chote ambacho Mungu anacho na Alicho, akichukua uchafu wa mwanadamu katika kazi yake ya ukweli. Hili husababisha kumwelewa Mungu visivyo na kumfedhehesha. Pia, kama Mungu angemtumia mwanadamu kuonyesha tabia na ukweli Wake wote, watu hawangetaka kukubali na hata wangepinga, kwa sababu ya uchafu wa mwanadamu. Kisha Shetani angewalaumu na kuwatafutia makosa. akichochea mwanadamu kutoridhika na Mungu, akichochea uasi, na kuwachochea waanzishe ufalme wao wenyewe ulio huru. Hili ni tokeo la mwanadamu kuifanya kazi ya Mungu. Hasa, katika hali ya Mungu kumwokoa mwanadamu aliyepotoshwa kabisa katika siku za mwisho, wanadamu hawakubali na kutii kwa urahisi kazi ya kupata mwili kwa Mungu. Kwa hiyo kama Mungu angewatumia wanadamu kuifanya kazi hii, wanadamu huenda hawangekubali zaidi na kutii kiasi hicho. Je, huu si ukweli mtupu? Watazame wazee wa kanisa na wachungaji wa ulimwengu wa kidini, je, upinzani na shutuma yao ya kazi ya kupata mwili kwa Mungu ni tofauti kwa hali yoyote na vile makuhani wakuu na Mafarisayo wa Kiyahudi walimpinga Bwana Yesu awali? Mungu kuwaokoa wanadamu wapotovu si kazi rahisi. Lazima tuelewe vile Mungu anafikiria!

Kazi ya Mungu mwenye mwili ya hukumu katika siku za mwisho ni kuwahukumu, kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, upande mwingine, na muhimu zaidi, Mungu anaifanya kazi Yake kwa njia ya maonyesho ya ukweli na maonyesho ya tabia ya Mungu na chote ambacho Anacho na Alicho kuwaruhusu wanadamu wote kumjua na kumwelewa Mungu kweli, na kuona kuonekana kwa Mungu katika mwili. Hebu tusome vifungu vingine vya neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu asema, “Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni kwa kubadilisha vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza na Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu, na kuwafanya watu kuvielewa ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. … Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe).

Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili kwa niaba ya Roho wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kwa njia ya kupata mwili ni ya maana kweli. Mungu amepata mwili duniani katika siku za mwisho, Akiishi miongoni mwa wanadamu na kulitangaza neno Lake kwa wanadamu, Akionyesha tabia ya Mungu Mwenyewe na chote ambacho Mungu anacho na Alicho kwa umati. Yule ambaye Mungu anampenda na yule ambaye Mungu anamchukia, yule ambaye ghadhabu ya Mungu inaelekezwa, yule Anayemwadhibu, hali Yake ya hisia, matakwa Yake kwa wanadamu, kusudi Lake kwa wanadamu, mtazamo wa njozi wa mwanadamu kuhusu maisha, maadili, n.k., Anawaarifu wanadamu kuhusu mambo haya yote, Akimruhusu mwanadamu kuwa na malengo wazi katika maisha ili wasihitaji kutafutatafuta bila malengo katika ufuatiliaji wa dini usio dhahiri. Kuonekana kwa kupata mwili kwa Mungu “anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri.” Wale wote ambao wamepitia neno na kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho wana utambuzi wa pamoja: Hata ingawa tumepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tumevumilia kila aina ya majaribio na usafishaji, na tumeteswa sana na ukimbizaji wa kinyama, katili na mateso ya serikali ya Kikomunisti ya Uchina, tumeiona tabia yenye haki ya Mungu ikija kwetu, tumeona uadhama na ghadhabu ya Mungu na uweza na hekima Yake, tumeona dhihirisho la chote ambacho Mungu anacho na Alicho, kama vile tu tungemwona Mungu Mwenyewe. Ingawa hatujauona mwili wa kiroho wa Mungu, tabia ya asili ya Mungu, uweza na hekima Yake, na chote ambacho Anacho na Alicho, vimefichuliwa kwetu kwa ukamilifu, kana kwamba Mungu alikuwa Amekuja mbele yetu, uso kwa uso, Akituruhusu tumjue Mungu kweli na tuwe na moyo unaomcha Mungu ili tuweze kutii mpango wowote ambao Mungu anao kutuhusu hadi kifo. Sote tunahisi kwamba katika neno na kazi ya Mungu tunamwona na kumjua Mungu kwa njia halisi na kweli, na tumeacha kabisa dhana na njozi zote na tumekuwa wale wanaomjua Mungu kweli. Awali, tulifikiria tabia ya Mungu ni yenye upendo na huruma, kumwamini Mungu kungesamehe dhambi za mwanadamu siku zote. Lakini baada ya kupitia hukumu ya neno la Mwenyezi Mungu, tumekuja kuelewa kweli kwamba tabia ya Mungu si yenye huruma na ya upendo tu, pia ni, yenye haki, adhimu, na yenye ghadhabu. Yeyote anayeikosea tabia Yake ataadhibiwa. Hivyo, tunaweza kumcha Mungu, kuukubali ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kwa kupitia kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, sote tumekuja kuelewa kweli na kwa uhalisi kwamba tabia ya Mungu ni takatifu, yenye haki, na isiyokosewa, tumepitia huruma na upendo wa Mungu, tumekuja kukubali kweli uweza na hekima ya Mungu, tumetambua jinsi Mungu amejishusha katika siri, tumekuja kujua makusudi Yake yenye ari, sifa nyingi za kupendeza, hali Yake ya hisia, uaminifu Wake, uzuri na wema Wake, mamlaka Yake, ukuu, na uchunguzi Wake makini wa kila kitu, n.k. chote ambacho Mungu anacho na Alicho kimeonekana mbele yetu, kana kwamba tunamwona Mungu Mwenyewe, kikituruhusu kumjua Mungu uso kwa uso. Hatumwamini na kumfuata Mungu tena kwa kutegemea dhana na njozi zetu, bali tunahisi uchaji na ibada ya kweli kwa Mungu, na kumwabudu na kumtegemea Mungu kweli. Tumetambua kwa kweli kwamba kama Mungu hangekuwa Amepata mwili mwenyewe kuonyesha ukweli na kumhukumu mwanadamu, hatungemjua Mungu kamwe, na hatungeweza kujiondolea dhambi na kufikia utakaso. Kwa hiyo haijalishi unavyoiona, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho lazima ifanywe na Mungu mwenye mwili Mwenyewe, hakuna anayeweza kuchukua nafasi Yake. Kwa ajili ya dhana na njozi za mwanadamu, kama Mungu angemtumia mwanadamu kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, Hangeweza kutimiza matokeo yanayotakikana.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Hivyo, hebu tupige hatua zaidi na kushiriki kuhusu tofauti za msingi kati ya Mungu mwenye mwili na wanadamu ambao Mungu huwatumia Hebu tuangalie kile ambacho Mwenyezi Mungu anasema kuhusu kipengele hiki cha ukweli. Mwenyezi Mungu asema,

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni).

Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa hawana chochote ila ubinadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).

Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni).

Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na safi, na halisi na wa kweli, mwili Wake unatoka kwa Roho. Hili ni wazi, na bila shaka. Sio tu kuweza kushuhudia kwa Mungu Mwenyewe, bali pia kuweza kufanya kabisa mapenzi ya Mungu: huu ni upande mmoja wa dutu ya Mungu. Kwamba mwili unatoka kwa Roho na sura kuna maana kwamba mwili ambao Roho anajivisha ni tofauti kimsingi na mwili wa mwanadamu, na tofauti hii hasa iko ndani ya roho zao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 9).

Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. …

… Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Mwenyezi Mungu ameweka wazi kabisa kwamba Mungu mwenye mwili ni Roho wa Mungu aliyepatikana katika mwili. Japokuwa ana ubinadamu wa kawaida, ana kiini cha kiungu. Wanadamu ambao Mungu huwatumia, hata hivyo, wana kiini cha kibinadamu. Wanaweza tu kuwa wanadamu, na hawana kiini cha kiungu hata kidogo. “Kristo ana kiini cha kiungu” maana yake ni kuwa kile ambacho Roho wa Mungu anacho, tabia Yake ya asili, kiini Chake cha haki na utakatifu, kile ambacho Mungu anacho na alicho, uweza na hekima, na mamlaka na nguvu za Mungu, vyote vimepatikana ndani ya mwili. Mwili huu ni mwili wenye kiini cha kiungu, Mungu halisi ambaye amekuja duniani kutenda kazi na kuokoa wanadamu. Kwa sababu Kristo ana kiini cha kiungu, hali Yake ya kihisia, mikao, mitazamo na maoni kuelekea watu mbalimbali, matukio na vitu, mawazo yote ya Kristo ni ukweli, vyote ni maonyesho ya kiini na tabia ya uzima mtakatifu ya Mungu. Kristo anaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu, anaweza kuonyesha moja kwa moja sauti ya Mungu, tabia Yake, na kile ambacho Mungu anacho na alicho kupitia utambulisho wa Mungu. Anaweza kumpa mwanadamu ukweli, njia, na uzima, na hii ni mbali sana na uwezo wa mwanadamu yeyote aliyeumbwa. Ni kwa sababu Kristo anao uungu kamili, na hivyo anaweza kuonyesha neno la Mungu moja kwa moja, wakati na mahali popote, tofauti na manabii ambao huwasilisha tu maneno machache ya Mungu kwa wakati maalum. Yote ambayo Kristo anaonyesha ni ukweli, na hiyo ndiyo kazi ya Mungu katika enzi mpya. Hazungumzi kuhusu maarifa na uzoefu wake kuhusu maneno ya Mungu. Kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Yeye anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote ili kutoa, kunywesha na kuchunga watu, kuongoza wanadamu wote. Na kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Yeye anaweza kuchukua kazi ya Mungu. Anaweza kuongoza na kukomboa wanadamu, kushinda na kuokoa wanadamu, kuhitimisha enzi ya zamani yote. Lakini wanadamu ambao Mungu anawatumia wana kiini cha kibinadamu. Hawana uungu, lakini ni wanadamu tu. Na hivyo, wanaweza tu kufanya kazi ya mwanadamu na kutimiza wajibu wa kibinadamu. Japokuwa wana elimu, mwangaza, kazi na ukamilifu wa Roho Mtakatifu, sanasana wanaweza tu kushirikiana na kazi ya Mungu na kuonyesha maarifa na uzoefu wao. Maneno yao yanaweza kukubaliana na ukweli na kuwanufaisha wengine mara nyingi, lakini si ukweli, na hayana usawa na maneno ya Mungu. Lazima tuelewe kwamba Mungu mwenye mwili anatenda kazi ya kuanzisha enzi na kuhitimisha enzi. Anaweza kuonyesha moja kwa moja ukweli na kuwaongoza wanadamu wote. Lakini wanadamu ambao Mungu huwatumia au wanadamu ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu sanasana wanashirikiana na kazi ya Mungu wakati wakitimiza wajibu wa mwanadamu. Sasa, wanaonyesha tu maarifa na uzoefu wao wa neno la Mungu, na kile wanachosema kinakubaliana na ukweli. Bila kujali wametenda kazi kwa muda mrefu kiasi gani kwa ajili ya Mungu na bila kujali wameongea kiasi gani, wao wanashiriki tu maarifa na uzoefu wao wa neno la Mungu, wanamwinua tu Mungu na kubeba ushuhuda wa Mungu. Hii ndiyo tofauti ya muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na wanadamu ambao Mungu hutumia au wanadamu wenye kazi ya Roho Mtakatifu.

Mungu mwenye mwili ni wa kiini cha kiungu, na kazi na neno Lake havijanajisiwa na mawazo, fikira, ubunifu, na mantiki za kibinadamu, bali, Mungu mwenye mwili anaonyesha moja kwa moja vyote ambavyo uungu unavyo na ulivyo, na maana ya asili ya Roho wa Mungu. Kama tu kwenye Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifichua mafumbo ya ufalme wa mbinguni, alileta njia ya toba, na alionyesha tabia Yake ya upendo na rehema, na kadhalika. Yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho wa Mungu, yote ni mafunuo ya asili ya tabia ya Mungu na vyote alivyonavyo na alicho. Yote hayawezi kufikiwa na fikira za mwanadamu. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote ambao utatakasa na kukamilisha wanadamu. Anafichua tabia ya haki ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote, na anaweka wazi mafumbo yote ya mpango Wake wa usimamizi, kama vile mafumbo ya kupata mwili kwa Mungu, tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu, ukweli wa ndani wa hatua tatu za kazi ya Mungu, asili ya upotovu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyoweza kujitoa kwenye dhambi na kufikia wokovu wa Mungu, hatima ya baadaye ya wanadamu, na kadhalika. Kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakifanya ni maonyesho ya moja kwa moja ya uungu, ni maana ya asili ya Roho wa Mungu, ambayo haifikiwi na fikira za mwanadamu. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili na tabia Yake iliyoonyeshwa vinatosha kuthibitisha kwamba Mungu mwenye mwili ni uungu katika kiini, na kwamba Yeye si mwingine ila ni Mungu Mwenyewe, Mmoja na wa pekee. Wanadamu ambao Mungu huwatumia, hata hivyo, hawawezi kuchukua nafasi ya Mungu katika kutenda kazi ya kiungu, wala kuonyesha moja kwa moja mapenzi ya asili ya Roho wa Mungu. Wanaweza tu kutenda kazi ya ushirikiano wa kibinadamu juu ya msingi wa kazi ya Mungu, kushiriki maarifa na uzoefu wao, kuongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika uhalisi wa ukweli wa maneno ya Mungu, kubeba ushuhuda kwa ajili ya Mungu na kumtumikia Yeye. Huku ndiko kutimiza wajibu wa mwanadamu. Wanatenda kazi ambayo akili ya kibinadamu inaiweza, kazi ambayo mwanadamu anaipitia, kazi ambayo kimsingi mwanadamu anacho na alicho. Kwa kuwa Mungu mwenye mwili na wanadamu ambao huwatumia wanatofautiana katika kiini, kazi yao ni tofauti kabisa katika kiini, Mungu mwenye mwili anatofautiana na wanadamu ambao Yeye huwatumia, kama tu ambavyo Mungu anatofautiana na mwanadamu. Mmoja ana kiini cha Mungu, ilhali mwingine ana kiini cha binadamu. Yule mwenye kiini cha kiungu anaweza kutenda kazi ya Mungu, ilhali wale wenye kiini cha kibinadamu wanaweza tu kutenda kazi ya mwanadamu. Kila mmoja anayemwamini Mungu ni lazima aelewe hili.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake.” Neno la Mungu ni wazi sana. Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu mwenyewe—ni kazi ambayo Mungu lazima atekeleze miongoni mwa wanadamu, ni kazi ambayo Mungu lazima atekeleze yeye binafsi, na ni kazi ambayo hakuna mwanadamu anayeweza kufanya badala Yake. Hakuna mwanadamu anayeweza kuifanya badala Yake; hili linamaanisha kwamba hakuna binadamu anayeweza kuchukua nafasi ya Mungu katika kufanya kazi hii. Kwa nini hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi Yake? Wengine wanaweza kusema: “Wakati wa Enzi ya Sheria, je, Mungu hakumtumia Musa kutekeleza kazi Yake? Basi mbona Mungu hawezi kuwatumia wanadamu kutekeleza kazi ya hukumu?” Je, kuna siri iliyo ndani ya hili? Katika Enzi ya Sheria Mungu alitoa sheria na amri kwa Waisraeli, ambalo lingeweza kufanywa kumtumia mwanadamu. Lakini kwa nini mwanadamu hawezi kuchukua nafasi ya Mungu na kutekeleza kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Kuna siri hapa. Siri hii inahusu nini? Hebu tuendelee kusoma kuona kile ambacho Mungu anacho cha kusema kuihusu. “Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu.” Mungu amejulisha ufafanuzi wa kazi ya hukumu—asili ya kazi hii ni ipi? Mungu asema, “Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli.” Tunapaswa kueleza vipi maneno haya? Hukumu ni nini hasa? Kwa msingi wa neno la Mungu tunaweza kuielewa kama ifuatavyo: Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu kwa kutumia ukweli kumshinda mwanadamu. “Kumshinda mwanadamu kupitia ukweli,” lazima tuyafikirie maneno haya kwa makini. Kwa nini mwanadamu hawezi kufanya kazi hii ya hukumu? Watu wengine wanasema ni kwa sababu mwanadamu hana ukweli, kwa hiyo hawezi kuonyesha ukweli. Aina hii ya ufahamu, aina hii ya ridhaa ni sawa kabisa. Kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hawajajiandaa na ukweli, hawawezi kutekeleza kazi ya hukumu. Watu wengine wanasema: “Mungu anaweza kuwatumia manabii kuonyesha neno Lake, kwa hiyo Mungu angeweza kuwatumia manabii kuonyesha neno Lake ili kutekeleza kazi ya hukumu?” La. Hii ni kwa sababu manabii kuwasilisha neno la Mungu na Mungu Mwenyewe kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote kutaleta matokeo tofauti, kwa sababu manabii si ukweli wao wenyewe. Kutakuwa na matokeo gani kutokana na kumruhusu mtu fulani ambaye si ukweli kuwasilisha neno la Mungu? Kristo, anapokuwa akitekeleza kazi ya hukumu katika utambulisho Wake kama Mungu, anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote, kufichua kile Mungu anacho na alicho, na kujulisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, nabii, si ukweli yeye mwenyewe na hawezi kufichua kile Mungu anacho na alicho wakati wowote na mahali popote. Tofauti kati ya matokeo yanayotolewa kwa kutumia nabii kuwasilisha neno la Mungu na kwa Mungu kuonyesha ukweli moja kwa moja ni ipi kwa kweli? Ikiwa hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa kikamilifu, basi utakuwa na ufahamu wa kweli wa maneno, “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake.” “Haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake.” ni nini kinachojumuishwa ndani ya haya? Haitafaa Mungu akitumia wanadamu au manabii kuwasilisha maneno Yake. Mbona hivyo? Mbona hilo halitaweza kufanikisha matokeo sawa na Mungu kutekeleza kazi Mwenyewe? Mara unapoweza kubaini hili suala utaweza kukubali maneno haya.

Mbona isiwe sawa kwa Mungu kuwatumia manabii kuwasilisha neno Lake la Mungu kutekeleza kazi ya hukumu? Ni matokeo gani ambayo hayangeweza kufanikishwa ikiwa kazi hii ingefanywa kwa njia hiyo? Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuona? Ikiwa manabii wangetumiwa kuwasilisha maneno ya Mungu, matokeo yangewaruhusu watu kuwa na ufahamu mdogo wa maneno ya Mungu pekee. Lakini kuhusu kuelewa tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, na ukweli ambao Anaonyesha, bila kujali jinsi mwanadamu fulani alivyotumia juhudi kubwa, haiwezekani kufanikisha matokeo bora kabisa. Kwa nini hawezi kufanikisha matokeo bora kabisa? Asili ya manabii ni ile ya ubinadamu. Kwa kuwa kiasili wao ni wanadamu, je, maonyesho yao wenyewe yanaweza kuwa kile uungu unacho na ulicho? Hawawezi kufanya hivyo kabisa. … Kwa msingi wa hoja hii, tunaweza kuona kwamba bila kujali jinsi nabii huenda akawasilisha neno la Mungu, hataweza kufichua tabia Yake, wala hataweza kufichua kile Mungu anacho na alicho, kwani manabii ni wanadamu kwa asili—wao hawana uungu. Kristo ana asili ya Mungu, na katika kutekeleza kazi ya hukumu Anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote; Anaweza kufichua kile Mungu anacho na alicho. Katika Kristo, mwanadamu anaweza kuona tabia ya Mungu, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kuona uweza na hekima ya Mungu. Kuhusu mwanadamu anayetumiwa na Mungu, bila kujali kiasi cha neno la Mungu tunachopata kuelewa kupitia yeye, hatimaye kupitia kwake bado hatutawahi kuweza kufanikisha ufahamu wa Mungu, na hata tukipata kiasi, utakuwa mdogo sana, sana! Unapaswa kuwa na uwazi wa hili sasa, siyo? Kwa hiyo sasa tunapaswa kuelewa vyema maana ya maneno ya Mungu, “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake.” Hata hivyo, watu katika dunia ya dini hawawezi kutambua maana ya maneno haya—hawayaelewi. Wanaamini kwamba kwa kuwa Mungu aliweza kumtumia Musa kutekeleza kazi Yake katika Enzi ya Sheria, basi Mungu anapaswa kuweza kumtumia mwanadamu kutekeleza kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Lakini, je, si hili ni tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu? Kupata ufahamu wa hoja hii ni neema ya Mungu. Watu katika jamii za dini hawawezi kuelewa hili, kwani hawajapitia kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Wanakosa kuelewa ukweli mwingi sana! Hawana ufahamu wa ukweli mwingi. Kwa kulinganishwa tumepata mengi zaidi, zaidi. Kila kitu katika kitabu Neno Laonekana Katika Mwili ni onyesho la ukweli. Kina ukweli ambao haujapatwa kupitia hatua za kazi ya Mungu ambazo wanadamu tayari wamepitia tangu kuumbwa kwa ulimwengu, ukweli ambao hadi sasa haujaeleweka. Lakini leo, kwa kuwa tunapitia kazi ya Mungu katika siku za mwisho, tumepata ukweli huu. Je, hii si neema ya Mungu? Je, huu si upendo mkubwa wa Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp