Wimbo wa Kusifu | Watu Wote wa Mungu Wamsifu Kikamilifu (Music Video)
29/12/2019
Tumenyakuliwa mbele ya Mungu.
Tunajiunga na karamu ya wingi, tuna furaha sana.
Tunafurahia maneno ya Mungu na tunaelewa ukweli,
roho zetu zimeokolewa na tunahisi huru.
Mioyo yetu imejaa shukrani na sifa.
Hatuna budi ila kuimba.
Furaha iliyo mioyoni mwetu haiwezi kuelezeka.
Sifu na uruke kwa furaha.
Mungu anastahili heshima na utukufu.
Mapenzi ya Mungu yanafanyika hapa duniani.
Watu wote wa Mungu wamsifu kikamilifu.
Tunafurahia maneno ya Mungu kila siku.
Tunayatenda maneno ya Mungu, tunaingia katika uhalisi.
Tunapitia hukumu na utakaso,
na tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu wapya.
Mwenyezi Mungu ametuokoa kutoka katika upotoshaji wa Shetani.
Sasa tumebadilika kweli.
Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!
Sifu na uruke kwa furaha.
Mungu anastahili heshima na utukufu.
Mapenzi ya Mungu yanafanyika hapa duniani.
Watu wote wa Mungu wamsifu kikamilifu.
Mwenyezi Mungu amemshinda Shetani,
kufanya kikundi cha watu kuwa washindi,
wakikamilishwa kwa majaribu na dhiki.
Wao ndio washindi mbele ya Shetani!
Tabia ya Mungu yenye haki imefichuliwa.
Wote wanaompinga Mungu wataangamia.
Mwenyezi Mungu amemshinda Shetani!
Sifu na uruke kwa furaha.
Mungu anastahili heshima na utukufu.
Mapenzi ya Mungu yanafanyika hapa duniani.
Watu wote wa Mungu wamsifu kikamilifu.
Wale wanaofuatilia ukweli wanapata wokovu wa Mungu.
Wale walio na imani ya kweli kwa Mungu wanapokea neema Yake.
Tabia ya Mungu yenye haki tunaisifu!
Hadi mbinguni zafika nyimbo zetu za sifa!
Kazi ya Mwenyezi Mungu ni ya kimiujiza kweli.
Maneno ya Mungu yatimiza yote.
Watu wote wanamrudia Mungu,
wakiisifu kazi kubwa ya Mungu ambayo imekamilika!
Sifu na uruke kwa furaha.
Mungu anastahili heshima na utukufu.
Mapenzi ya Mungu yanafanyika hapa duniani.
Watu wote wa Mungu wamsifu kikamilifu.
Umetoholewa kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video