Filamu ya Kikristo | Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China | “Ujana wa Machozi yenye Damu”

11/11/2020

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii inasimulia hadithi ya kweli ya mateso ambayo familia ya Mkristo wa Kichina, Lin Haochen, ilipitia mikononi mwa chama cha CCP. Lin Haochen alifuata nyayo za baba yake na akamwamini Bwana, na matokeo yake ni kwamba kama mtoto alishuhudia maofisa wa jeshi wa kijiji chake wakija nyumbani kwake mara nyingi kuwatisha na kuwaogofya wazazi wake ili waache imani na juhudi zao za kueneza injili. Baada ya familia ya Lin Haochen ikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, waliteswa na kukamatwa kwa ukali hata zaidi na serikali ya CCP. Mamake Lin Haochen alifariki kutokana na ugonjwa alipokuwa akikimbia kukamatwa, na Lin Haochen, baba yake, na kaka yake mkubwa walilazimika kukimbia kutoka nyumbani, na waliona kuwa kurudi kulikuwa kugumu sana. Familia ambayo wakati mmoja ilikuwa yenye furaha na nzuri ilivunjwa na kutawanywa na mateso ya chama cha CCP ...

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp