Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 43

08/06/2020

Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 2:3 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu.

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani

Ayubu 2:4-5 Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio

Ayubu 2:9-10 Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya? Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.

Ayubu 3:3 Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba.

Upendo wa Ayubu wa Njia ya Mungu Unazidi Yote Mengine

Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu” (Ayubu 2:3). Katika maneno haya Mungu Anarudia swali moja kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha ukadiriaji wa uthibitisho wa Yehova Mungu kuhusu kile kilichoonyeshwa na kuishi na kudhihirishwa na Ayubu kwenye jaribio lake la kwanza, na ule ambao si tofauti na ukadiriaji wa Mungu wa Ayubu kabla ya kupitia jaribio lile la Shetani. Hivi ni kusema, kabla jaribio halijamfika, katika macho ya Mungu Ayubu alikuwa mtimilifu, na hivyo basi Mungu Alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki, alistahili kubarikiwa kwa macho ya Mungu. Baada ya jaribio, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova Mungu. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu kumpongeza, na kumpa alama zote. Kwani machoni mwa Ayubu, watoto wake au rasilimali zake hazikutosha kumfanya yeye kumkataa Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, isingeweza kusawazishwa na watoto wake au kipande chochote cha mali yake. Kwenye jaribio la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwa sababu tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea tuzo kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.

Kwa Ayubu, hali hii aliyoipitia ilikuwa ya kweli na ambayo ilisafisha nafsi yake ikawa safi, ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza uwepo wake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu ya kutosha iliyojaribu utiifu wake kwa, na yeye kumcha Mungu. Jaribio hili lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka ule wa bwana tajiri hadi kwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia likamruhusu kupitia dhuluma za shetani kwa wanadamu. Ufukara wake haukumfanya kuchukia Shetani; badala yake, kwenye vitendo vibovu vya Shetani aliuona ubaya na hali ya kudharau ya Shetani pamoja na uadui wa Shetani na uasi wake kwa Mungu, na hali hii ilimhimiza vizuri zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kugeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au urithi, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa jaribio, Ayubu alikuwa pia amepata jambo jingine: Alikuwa amepata utajiri mkubwa katikati ya majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.

Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova Mungu na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu, na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa: Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp