Jana usiku nilisoma maneno ya Mwenyezi Mungu, “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili.” Nadhani hiki ni kifungu cha ajabu cha neno la Mungu, halisi kabisa, na cha maana sana. Kuhusu ni kwa nini wanadamu wapotovu lazima wapokee wokovu wa kupata mwili kwa Mungu, hiki ni kipengele cha ukweli ambacho mwanadamu anatakiwa kufahamu kwa haraka. Tafadhali wasiliana nasi kuhusu jambo hili zaidi kiasi.

14/04/2020

Jibu:

“Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili,” kifungu hiki cha neno la Mungu kinaeleza kabisa maana ya wokovu wa wanadamu wapotovu na kupata mwili kwa Mungu. Hebu tusome kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu asema,

Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na amchunge mwanadamu binafsi. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi Yake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu).

Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko tabia potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi ambayo Amekusudia kufanya, na kupambana na Shetani. Lengo Lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na huku akimwokoa mwanadamu aliyepotoka. Hivyo, ni kazi ambayo inatimiza matatizo mawili kwa wakati mmoja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu tunatambua kwamba sababu ya wanadamu wapotovu lazima kuokolewa na kupata mwili kwa Mungu ni kwamba mwili wa mwanadamu umedanganywa na kupotoshwa kabisa na Shetani. Wanadamu wote wanamilikiwa na Shetani, hawawezi kubainisha kati ya mema na maovu, uzuri na ubaya. Hawawezi kutofautisha kati ya chanya na hasi. Wanaishi kulingana na falsafa, sheria na asili ya Shetani, ni wenye kiburi, wa kujidai wasiojali, na wahalifu. Wote ni mifano halisi ya Shetani na wamegeuka kuwa wapotovu wakiungana na Shetani kumpinga Mungu, lakini hawatambui kwamba. Mungu ni Muumba, Mungu pekee ndiye Anajua kabisa asili ya kweli ya wanadamu, wamepotoshwa kwa kiwango kipi. Na Mungu pekee ndiye Anaweza kufichua na kuchangua asili ya kishetani na tabia potovu ya mwanadamu, Anaweza kumwambia mwanadamu namna ya kuishi na kutenda kama wanadamu, na Anaweza kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu kabisa. Isipokuwa Mungu, hakuna mwanadamu aliyeumbwa anaweza kubaini kiini cha upotovu wa mwanadamu na bila shaka hawezi kumpa mwanadamu ukweli wa namna ya kutenda kama wanadamu. Kwa hiyo, ikiwa Mungu anataka kuwapokonya wanadamu wapotovu sana kutoka kwa fumbato za Shetani na kuwaokoa, basi ikiwa tu kupata mwili kwa Mungu ataonyesha mwenyewe ukweli na tabia ya Mungu na Amwambie mwanadamu kuhusu ukweli wote ambao anapaswa kumiliki, Akimruhusu mwanadamu kufahamu ukweli, kumjua Mungu, na abaini njama zenye uovu za Shetani na uwongo mbalimbali, wakati huo tu ndipo mwanadamu anaweza kumwacha na kumkataa Shetani na kurudi mbele za Mungu. Pia, kazi ya kupata mwili kwa Mungu hufichua kila aina za wanadamu. kwa sababu wanadamu wote ni wenye kiburi na hukataa kusalimu amri. Wakati Mungu anapata mwili kuonyesha ukweli, Wanadamu huitikia kila wakati kwa dhana zao, upinzani na hata vita. Kwa hivyo, ukweli wa upinzani na usaliti wa wanadamu wapotovu kwa Mungu hufichuliwa kwa ukamilifu na Mungu hutoa hukumu Yake kwa mwanadamu kutegemea upotovu wanaofichua na asili yao ya kweli. Ni kwa njia hii tu, ndio kushindwa, kutakaswa, na kukamilisha kwa wanadamu na Mungu kunaweza kutekelezwa kwa urahisi. Kupitia hukumu kwa maneno ya Mungu, mwanadamu anashindwa na anatakaswa polepole. Mwanadamu anaposhindwa kabisa, anaanza kutii Mungu mwenye mwili, anaanza kukubali na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu na anapitia kazi ya Mungu, anaamua kutafuata ukweli na kutoishi kamwe kwa kufuata falsafa na sheria za Shetani. Mwanadamu anapoishi kabisa kulingana na neno la Mungu, basi Mungu amemshinda Shetani kabisa na mwanadamu mpotovu anatumika kama mateka wa ushindi Wake dhidi ya Shetani. La msingi, Mungu anawapokonya wanadamu wapotovu kutoka kwa kukamata kwa Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili tu ndiyo inaweza kuwa na athari kama hiyo. Hii ndiyo haja kamili ya Mungu kupata mwili ili kuwaokoa wanadamu, na Mungu mwenye mwili tu ndiye Anaweza kuwashinda na kuwaokoa wanadamu kabisa. Watu wanaotumiwa na Mungu hawawezi kufanya kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu.

Mwanadamu mpotovu kweli anahitaji Mungu apate mwili kumhukumu na kumtakasa yeye mwenyewe ikiwa anataka kuokolewa. Katika harakati za uingiliano wa Mungu mwenye mwili na mwanadamu, Anamruhusu mwanadamu kumfahamu na kumjua Mungu uso kwa uso. Kwa sababu watafutaji halisi wa ukweli hukubali hukumu na utakaso wa Kristo wa siku za mwisho, kwa kawaida wanaweza kumtii Mungu na kuhisi upendo moyoni mwao kwa Mungu na waokolewe kabisa kutoka kwa milki ya Shetani. Je, hii si njia bora zaidi ya Mungu kuwaokoa na kuwakamilisha wanadamu? Kwa kuwa Mungu amepata mwili, tumekuwa na nafasi ya kumkaribia Mungu uso kwa uso na kupitia kazi Yake halisi, na tumekuwa na nafasi ya kupokea utoaji wa neno sahihi la Mungu na kuchungwa na kunyunyiziwa naye moja kwa moja ili tuanze kumtegemea Mungu, kumtii Mungu, na kumpenda kweli. Kama Mungu hangepata mwili kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu, athari hii halisi isingeweza kutimizwa. Mwenyezi Mungu asema, “Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ushawishi, na mapenzi Yake mahususi kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili). “Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili). “Mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mungu anapopata mwili ili kuwaokoa wanadamu wapotovu, Anaweza kutumia lugha ya wanadamu kuwaambia wanadamu waziwazi kuhusu matakwa ya Mungu, mapenzi Yake, tabia Yake na chote ambacho Anacho na Alicho. Kwa namna hii, bila kuhitaji kutafuta huku na huko, mwanadamu anaweza kufahamu mapenzi ya Mungu kwa dhahiri, ajue matakwa ya Mungu na njia ambayo anapaswa kutenda. Pia anaweza, kwa hivyo, kuwa na ufahamu na maarifa halisi kuhusu Mungu. Kama vile tu katika Enzi ya Neema, Petro alimwuliza Bwana Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba?” (Mathayo 18:21). Yesu akamwambia Petro moja kwa moja: “Sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba(Mathayo 18:22). Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu aliyepata mwili aliwalisha na kuwasaidia wanadamu wakati wowote na kokote Alikoenda, Akimpa mwanadamu ruzuku halisi na kamili. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amepata mwili miongoni mwa wanadamu, Akionyesha ukweli ili kushughulikia hali halisi ya mwanadamu, Akionyesha tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho ili kuwasaidia na kuwakimu wanadamu. Akieleza upungufu na uwongo wote ulio ndani ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, Akimwarifu mwanadamu kuhusu mapenzi ya Mungu na matakwa Yake, Akiwapa wanadamu ruzuku na riziki ya maisha halisi na sahihi zaidi. Kwa mfano, wakati tunaishi katika uasi na upinzani kwa Mungu bila kujua, Neno la Mungu linatufichua na kutuhukumu moja kwa moja, likituruhusu kuona, katika neno la Mungu, jinsi asili yetu ya kishetani inampinga Mungu. Tunapomfuata Mungu kwa manufaa yetu binafsi na tunajidai kwa kufanya hivyo, Mungu hufichua udhaifu wetu na hutwambia ni imani gani tunapaswa kushikilia kama wafuasi wa Mungu. Tunapomwelewa Mungu visivyo katika kupitia hukumu Yake, Neno la Mungu hutukumbusha kuhusu makusudi ya ari ambayo Mungu hutumia kuwaokoa na kuwahukumu wanadamu, Akitatua kutoelewa kwetu visivyo kuhusu Mungu, n.k. Wateule wote wa Mungu wamepitia kabisa vile Mungu mwenye mwili Anatusaidia na kuturuzuku sisi siku zote ili tusihitaji kutafuata huku na huko. Tunachohitaji kufanya tu ni kusoma neno la Mwenyezi Mungu zaidi ili kupata kulishwa na kunyunyiziwa halisi kwa Mungu. Kupitia kwa neno hilo Mungu anaonyesha, tunapata ufahamu wa kweli kiasi wa mapenzi ya Mungu, tabia Yake na chote ambacho Anacho na Alicho na kupitia kwa ufahamu huu, na kupitia kwa ufahamu huu, kwa namna ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli na kujifunza jinsi ya kubaini njama za woga za Shetani, tukiona waziwazi jinsi sisi wenyewe tumepotoshwa na Shetani kabisa, na kwa kufanya hivyo, tunaacha polepole dhambi zetu na ushawishi wa Shetani wa giza. Kutokana na hilo, tabia yetu ya maisha hubadilika na tunaishika njia sahihi, tukiishi kulingana na uhalisi wa ukweli. Kupata mwili kwa Mungu amewezesha haya yote.

Mungu amepata mwili kufanya kazi na kuonyesha neno Lake, Akimruhusu mwanadamu kupata ruzuku na riziki ya maisha iliyo halisi zaidi. Licha ya kuwa mwanadamu ana dhana nyingi kuhusu kazi ya hukumu ya Mungu mwenye mwili, Mungu amemletea mwanadamu njia ya uzima na wokovu wa milele. Na mwanadamu amekuja kumtegemea! Hebu tusome kifungu kingine kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu asema, “Hakuna namna ya kufikiri au kupima kazi Anayofanya katika mwili, maana mwili Wake si kama wa mwanadamu; ingawa sura za nje zinafanana kiini chao si sawa. Mwili Wake unatoa mitazamo mingi kuhusu Mungu miongoni mwa mwanadamu, bado mwili Wake unaweza pia kumruhusu mwanadamu kuwa na maarifa mengi, na anaweza hata kumshinda mwanadamu yeyote mwenye ganda la sawa nje. Maana Yeye si mwanadamu wa kawaida tu, bali ni Mungu mwenye umbo la nje kama la mwanadamu, na hakuna anayeweza kumwelewa au kumfahamu kikamilifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu mwenye mwili ndiyo Mungu amefanyika mwili ambaye ana umbo la kugusika, na ambaye anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu. Yeye si Roho asiyekuwa na umbo, bali mwili ambao unaweza kuhusiana na kuonekana kwa mwanadamu. Hata hivyo, Miungu mingi ambayo watu wanaamini kwayo ni miungu isiyo na mwili na umbo maalumu, na ambayo haifungwi na umbo maalumu. Kwa njia hii, Mungu mwenye mwili amekuwa adui wa wengi wanaomwamini Mungu, na wale ambao hawawezi kuukubali ukweli wa Mungu mwenye mwili, vilevile, wamekuwa maadui wa Mungu. … Ingawa watu wengi wamekuwa maadui wa Mungu kwa sababu ya mwili huu, Anapokamilisha kazi Yake, wale ambao wapo kinyume Chake hawataacha tu kuwa maadui Zake, bali kinyume Chake watakuwa mashahidi Wake. Watakuwa mashahidi watakaokuwa wameshindwa naye, mashahidi ambao wana ulinganifu na Yeye na ambao hawatenganishwi naye. Atamsababisha mwanadamu kujua umuhimu wa kazi Yake katika mwili kwa mwanadamu, na mwanadamu atajua umuhimu wa mwili huu katika maana ya uwepo wa mwanadamu, atajua thamani Yake halisi katika ukuaji wa maisha ya mwanadamu, aidha, atajua mwili huu utakuwa chemchemi ya uhai ambayo kwayo mwanadamu hataachana nayo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Licha ya kuwa Mungu amechukua umbo la Mwana wa Adamu wa kawaida katika kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ili kuwaokoa na kuwakamilisha wanadamu, licha ya Yeye kutofanya ishara na maajabu, na kutokuwa na sifa zinazozidi za mwanadamu au kimo kikubwa na Yeye kuwa shabaha la dhana za mwanadamu, kukana kwao, upinzani, na kukataa, ukweli ambao Kristo anaonyesha na kazi ya hukumu ambayo Anatekeleza vimempa mwanadamu ugavi wa neno la Mungu, na vimewaruhusu kufikia ukweli na kuona kuonekana kwa Mungu. Ingawa hatujaona nafsi halisi ya Mungu, tumeona tabia Yake ya asili, na kiini Chake kitakatifu, ambayo ni sawa tu na kana kwamba tulikuwa tumeiona nafsi Yake halisi. Tumemwona Mungu akiishi miongoni mwetu kwa kweli. Tunahisi kwa kweli kwamba tumenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi, tukiipitia kazi ya Mungu uso kwa uso na Mungu, na tukifurahia ruzuku ya maji hai ya uzima yanayotiririka kutoka kwa kiti cha enzi. Baada ya kupitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, tumekuja kutambua polepole makusudi ya ari ambayo Mungu anatumia kuwakokoa wanadamu, na tumeona kwamba gharama anayolipa Mungu na mateso Anayovumilia ili kuwaokoa wanadamu ni makubwa kweli. Yote ambayo Mungu anatufanyia sisi ni maonyesho ya upendo Wake na lengo lake ni wokovu wetu. Tunajidharau kwa ajili ya uasi na upumbavu wetu wa awali na tunaanza kumpenda na kumtii Mungu kweli. Baada ya kupitia kazi ya Mungu kufikia sasa, sote tumetambua kwamba mabadiliko tunayoyaona ndani yetu yote ni matokeo ya wokovu wa kupata mwili kwa Mungu! Kriso wa siku za mwisho ni wokovu mkuu wa wanadamu wapotovu. Yeye ndiye njia pekee ya kuelekea kwa ufahamu wa Mungu na kupokea sifa za Mungu! Hebu tusome kifungu kingine cha neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu asema, “Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. … Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Ukweli kwamba mmefika siku ya leo ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu, kwa sababu ni ukweli, uzima, na njia Aliyoleta ndivyo vilivyowaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya mwanadamu na Mungu, ikafupisha umbali kati yao, na kufungua kiungo kati ya mawazo ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp