Swahili Gospel Movie "Kusubiri" | Bwana Yesu Kristo Ameonekana Kufanya Kazi Yake

26/04/2018

Yang Hou'en ni mchungaji katika kanisa la nyumbani Uchina. Pamoja na babake Yang Shoudao, wamemngoja Bwana Yesu ashuke kutoka mawinguni na kuwachukua juu hadi katika ufalme wa mbinguni. Kwa ajili ya hili, walimfanyia Bwana kazi kwa bidii, walishikilia imara jina Lake, na kuamini kuwa yeyote ambaye sio Bwana Yesu ashukaye mawinguni ni Kristo wa uongo. Na hivyo, waliposikia habari kuhusu kuja mara ya pili kwa Bwana, hawakuisikiliza wala kuikubali. Walidhani ni bora kukesha na kungoja. …Wakiendelea kungoja kwa kimyakimya, binamu wa Yang Hou'en, Li Jiayin alikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, na kueneza injili kwao. Baada ya majadiliano makali sana, Yang Hou'en hatimaye alielewa maana ya kweli ya “kukesha na kuomba,” na aliiweza kuona kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, njia, uzima, na hii ni sauti ya Bwana, na Mwenyezi Mungu ni kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu ambaye walikuwa wamemngoja kwa miaka mingi sana …

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp