Christian Dance | Ulimwengu Unavuma kwa Sauti ya Sifa kwa Mungu | Sauti za Sifa 2026
14/01/2026
1
Nyimbo nyingi sana, densi nzuri sana—
ulimwengu umekuwa mfuro wa mawimbi ya bahari ya furaha!
Nyota zinaruka, mwezi unatabasamu, ulimwengu umejaa sifa;
tunashangilia na kuruka kwa furaha!
Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho,
Ameonyesha ukweli, akitikisa mataifa na madhehebu yote.
Watu wateule wa Mungu wanaisikia sauti Yake,
wakirejea mbele ya kiti Chake cha enzi kuabudu kwa umoja.
Akiwa Sayuni, Mungu anatazama upande wa ulimwengu mzima,
akifunua haki na utakatifu Wake.
Watu wote wa Mungu wamejawa na furaha, wakimsifu bila kikomo.
Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!
Msifuni Mungu, msifuni Mungu, msifuni Mungu!
2
Ili kumpenda Mungu, lazima tutimize wajibu wetu na kujali nia za Mungu.
Mioyo ya ndugu na dada zetu imekumbatiana kwa karibu,
na wote wanamsifu Mungu kwa umoja—wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee.
Unatoa wimbo na mimi ninatoa densi; unamshuhudia Mungu na mimi nashirikiana.
Tunamwaibisha ibilisi, joka kuu jekundu,
na kulitukuza jina la Mwenyezi Mungu.
Sote tumeiona tabia ya haki ya Mungu kupitia kazi Yake.
Watu wote wa Mungu wameuona uso Wake mtukufu,
na wote wanatafuta Kumpenda na Kumridhisha.
Tuko tayari kuwa waaminifu kwa Mungu milele.
Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!
Msifuni Mungu, msifuni Mungu, msifuni Mungu!
3
Mungu anapata utukufu duniani,
na mataifa yote na watu wote wa Mungu wanafurahi pamoja.
Maisha ya ufalme ni mazuri sana!
Mbingu mpya, dunia mpya, ufalme mpya.
Tunamchezea na kumwimbia Mungu nyimbo mpya—ni furaha iliyoje.
Nyimbo nzuri zaidi zinaimbwa kwa ajili ya Mungu,
densi nzuri zaidi zinatolewa kwa Mungu.
Tunatoa mioyo yetu ya kweli kwa Mungu, na tunampenda kwa usafi na unyofu.
Watu wote wa Mungu na vitu vyote vitamsifu milele, bila kukoma!
Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!
Msifuni Mungu, msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Ee Sayuni, ee Sayuni, utukufu ulioje! Makao ya Mungu yanametameta kwa mng'aro,
mwanga mtukufu ukimiminika katika ulimwengu mzima.
Mwenyezi Mungu anaketi kwenye kiti Chake cha enzi huku akitabasamu,
akiutazama mwonekano mpya wa ulimwengu.
Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!
Msifuni Mungu, msifuni Mungu, msifuni Mungu!
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video