Wimbo wa Dini | Watu Waaminifu Tu Ndio Wana Mfano wa Binadamu | Asante kwa Upendo na Wokovu wa Mungu

26/06/2019

Kwa ajili ya umaarufu na faida niliacha viwango vyote vya kutenda,

na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.

Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.

Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.

Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,

bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Utajiri wa maisha na raha za muda mfupi

hazingeweza kuficha utupu na maumivu ndani ya moyo wangu.

Mbona ni vigumu sana kuwa na uadilifu maishani?

Mbona wanadamu ni wenye hila sana, wabaya sana?

Hii ni dunia ya aina gani? Nani anayeweza kuniokoa?

Hii ni dunia ya aina gani? Nani anayeweza kuniokoa?

Nilisikia sauti ya Mungu na kurudi mbele ya Mungu.

Nafaidika sana kutokana na kusoma maneno ya Mungu kila siku.

Kwa kuelewa ukweli mwingi, sasa nina kanuni za tabia za kibinadamu.

Ni ukweli unaoonyeshwa na Mungu ndio huutakasa upotovu wangu.

Maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu yatembea nami maishani mwangu.

Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani.

Hakuna udanganyifu, hakuna uongo, ninaishi katika nuru.

Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu, na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe.

Nikipitia majaribio na usafishaji, nimeuona uso wa Mungu,

na kupata maisha mapya ndani ya maneno ya Mungu.

Sasa naweza kuwa mtu mwaminifu, nitupe hila na udanganyifu wangu.

Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!

Nina shukrani milele kwa Mwenyezi Mungu. Asante Mwenyezi Mungu!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp