Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Aliikaribisha Enzi ya Neema na Aliimaliza Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu Alipata mwili kwa mara nyingine, na Alitamatisha Enzi ya Neema na Akaikaribisha Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaoweza kukubali kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu wataongozwa kuingia katika Enzi ya Ufalme, na zaidi ya hayo wao binafsi watakuwa na uwezo wa kukubali uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alikuja miongoni mwa wanadamu na alifanya kazi nyingi, Alimaliza tu kazi ya kuwakomboa wanadamu wote na Akawa kama sadaka ya dhambi ya mwanadamu; Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu.

2

Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukuhitaji Yesu tu kuwa sadaka ya dhambi na kubeba dhambi za mwanadamu, lakini pia kulihitaji Mungu afanye kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake iliyopotoshwa na Shetani kikamilifu. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Alirudi katika mwili kumwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya, na Akaanza kazi ya kuadibu na hukumu. Kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wale wote wanaotii chini ya utawala Wake watafurahia ukweli wa juu zaidi na kupokea baraka kuu zaidi. Wataishi kikweli katika nuru, na watapata ukweli, njia na uzima.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp