Wimbo wa Sifa | Yasifu Maisha Mapya (Muziki wa Akapela)

28/05/2017

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe!

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu!

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu.

Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ni neno la Mungu ambalo limenibadilisha,

kwa hivyo nina maisha mapya ya kumsifu Mungu. (Halleluya!)

Maumivu na mkanganyo vimetoweka; Nimefunguliwa katika roho na ninaimba wimbo. (Halleluya!)

Ni vizuri kweli kuelewa ukweli. Nimeupita mwili, mimi ni huru sana! (Msifu Mungu!)

Dhana zote na kutokuelewana kumeondolewa mbali, tabia yangu asi imebadilishwa.

Mimi hutembea katika njia ng'avu ya maisha ya binadamu; upendo wa Mungu ni wa thamani na halisi sana! (Msifu Mungu!)

Ni furaha ya Mungu kuufurahia upendo wa Mungu.

Nimeuonja upendo wa Mungu na siwezi kumwacha Mungu tena.

Ndugu wako pamoja, bila vikwazo au umbali.

Sisi huhudumu kwa uratibu katika kanisa, kwa moyo mmoja na akili, na kwa furaha sisi huimba wimbo wa sifa.

Kuimba kumejaa upendo wa Mungu. Twaimba mioyo minyofu.

Mungu wa vitendo Ametufanya wapya na kutubadilisha, kutufanya wapya na kutugeuza kuwa mtu mpya.

Ni nani hadhihirishi upendo katika moyo wake? Ni nani hadhihirishi mapenzi katika moyo wake?

Unacheza kumtukuza Mungu, nami napiga makofi yangu kando.

Tumeipita mipaka ya mizigo ya dunia, familia, na mwili; tukipendana, sisi ni watamu!

Siku zilizopita za maisha ya zamani kamwe hazitarudi, na wakati wa thamani uko mbele. Wakati wa thamani uko mbele!

Ni la kufurahisha sana kutekeleza wajibu wangu na kushuhudia, sisi huwa na ushirika kuhusu ukweli, tuliofunguliwa na huru.

Watu wa Mungu hufurahia maisha mapya; maisha bashashi ya ubinadamu yanipungia. (O.)

Ni la kufurahisha sana kutekeleza wajibu wangu na kushuhudia, sisi huwa na ushirika kuhusu ukweli, tuliofunguliwa na huru.

Watu wa Mungu hufurahia maisha mapya; maisha bashashi ya ubinadamu yanipungia.

Nitamwabudu Mungu wa vitendo milele!

Haleluya!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp