Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

"Ivunje Laana" (2) - Bwana Atakaporudi, Ataonekanaje kwa Wanadamu?

Dondoo za Filamu   527  

Utambulisho

Siku za mwisho tayari zimefika, na waumini wengi wanatamani Bwana arudi na kuwachukua kwenda katika ufalme wa mbinguni. Lakini unajua Bwana atakavyoonekana kwetu Atakaporudi? Je, kweli itakuwa kama tunavyofikiria, kwamba Ataonekana wazi, moja kwa moja Akishuka juu ya wingu? Mwenyezi Mungu alisema, "Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu?… Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi?" "Mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. … Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu" (Neno Laonekana katika Mwili).