Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia

01/07/2018

Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi. Biblia ilikuwa imepata nafasi takatifu moyoni mwake, mahali pa mamlaka ya juu na isiyoweza kushindwa. Hata hivyo, katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kanisa lake lilianza kuwa tupu siku baada ya siku, na Feng Jiahui na wafanyakazi wenzake walianza kuhisi giza likiingia ndani ya roho zao, na hawakuweza kuhisi uwepo wa Bwana miongoni mwao.... Aliwaalika wahubiri kutoka katika makanisa mengine ili kusaidia kurejesha kanisa, lakini bila mafanikio …

Wakati mmoja, Ndugu Yuan, mfanyakazi mwenzake Feng Jiahui alimwalika shahidi kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu aje kanisani. Shahidi alipokuwa akifanya ushirika juu ya ukweli kuhusu Biblia, kila kitu alichosema kilikuwa cha utendaji, wazi sana, na waumini waliona kuwa ya faida sana kwao. Hata hivyo, Feng Jiahui aliendelea kushikilia Biblia, akisisitiza kwa uthabiti kwamba imani katika Mungu lazima iwe na msingi katika Biblia, na kuondoka kwa Biblia kulikuwa uzushi. Baadaye, baada ya kuwa na mjadala mkubwa, Feng Jiahui hatimaye alielewa... undani wa Biblia na kiini cha kweli cha Biblia: Biblia ni kumbukumbu tu ya hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, na Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu, sembuse kufanya kazi ya Mungu ya wokovu kwa ajili Yake. Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima kwa mwanadamu, na Mungu pekee ndiye anaweza kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, sisi ambao tunamwamini Mungu lazima tufuate nyayo za Mungu, na wakati huo tu ndiyo tutaweza kufikia njia ya uzima wa milele. Hatimaye, Feng Jiahui aliweza kwenda zaidi ya Biblia, kukubali kazi ya Mungu ya siku zile za mwisho, na kuwaongoza waumini katika kanisa lake kurudi kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp