Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Ufalme wa Mungu Umeonekana Duniani” | Sauti za Sifa 2026

18/01/2026

1

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme akaliaye kiti cha enzi, Atawala ulimwengu mzima, Akitazama kuelekea mataifa yasiyohesabika na watu wasiohesabika, na utukufu wa Mungu unang'aa ulimwenguni kote. Viumbe vyote hai ulimwenguni na hadi miisho ya dunia vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari, na viumbe vyote viishivyo vimefungua pazia zao katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli, na vimefufuliwa kana kwamba vimeamka kutoka ndotoni, kana kwamba hivyo ni chipuko zinazochipuka kutoka mchangani! Ah! Mungu mmoja wa kweli anaonekana mbele ya watu wa dunia. Ni nani anayethubutu kumchukulia Yeye kwa upinzani? Wote wanatetemeka kwa hofu. Wote wameshawishika kabisa, na wote wanaomba msamaha kwa kurudia. Watu wasiohesabika wanapiga magoti mbele Yake, na vinywa visivyohesabika vinamwabudu!

2

Mabara na bahari, milima, mito, na vitu vyote vinamsifu Yeye bila kikomo! Upepo mwanana wenye joto, ukiandamana na pumzi ya majira ya kuchipua, unaleta mvua nyepesi isiyokoma ya majira ya kuchipua. Vijito vinavyobubujika na umati ni sawa, wote wamejawa na huzuni na furaha, wakimwaga machozi ya kuhisi deni na kujilaumu. Mito, maziwa, mawimbi na mawimbi makubwa vyote vinaimba, vikilisifu jina takatifu la Mungu wa kweli! Sauti ya sifa inasikika kwa uwazi sana! Vitu vya zamani vilivyopotoshwa na Shetani wakati fulani—kila kimoja kitafanywa upya na vitabadilishwa na vitaingia katika ulimwengu mpya kabisa …

3

Hii ni tarumbeta takatifu, na imeanza kulia! Isikilize. Sauti hiyo, tamu sana, ni tamko kwenye kiti cha enzi. Inatangaza kwa kila taifa na watu kwamba wakati umefika, matokeo ya siku za mwisho yamewadia, mpango Wangu wa usimamizi umekamilika, ufalme Wangu umeonekana waziwazi duniani, na falme za dunia zimekuwa ufalme Wangu, Mimi ambaye ni Mungu. Tarumbeta Zangu saba zinalia kutoka katika kiti cha enzi, na mambo ya ajabu sana yatatukia! Ninawatazama watu Wangu kwa furaha, wanaoweza kuisikia sauti Yangu na kukusanyika kutoka kila taifa na nchi. Halaiki, wakimzungumzia Mungu wa kweli daima, wakisifu na kurukaruka bila kukoma! Wanatoa ushahidi kwa ulimwengu, na sauti ya ushahidi wao kwa Mungu wa kweli ni kama sauti ya ngurumo ya maji mengi. Halaiki itasongamana katika ufalme Wangu.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 36

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp