Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 196

23/12/2020

Kinachofuata ni mzunguko wa uhai na mauti wa watendaji huduma. Tulisema asili za watendaji huduma ni gani? (Wengine walikuwa wasioamini, wengine walikuwa wanyama.) Hawa watendaji huduma walipata mwili baada ya kuwa wasioamini au wanyama. Na ujio wa hatua ya mwisho ya kazi, Mungu amechagua kundi la watu hawa kutoka kwa wasioamini, na ni kundi ambalo ni maalum. Nia ya Mungu ya kuchagua watu hawa ni kuhudumia kazi Yake. “Huduma” si neno la jamala kutamka, wala si kitu ambacho mtu yeyote angependa, lakini tunapaswa kuona ambao linawalenga. Kuna umuhimu maalum katika uwepo wa watendaji huduma wa Mungu. Hamna mwingine awezaye kuchukua nafasi yao, kwa kuwa walichaguliwa na Mungu. Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. Haijalishi kama wanafanya kazi ngumu, wanafanya kazi fulani, au wanajiandaa kufanya kazi fulani, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa hawa watu? Je, anawadai sana kwa masharti Yake kwao? (La, Mungu anawataka wawe waaminifu.) Watendaji huduma pia wanapaswa kuwa waaminifu. Haijalishi asili zako, au kwa nini Mungu alikuchagua, ni lazima uwe mwaminifu: Ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa kile anachokuagiza, na vilevile kazi unayoiwajibikia na jukumu unalolifanya. Ikiwa watendaji huduma wanaweza kuwa waaminifu, na kumridhisha Mungu, basi hatima yao itakuwaje? Wataweza kubaki. Je, ni baraka kuwa mtendaji huduma anayebaki? Kubaki kunamaanisha nini? Hii baraka inamaanisha nini? Kihadhi, hawafanani na wateule wa Mungu, wanaonekana tofauti. Kwa hakika, hata hivyo, wakipatacho katika maisha haya siyo sawa na wakipatacho wateule wa Mungu? Angalau, katika haya maisha ni sawa. Hamlipingi hili, naam? Matamko ya Mungu, neema ya Mungu, riziki ya Mungu, baraka za Mungu—ni nani hafurahii vitu hivi? Kila mtu anafurahia wingi wa haya. Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Kama unaweza kuhudumu hadi mwisho, ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kukamilisha kazi upewayo na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. Inamaanisha nini ukiwa mmoja wa wateule wa Mungu? Inamaanisha kuwa hawatapata tena mwili kama wanyama au wasioamini. Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.

Lakini kuna watendaji huduma ambao hawana uwezo wa kumtumikia Mungu hadi mwisho; wakati wa huduma yao, kuna wale ambao wanajitoa nusu na kutelekeza Mungu, kuna wale ambao hufanya mambo mengi mabaya, na hata wale ambao wanasababisha madhara makubwa na kufanya uharibifu mkubwa kwa Kazi ya Mungu, kuna hata watendaji huduma ambao humlaani Mungu, na kadhalika—na ni nini maana ya matokeo haya yasiyorekebishika? Matendo maovu yoyote kama hayo humaanisha kufikia mwisho kwa huduma yao. Kwa sababu matendo yako wakati wa huduma yamekuwa maovu sana, kwa sababu umevuka mipaka yako, wakati Mungu anaona huduma yako haijafikia kiwango Atakutoa ustahiki wa kutoa huduma, Hatakubali ufanye huduma, Atakutoa mbele ya macho Yake, na kutoka katika nyumba ya Mungu. Au ni kwamba hutaki kufanya huduma? Je, siku zote hutamani kufanya maovu? Je, siku zote wewe si mwaminifu? Sawa basi, kuna suluhisho rahisi: Utanyang’anywa ustahiki wako wa kuhudumu. Kwa Mungu, kunyang’anya mtendaji huduma ustahiki wa kufanya huduma kuna maana kuwa mwisho wa mtendaji huduma huyu umetangazwa, na hatakuwa anastahili kufanya huduma kwa Mungu tena, Mungu hahitaji huduma zake tena, na haijalishi ni vitu vipi vizuri atasema, maneno haya yatabaki ya bure. Mambo yanapofikia kiwango hiki, hii hali itakuwa isiyorekebishika; watendaji huduma kama hawa hawana njia ya kurudi nyuma. Na Mungu huwafanyia nini watendaji huduma kama hawa? Anawaachisha tu kutoa huduma? La! Je, Anawazuia tu wasibaki? Au anawaweka katika upande mmoja. Na kuwangoja wabadilike? Hafanyi hivyo. Kwa kweli Mungu hana upendo sana kwa watendaji huduma. Iwapo mtu ana aina hii ya mwelekeo katika huduma yake kwa Mungu, Mungu, kutokana na matokeo ya mwelekeo huu, Atawanyang’anya ustahiki wao wa kutoa huduma, na kwa mara nyingine kuwatupa tena miongoni mwa wasioamini. Na ni ipi hatima ya watendaji huduma waliorudishwa tena kati ya wasioamini? Ni sawa na ile ya wasioamini; kupata mwili kama wanyama na kupokea adhabu ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho. Na Mungu hatakuwa na maslahi ya kibinafsi katika adhabu yao, kwa kuwa hawana umuhimu wowote tena katika kazi ya Mungu. Huu si mwisho tu wa maisha yao ya imani kwa Mungu, ila mwisho wa hatima yao pia, kutangazwa kwa hatima yao. Kwa hiyo watendaji huduma wakihudumu vibaya, watapata matokeo wao wenyewe. Kama mtendaji huduma hana uwezo wa kufanya huduma hadi mwisho kabisa, au amenyang’anywa ustahiki wake wa kutoa huduma katikati ya njia, basi watatupwa miongoni mwa wasioamini—na kama watatupwa miongoni mwa wasioamini watashughulikiwa sawa na jinsi mifugo wanavyoshughulikiwa, sawa na watu wasio na akili au urazini. Ninapoielezea namna hiyo, unaelewa, naam?

Hivyo ndivyo Mungu anavyoushughulikia mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wake na watendaji huduma. Mnajihisi vipi baada ya kusikia haya? Nimewahi kuzungumza kuhusu mada ambayo Nimeitaja sasa hivi, mada ya wateule wa Mungu na watendaji huduma? Kwa kweli Nimewahi, lakini hamkumbuki. Mungu ni mwenye haki kwa wateule wake na watendaji huduma. Kwa vyovyote vile Yeye ni mwenye haki, siyo? Kuna mahali popote unaweza kupata makosa? Wapo watu ambao watasema: “Kwa nini Mungu ni mvumilivu sana kwa wateule? Na kwa nini anawavumilia kidogo sana watendaji huduma?” Kuna yeyote angependa kuwatetea watendaji huduma? “Je, Mungu anaweza kuwapa watendaji huduma muda zaidi, na kuwa mstahimilivu na mvumilivu zaidi kwao?” Haya maneno yako sahihi? (Hapana, hayapo sahihi.) Na ni kwa nini hayapo sahihi? (Kwa kuwa tumeonyeshwa neema kweli kwa kufanywa kuwa watendaji huduma.) Watendaji huduma wameonyeshwa neema kwa kuruhusiwa kufanya huduma! Bila ya dhana “watendaji huduma,” na bila Kazi ya watendaji huduma, hawa watendaji huduma wangekuwa wapi? Miongoni mwa wasioamini, wakiishi na kufa pamoja na mifugo. Ni neema iliyoje wanayoifurahia leo, kuruhusiwa kuja mbele za Mungu, na kuja katika nyumba ya Mungu! Hii ni neema kubwa! Kama Mungu hakukupa nafasi ya kutoa huduma, usingekuwa na nafasi ya kuja mbele za Mungu. Kwa kusema machache, hata kama wewe ni Mbudha na umepata maisha ya milele, sanasana wewe ni mtumwa katika ulimwengu wa kiroho; hutaweza kamwe kumwona Mungu, au kusikia sauti Yake, au kusikia maneno Yake, au kuhisi upendo Wake na baraka Zake kwako, na hata isingewezekana kamwe kuonana na Yeye uso kwa uso. Kilicho tu mbele ya wafuasi wa Budha ni kazi rahisi. Hawawezi kamwe kumjua Mungu, na wanaitikia na kutii kiupofu tu, wakati ambapo watendaji huduma wanafaidi mengi sana katika hatua hii ya kazi. Kwanza, wanaweza kuonana na Mungu uso kwa uso, kusikia sauti Yake, kuyasikia maneno Yake, na kupitia neema na baraka Anazowapa watu. Zaidi ya hayo, wanaweza kufurahia maneno na ukweli unaotolewa na Mungu. Wanapata mengi zaidi! Mengi zaidi! Hivyo, kama mtendaji huduma, huwezi hata kufanya juhudi zilizo za kweli, je, Mungu bado atakuweka? Hawezi kukuweka. Hataki mengi kutoka kwako lakini hufanyi chochote Anachotaka vizuri, hujawajibika ipasavyo—na kwa hivyo, bila shaka, Mungu hawezi kukuweka. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Mungu hakudekezi, lakini wala Hakubagui. Mungu anafanya kazi na kanuni hizo. Mungu hutekeleza mambo jinsi hii kwa watu na viumbe wote.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp