Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 28

19/05/2020

Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.

Watu wengi zaidi wanajua upinde wa mvua ni nini na wamesikia baadhi ya hadithi zinazohusiana na pinde za mvua. Kuhusiana na hadithi ile ya upinde wa mvua kwenye biblia, baadhi wa watu wanaisadiki, baadhi wanaichukulia tu kama hadithi ya kale, huku wengine hawaisadiki kamwe. Haijalishi ni nini, kila kitu kilichofanyika kuhusiana na upinde wa mvua ndicho kila kitu ambacho Mungu Alifanya hapo awali, na mambo yaliyofanyika katika mchakato huu wa usimamizi wa Mungu wa binadamu. Mambo haya yamerekodiwa vivyo hivyo kwenye Biblia. Rekodi hizi hazituambii chochote kuhusu hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo au nia zake nyuma ya maneno haya ambayo Mungu alisema. Zaidi, hakuna anayeweza kutambua ni nini Mungu alikuwa akihisi Aliposema maneno hayo. Hata hivyo, hali ya akili ya Mungu kuhusiana na hiki kitu chote inafichuliwa katikati ya mistari ya maandishi. Ni kana kwamba fikira zake wakati huo zinatoka kwenye ukurasa kupitia kila neno na kauli ya neno la Mungu.

Fikira za Mungu ni kile ambacho watu wanafaa kujali kuhusu na kile wanafaa kujaribu kujua zaidi. Hii ni kwa sababu fikira za Mungu zinahusiana kwa karibu na uelewa wa binadamu wa Mungu na uelewa wa binadamu wa Mungu ni kiungo muhimu sana kwa kuingia kwa binadamu katika maisha. Hivyo ni nini alichokuwa akifikiria Mungu wakati huo mambo haya yalipofanyika?

Hapo mwanzo, Mungu aliumba binadamu ambao katika macho Yake walikuwa wazuri sana na karibu na Yeye, lakini waliangamizwa na gharika baada ya kuasi dhidi Yake. Je, ilimwumiza Mungu kwamba binadamu kama hao walitoweka tu papo hapo hivyo? Bila shaka Aliumizwa! Kwa hivyo Maonyesho Yake ya maumivu haya yalikuwa nini? Ilirekodiwa vipi kwenye Biblia? Ilirekodiwa kwenye Biblia kama: “Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia.” Sentensi hii rahisi inafichua fikira za Mungu. Kuangamizwa huku kwa ulimwengu kulimpa Yeye maumivu sana. Kwa maneno ya binadamu, Alikuwa na huzuni sana. Tunaweza kufikiria: Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa maisha inavyofanana baada ya kuangamizwa na gharika? Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa binadamu inavyofanana hivi sasa? Hakuna makazi ya binadamu, hakuna viumbe walio hai, maji kila mahali na machafuko kabisa juu ya maji. Hilo ndilo lililokuwa onyesho la kusudio la asili ya Mungu wakati alipoumba ulimwengu? Bila shaka la! Nia asilia ya Mungu ilikuwa ni kuyaona maisha katika maeneo yote, kuwaona wanadamu Aliowaumba wakimwabudu Yeye, si tu kwa Nuhu kuwa mtu pekee anayemwabudu, au kuwa wa pekee ambaye angejibu mwito Wake ili kukamilisha kile alichoaminiwa kufanya. Wakati binadamu walitoweka, Mungu hakuona kile alichonuia awali lakini kinyume cha mambo. Ni vipi ambavyo moyo Wake usingekuwa katika maumivu? Hivyo Alipokuwa akifichua tabia Yake na kuelezea hisia Zake, Mungu alifanya uamuzi. Ni aina gani ya uamuzi Alifanya? Kuunda uta mawinguni (kumbuka: upinde wa mvua tunaouona) kama agano na binadamu, ahadi kwamba Mungu hangemwangamiza mwanadamu kwa gharika tena. Wakati huohuo, ulikuwa pia ni kuwaambia watu kwamba Mungu aliwahi kuangamiza ulimwengu kwa gharika, kumfanya mwanadamu kukumbuka milele ni kwa nini Mungu alifanya kitu kama hicho.

Je, kuangamizwa kwa ulimwengu wakati huu kulikuwa ni jambo alilotaka Mungu? Bila shaka lilikuwa ni jambo asilotaka Mungu Huenda tukaweza kufikiria sehemu ndogo ya picha ile ya kusikitikia ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu lakini hatuwezi kukaribia kufikiria namna hali ilivyokuwa wakati huo mbele ya macho ya Mungu. Tunaweza kusema kwamba, haijalishi kama ni watu wa sasa au wa wakati huo, hakuna yeyote anayeweza kufikiria au kutambua ni vipi Mungu alikuwa akihisi Aliposhuhudia tukio hilo, picha hiyo ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwake kwa gharika. Mungu alilazimishwa kufanya haya kutokana na kutotii kwa binadamu, lakini maumivu ambayo moyo wa Mungu ulipitia kutokana na maangamizo haya ya ulimwengu kwa gharika ni uhalisia ambao hakuna anayeweza kuufikiria au kuutambua. Ndiyo maana Mungu aliweka agano na mwanadamu, ambalo lilikuwa ni kuambia watu kukumbuka kwamba Mungu aliwahi kufanya kitu kama hiki, na kuapa kwamba Mungu asingewahi kuangamiza ulimwengu kwa njia hii tena. Katika agano hili, tunauona moyo wa Mungu—tunaona kwamba moyo wa Mungu ulikuwa katika maumivu Alipoangamiza binadamu hawa. Katika lugha ya binadamu, wakati Mungu aliangamiza mwanadamu na Akaona mwanadamu akitoweka, moyo Wake ulikuwa ukiomboleza na kuvuja damu. Je, hivyo sivyo tunavyoweza kuifafanua kwa njia bora zaidi? Maneno haya yanatumika na binadamu kuonyesha hisia za binadamu, lakini kwa sababu lugha ya binadamu inao ukosefu mwingi, kuitumia kufafanua hisia za Mungu hakuonekani kuwa mbaya sana kwangu Mimi, na wala si kubwa mno. Angaa inawapa uelewa sahihi kabisa, wa kufaa zaidi, wa hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo. Sasa mtafikiria nini mtakapouona upinde wa mvua tena? Angaa mtakumbuka namna ambavyo Mungu aliwahi kuwa katika huzuni kwa sababu ya kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Mtakumbuka namna, hata kama Mungu aliuchukia ulimwengu huu na kudhalilisha binadamu hawa, Alipowaangamiza wanadamu Alioumba kwa mikono Yake mwenyewe, moyo Wake ulikuwa ukisononeka, ukipambana kuachilia, ukihisi kusita, na kuhisi vigumu kuvumilia mambo. Tulizo lake pekee lilikuwa katika familia ya wanane ya Nuhu. Ulikuwa ni ushirikiano wa Nuhu uliofanya jitihada Zake za kipekee za kuumba viumbe wote kuwa cha thamani. Kwa wakati ambao Mungu alikuwa akiteseka, hili ndilo jambo tu ambalo lingeweza kusawazisha maumivu Yake. Kuanzia hapo, Mungu aliweka matarajio Yake yote ya binadamu kwa familia ya Nuhu, akitumai kwamba wangeishi chini ya baraka Zake na si laana Yake, akitumai kwamba wasingewahi kumwona Mungu akiuangamiza ulimwengu kwa gharika na pia akitumai kwamba wasingeangamizwa.

Ni sehemu gani ya tabia ya Mungu tunayofaa kuelewa kutoka hapa? Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa binadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya binadamu. Tunaona nini kutoka kwa haya? Bila shaka, tunaona kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kweli na si tu jambo ambalo Analizungumzia tu bila matendo. Ni jambo hakika, linaloweza kushikika na kutambulika, si bandia, halijatiwa najisi, halidanganyi wala halisingizii. Mungu kamwe hatumii uongo au kuunda taswira za bandia ili kufanya watu kuona kwamba Yeye anapendeka. Kamwe hatumii ushuhuda wa uongo ili kuwafanya kuona uzuri Wake, au kuringia uzuri wake na utakatifu Wake. Je, dhana hizi za tabia ya Mungu zinastahili upendo wa binadamu? Kwani nazo hazistahili kuabudiwa? Kwani nazo hazistahili kupendwa sana? Kwa sasa, Ningependa kuwauliza: Baada ya kuyasikia maneno haya, mnafikiri kwamba ukubwa wa Mungu ni tu maneno kwenye kipande cha karatasi? Je, uzuri wake Mungu ni maneno matupu tu? La! Bila shaka la! Mamlaka ya juu, ukubwa, utakatifu, uvumilivu, upendo, wa Mungu na kadhalika—dhana hizi zote mbalimbali za tabia ya Mungu na kiini chake zinaanza kutekelezwa kila wakati Anapoanza kazi Yake, zikiwa katika mapenzi Yake kwa binadamu, na pia zikitimizwa na kuonyeshwa kwa kila mtu. Licha ya kama umewahi kuzihisi awali, Mungu anamtunza kila mtu katika kila njia inayowezekana, kwa kutumia moyo Wake wa dhati, hekima, na mbinu mbalimbali ili kupashana mioyo ya kila mtu, na kuzindua roho ya kila mmoja. Huu ni ukweli usiopingika.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp