Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 144

13/07/2020

Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa “Neno linakuwa mwili” ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Anazungumza hasa. Usisubiri kuona ishara na maajabu; hutayaona! Maana hukuzaliwa katika Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa katika Enzi ya Neema, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini umezaliwa katika siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhalisia na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza kumwona tu Mungu katika mwili wa vitendo, Ambaye si tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu Anaweka wazi matendo mbalimbali. Katika kila enzi Anaweka wazi sehemu ya matendo ya Mungu, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na inawakilisha sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayoyaweka wazi yanatofautiana na enzi ambayo kwayo Anafanya kazi, lakini yote yanampatia mwanadamu maarifa ya Mungu ambayo ni ya kina, imani kwa Mungu ambayo ni yenye kuhusika na mambo halisi sana, na ambayo ni ya kweli zaidi. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, na kwa sababu Mungu ni wa ajabu ni mkuu sana, kwa sababu Yeye ni mwenyezi, na ambaye Hapimiki kina. Ikiwa unamwamini Mungu kwa kuwa Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na baadhi ya watu watakwambia, “Je, pepo wachafu pia hawawezi kufanya mambo hayo?” Je, hii sio kuielewa vibaya taswira ya Mungu kwa kuilinganisha na taswira ya Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na njia nyingi ambazo kwazo Anafanya kazi na kuzungumza. Mungu Anatumia matamshi yake kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Mwanadamu anamwamini Mungu, kwa sababu ya matendo Yake mengi, na si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, na wanadamu wanamwelewa tu kwa sababu wanaona matendo Yake, Ni kwa kujua tu matendo halisi ya Mungu, namna Anavyofanya kazi, njia ambazo Anaonyesha hekima Yake, vile Anavyozungumza, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa mkamilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhalisia wa Mungu na kuelewa tabia Yake. Kile Anachopenda, kile Anachochukia, namna Anavyomfanyia kazi mwanadamu—kwa kuelewa yale ambayo Mungu Anayapenda na Asiyoyapenda, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na kile ambacho ni hasi, na kupitia maarifa yako juu ya Mungu kunakuwa na maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi unapaswa kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na unapaswa kuweka sahihi mitazamo yako kuhusu kuwa na imani kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp