Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 12

22/05/2020

Wakati wakimfuata Mungu, ni nadra sana kwa watu kutilia maanani makusudi ya Mungu, na wanatilia maanani fikira za Mungu na mwelekeo wa Mungu kwa binadamu kwa nadra sana. Ninyi hamwelewi fikira za Mungu, kwa hivyo mnapoulizwa maswali yanayohusisha nia za Mungu, yanayohusisha tabia ya Mungu, mnaingia katika hali ya kutokuwa na hakika; mnakuwa kwa kweli hamna uhakika, na mnakisia au kubahatisha. Mwelekeo huu ni upi? Unathibitisha hoja hii: Watu wengi wanaomwamini Mungu wanamchukulia kuwa hewa tupu, asiyebainika. Kwa nini Nasema hivyo? Kwa sababu kila wakati mnapokumbwa na suala, hamzijui nia za Mungu. Kwa nini hamzijui? Si kwamba hamzijui tu kwa sasa. Badala yake kuanzia mwanzo hadi mwisho hamjui mwelekeo wa Mungu katika suala hili. Kwenye nyakati zile ambazo huwezi kuona na hujui mwelekeo wa Mungu, umewahi kuutafakaria? Umeutafuta? Umewasiliana ili kuupata? La! Hii inathibitisha hoja: Mungu unayemsadiki na Mungu wa kweli hawajaunganika. Wewe, unayemsadiki Mungu, unafikiria Mungu kuhusu mapenzi yako, unafikiria tu kuhusu mapenzi ya kiongozi wako, na unafikiria tu yale mambo ya juujuu na maana ya kifalsafa ya neno la Mungu, lakini hujaribu kwa kweli kujua na kutafuta mapenzi ya Mungu kamwe. Sivyo ndivyo hali ilivyo? Kiini halisi cha suala hili hakipendezi! Kwa miaka na mikaka Nimeona watu wanaomsadiki Mungu. Kusadiki huku kunachukua mfumo gani? Baadhi ya watu wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu. Watu hawa hawana majibu ya maswali kuhusu uwepo wa Mungu kwa sababu hawawezi kuhisi au kuwa na ufahamu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu, sikuambii hata kuuona waziwazi au kuuelewa. Kwa nadharia yao, watu hawa wanafikiria kwamba Mungu hayupo. Baadhi wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni binadamu. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hawezi kufanya mambo yale ambayo wao hawawezi kufanya, na kwamba Mungu anafaa kufikiria namna wanavyofikiria. Ufafanuzi wa mtu huyu kuhusu Mungu ni “mtu asiyeonekana na asiyegusika.” Kunalo pia kundi la watu wanaosadiki katika Mungu kana kwamba Yeye ni kikaragosi. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hana hisia, kwamba Mungu ni sanamu. Wakati wanapokabiliwa na suala, Mungu hana mwelekeo, hana mtazamo, hana mawazo; Anatawaliwa na binadamu. Watu wanasadiki tu wanavyotaka kusadiki. Wakimfanya kuwa mkubwa, Yeye ni mkubwa; wakimfanya kuwa mdogo, Yeye ni mdogo. Wakati wanapotenda dhambi na wanahitaji rehema ya Mungu, wanahitaji uvumilivu wa Mungu, wanahitaji upendo wa Mungu, basi Mungu anafaa kutoa rehema Zake. Watu hao wanafikiria kuhusu Mungu kwenye akili zao binafsi na kumfanya Mungu kutimiza mahitaji yao na kutosheleza matamanio yao yote. Haijalishi ni lini na ni wapi, na haijalishi hata mtu huyu anafanya nini, watakubali mvuto huu katika matendo yao kwa Mungu na kusadiki kwao katika Mungu. Kuna hata wale wanaosadiki katika Mungu kuweza kuwaokoa baada kuikera tabia ya Mungu. Hii ni kwa sababu wanasadiki kuwa upendo wa Mungu hauna mipaka, tabia ya Mungu ni haki, na kwamba bila kujali ni vipi ambavyo watu wanakosea Mungu, Hatakumbuka chochote. Kwa sababu makosa ya binadamu, dhambi za binadamu na kutotii kwa binadamu ni maonyesho ya mara moja ya tabia ya mtu huyo, Mungu atawapatia watu fursa, kuvumilia na kuwa na subira nao. Mungu angali atawapenda kama awali. Kwa hivyo tumaini la wokovu wao lingali kubwa. Kwa hakika, haijalishi ni vipi mtu anavyosadiki Mungu, mradi tu hafuatilii ukweli basi Mungu anashikilia mwelekeo mbaya kwake. Hii ni sababu wakati unamsadiki Mungu, labda unakithamini kile kitabu cha neno la Mungu unakichambua kila siku, unakisoma kila siku, lakini unamweka Mungu halisi pembeni, unamchukulia kama hewa tupu, unamchukulia Yeye kama mtu, na baadhi yenu mnamchukulia kuwa kikaragosi. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu kutokana na vile Ninavyoona, licha ya kama unakabiliwa na suala au kukumbana na hali, yale mambo yanayopatikana katika nadharia yako, yale mambo ambayo yameimarishwa ndani kwa ndani—hakuna kati ya haya ambayo yana uunganisho wa neno la Mungu au yanafuatilia ukweli. Unajua tu kile wewe mwenyewe unatafuta, maoni yako wewe binafsi, na kisha mawazo yako binafsi, mitazamo yako binafsi inalazimishiwa Mungu. Inakuwa mitazamo ya Mungu, ambayo inatumika kama viwango vya kutii bila kusita. Kwa muda, kuendelea namna hii kunakufanya uwe mbali zaidi na Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp