Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 15

19/05/2020

Watu Huishia Kumfafanua Mungu Kutokana na Uzoefu Wao

Wakati wa kuwasilisha mada ya kumjua Mungu, mmegundua kitu? Mmegundua kwamba mwelekeo wa sasa wa Mungu umepitia mabadiliko? Je, mwelekeo wa Mungu kwa wanadamu hauwezi kubadilika? Je, siku zote Mungu atavumilia hivi, huku akimpa upendo Wake wote na rehema kwa binadamu bila kikomo? Suala hili pia linahusu kiini halisi cha Mungu. … Punde tu watu wanapojua kwamba Mungu anawapenda wanadamu, wanamfafanua Mungu kama ishara ya upendo: Haijalishi kile wanachofanya watu, haijalishi namna wanavyotenda mambo, haijalishi vipi wanavyomshughulikia Mungu na haijalishi ni vipi wasivyotii, hakuna chochote kinachojalisha kwa sababu Mungu ni upendo na upendo wa Mungu hauna mipaka na haupimiki. Mungu anao upendo, hivyo basi Anaweza kuvumilia watu; Mungu anao upendo, hivyo basi Anaweza kuwa mwenye rehema kwa watu, mwenye rehema kwa kutokomaa kwao, mwenye rehema kwa kutojua kwao, na mwenye rehema kwa kutotii kwao. Hivi ndivyo ilivyo kwa kweli? Kwa baadhi ya watu, wakati wamepitia subira ya Mungu mara moja, au mara chache, watashughulikia suala hili kama mtaji katika uelewa wao wa Mungu, wakisadiki kwamba Mungu atakuwa mara moja na milele mwenye subira kwao, atakuwa mwenye rehema kwao, na kwenye mkondo wa maisha yao watachukua subira ya Mungu na kuichukulia kama kiwango cha ni vipi ambavyo Mungu anawashughulikia. Kunao pia watu ambao, wakati wamepitia uvumilivu wa Mungu mara moja, daima watamfafanua Mungu kuwa uvumilivu, na uvumilivu huu hauna mipaka, hauna masharti, na hata usio na kanuni zozote. Je, kusadiki huku ni sahihi? Kila wakati mambo kuhusu kiini cha Mungu au tabia ya Mungu yanapozungumziwa, mwaonekana mmekanganywa mno. Kuwaona mkiwa hivi kunanifanya Mimi kukasirika kidogo. Mmeusikia ukweli mwingi kuhusiana na kiini halisi cha Mungu; mmeweza pia kusikiliza mada mengi kuhusiana na tabia ya Mungu. Hata hivyo, katika akili zenu masuala haya, na ukweli wa dhana hizi, ni kumbukumbu tu kutokana na nadharia na maneno yaliyoandikwa. Hakuna kati yenu anaweza kupitia kile ambacho tabia ya Mungu inamaanisha katika maisha yenu halisi, wala hamwezi kuona tu tabia ya Mungu ni nini. Hivyo basi, nyote mmechanganyikiwa katika kusadiki kwenu, nyote mnasadiki bila kujua, hadi kufikia kiwango ambacho mnao mwelekeo usiofaa kwa Mungu, kwamba mnamweka pembeni. Mwelekeo kama huu kwa Mungu unawaongoza wapi? Mnaongozwa katika hali ya kutoa hitimisho siku zote kuhusu Mungu. Punde unapopata maarifa kidogo, unahisi umetosheka kweli, unahisi ni kana kwamba umempokea Mungu kwa uzima Wake wote. Baadaye unahitimisha kwamba hivi ndivyo Mungu Alivyo, na humruhusu kuendelea mbele na shughuli Zake kwa furaha zaidi. Na kila Mungu anapofanya jambo jipya, hukubali kwamba Yeye ni Mungu. Siku moja, wakati Mungu atakaposema: “Simpendi binadamu tena; Sitoi rehema kwa binadamu tena; Sina uvumilivu au subira yoyote kwa binadamu tena; Nimejaa chuki na uhasama kupindukia kwa binadamu,” watu watakinzana na aina hii ya taarifa kutoka kwenye ndani ya mioyo yao. Baadhi yao wataweza hata kusema: “Wewe si Mungu wangu tena; Wewe si Mungu ninayetaka kufuata tena. Kama hivi ndivyo Unavyosema, basi Hujafuzu tena kuwa Mungu wangu, na sitaki kuendelea kukufuata Wewe. Kama Hunipi rehema, hunipi upendo, hunipi uvumilivu, basi nami sitakufuata Wewe tena. Kama Utakuwa mvumilivu tu kwangu bila kikomo, utakuwa mwenye subira kwangu mimi, na kuniruhusu mimi kuona kwamba Wewe ni upendo, kwamba Wewe ni subira, kwamba Wewe ni uvumilivu, hapo tu ndipo nitakapoweza kukufuata Wewe, na hapo tu ndipo nitakapoweza kuwa na ujasiri kukufuata mpaka mwisho. Kwa sababu ninapata subira na rehema Yako, kutotii kwangu na dhambi zangu zinaweza kusamehewa bila kikomo, kuondolewa bila kikomo, na ninaweza kutenda dhambi wakati wowote na mahali popote, kutubu na kusamehewa wakati wowote na mahali popote, na kukughadhabisha wakati wowote na mahali popote. Hufai kuwa na fikira au hitimisho Zako binafsi kuhusiana na mimi.” Ingawa huenda usifikirie kuhusu aina hii ya swali kwa namna ya kibinafsi na ya kufahamu kama hiyo, kila unapomchukulia Mungu kuwa zana ya dhambi zako kusamehewa na kifaa cha kutumika cha kupata hatima nzuri, tayari unamweka kwa njia isiyoeleweka Mungu aliye hai na katika hali ya kukupinga wewe, kuwa adui yako. Hivi ndivyo Ninavyoona. Unaweza kuendelea kusema, “Ninasadiki Mungu”; “Ninafuatilia ukweli”; “Ninataka kubadilisha tabia yangu”; “Ninataka kuwa huru dhidi ya ushawishi wa giza”; “Ninataka kumtosheleza Mungu”; “Nataka kumtii Mungu”; “Ninataka kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya wajibu wangu vizuri”; na kadhalika. Hata hivyo; haijalishi ni vipi utakavyosema kinasikika kuwa kizuri, haijalishi ni nadharia kiasi kipi unayojua, haijalishi ni vipi nadharia hiyo inavyovutia, ni vipi nadharia hiyo ilivyo na heshima, hoja ya mambo ni kwamba kunao wengi wenu ambao tayari wamejifunza namna ya kutumia taratibu, falsafa, nadharia mlizojifunza katika kuhitimisha mambo kuhusu Mungu, na kumweka yeye katika upinzani na nyinyi wenyewe kwa njia ambayo ni ya kimaumbile kabisa. Ingawa umejifunza barua na kujifunza falsafa, bado hujaingia kwa hakika katika uhalisia wa ukweli, hivyo basi ni vigumu sana kwako kuwa karibu na Mungu, kumjua Mungu, na kumwelewa Mungu. Hali hii inasikitisha!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp