Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 66

29/06/2020

Mimi Natawala katika ufalme, na zaidi ya hapo, Ninatawala katika ulimwengu mzima; Mimi ni Mfalme wa ufalme na pia Mkuu wa ulimwengu. Kutoka wakati huu na kuendelea, Nitawakusanya wote wasio wateule na Nitaanza kufanya kazi Yangu katika mataifa, Na Nitatangaza amri Yangu ya utawala kwa ulimwengu mzima, ili kwa mafanikio Niweze kuingia katika hatua ifuatayo ya Kazi Yangu. Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile Kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa. Wakati watu Wangu wanatawala na kushika madaraka duniani ndio pia itakuwa siku ambayo watu wote duniani watakuwa wameshindwa, na zaidi ya hayo, utakuwa wakati Wangu wa mapumziko—na hapo tu ndipo Nitawaonekania wale walioshindwa. Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu. Wote walioshindwa na kuwa watiifu mbele Yangu wana uwezo wa kuuona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, na uwezo wa kusikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa katika siku za mwisho, hii ni baraka Niliyoamua kabla, na hii haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Leo, Ninafanya kazi kwa namna hii kwa ajili ya kazi ya baadaye. Kazi Zangu zote zinahusiana, katika yote kuna wito na mwitikio: Kamwe hakuna hatua yoyote iliyokoma kwa ghafla, na kamwe hakuna hatua yoyote iliyofanywa kwa kujitegemea kivyake. Je, hivi sivyo ilivyo? Je, kazi ya siku za nyuma siyo msingi wa kazi ya leo? Je, maneno ya zamani si utangulizi wa maneno leo? Je, hatua za zamani si asili ya hatua za leo? Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu, na ndicho kilele cha Kazi Yangu; watu wote wanaishi katika nchi bila mwanga, na watu wote wanaishi huku kukiwa na tishio la mazingira yao. Kwa maneno mengine, ni maisha ambayo mwanadamu hajawahi kupitia kutoka wakati wa uumbaji mpaka siku ya leo, na hakuna yeyote katika enzi zote aliyeweza “kustarehe” na aina hii ya maisha, na hivyo Ninasema kwamba Ninafanya kazi ambayo haijawahi kufanyika mbeleni. Hii ndiyo hali halisi ya mambo, na hii ni maana ya ndani. Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu, ni nani asiyeweza kuwa na uoga kwa sababu ya jambo hili? Ni nani asiyekuwa na furaha katika hili? Mji mchafu wa Babeli hatimaye umefika mwisho wake; mwanadamu amekutana na dunia mpya kabisa, na mbingu na dunia zimebadilishwa na kufanywa mpya.

Wakati Najitokeza kwa mataifa yote na watu wote, mawingu meupe yanaenea angani na kunifunika. Na pia, ndege duniani wanaimba na kunichezea kwa shangwe, wakiangazia hali duniani, na hivyo kusababisha vitu vyote duniani kuwa hai, kusiwe tena na “kuwa vumbi” lakini badala yake kuishi katika hali ya uzima. Wakati Niko mawinguni, mwanadamu anatambua uso Wangu na macho Yangu kwa umbali, na kwa wakati huu yeye anahisi uoga kidogo. Katika siku za nyuma, yeye alisikia “kumbukumbu za kihistoria” kunihusu katika ngano, na matokeo yake ni kuwa anayo imani nusu na nusu shaka Kwangu. Yeye hajui Niliko Mimi, au ukubwa wa uso Wangu—je ni mpana kama bahari, au kama usio na mwisho kama malisho ya majani mabichi? Hakuna anayejua mambo haya. Ni wakati tu mwanadamu anapouona uso Wangu katika mawingu leo ndipo anapohisi kwamba Mimi wa hadithi ni wa kweli, na hivyo anakuwa na upendeleo zaidi Kwangu, na ni kwa sababu tu ya matendo Yangu ndio upendo wake Kwangu unazidi kuwa mkubwa kidogo. Lakini mwanadamu bado hanijui, na anaona tu sehemu moja Yangu katika mawingu. Baada ya hapo, Ninanyosha mikono Yangu na kuionyesha kwa mwanadamu. Mwanadamu anashangaa, na kufunika mdomo kwa mikono yake, akiwa na uoga kuwa Nitampiga chini kwa mkono Wangu, na hivyo anaongeza heshima kidogo kwa upendo wake. Mwanadamu anaweka macho yake juu ya kila hatua Yangu, akiwa na hofu kuu kuwa Nitampiga chini wakati yeye hayuko makini—lakini kutazamwa na mwanadamu hakunizuii Mimi, na Ninaendelea kufanya kazi iliyo mikononi Mwangu. Ni tu katika matendo yote Ninayofanya ndipo mwanadamu ana upendeleo fulani Kwangu, na hivyo hatua kwa hatua anakuja mbele Zangu kujiunga Nami. Wakati ukamilifu Wangu unafichuliwa kwa mwanadamu, mwanadamu atauona uso Wangu, na kutoka hapo Sitauficha au kujikinga kutoka kwa mwanadamu. Katika ulimwengu, Nitaonekana hadharani kwa watu wote, na walio nyama na damu wote wataona matendo Yangu yote. Wale wote ambao ni wa roho hakika wataishi kwa amani katika Nyumba Yangu, na bila shaka watafurahia baraka za ajabu pamoja na Mimi. Wale wote ambao Ninawajali hakika wataepuka kuadibu, na kwa hakika wataepuka maumivu ya roho na maumivu makali ya mwili. Mimi Nitaonekana hadharani kwa watu wote na kutawala na kutumia mamlaka, ili harufu ya maiti isisambae tena ulimwenguni; badala yake, manukato Yangu yataenea katika dunia nzima, kwa sababu siku Yangu inakaribia, mwanadamu anaamka, kila kitu kilicho duniani kiko katika utaratibu, na siku za kunusurika kwa dunia hazipo tena, kwa maana Mimi Nimefika!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp