Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Jina la Mungu Hakika Litatukuzwa kama Kuu Miongoni mwa Mataifa” | Sauti za Sifa 2026

18/01/2026

1

Kusudi la hukumu Yangu ni kumwezesha binadamu anitii Mimi vyema zaidi, na kusudi la kuadibu Kwangu ni kumwezesha binadamu afikie mabadiliko mema zaidi. Ingawa kila kitu Ninachofanya ni kwa ajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya kazi yoyote ambayo si ya manufaa kwa mwanadamu, kwa maana Ninataka kuyafanya mataifa yote nje ya Israeli yawe na utii kama walivyo Waisraeli, kuwafanya wawe binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa kusimama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Yangu katika Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajali kuhusu mambo kama hayo, na badala yake wanajali tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi kile Ninachosema, watu wanabaki kuwa wasiojali kazi Ninayoifanya, badala yake wakilenga kwa moyo wote hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itaeneaje? Injili Yangu itahubiriwaje kotekote ulimwenguni?

2

Mnapaswa kujua kwamba kazi Yangu itakapoenea, Nitawatawanya, Nitawapiga kama vile Yehova alivyoyapiga makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili kwamba injili Yangu iweze kuenea ulimwenguni kote, ili kwamba kazi Yangu iweze kuenea katika Mataifa, na hivyo jina Langu litukuzwe kama kuu na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu lihimidiwe katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Katika enzi hii ya mwisho, acha jina Langu litukuzwe kama kuu miongoni mwa Mataifa, acha matendo Yangu yaonekane na watu wa Mataifa, acha waniite mwenye Uweza kwa sababu ya matendo Yangu, na maneno Yangu yatimie hivi karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi si Mungu wa Waisraeli tu, lakini pia Mungu wa watu wa Mataifa yote, hata yale mataifa ambayo Nimeyalaani. Nitawafanya watu wote waone kuwa Mimi ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa. Hii ndiyo kazi Yangu kuu zaidi, ndilo kusudi la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi pekee ambayo Ninatamani kutimiza katika siku za mwisho.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp