Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 122

18/07/2020

Kazi ya awali ya hatua tatu za kazi ya Mungu ilifanywa moja kwa moja na Roho, na wala si mwili. Hata hivyo, kazi ya mwisho ya hatua tatu za kazi ya Mungu, inafanywa na Mungu mwenye mwili, na wala haifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya wokovu ya hatua ya katikati pia imefanywa na Mungu mwenye mwili. Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi. Katika hatua tatu za kazi ya wokovu, hatua ya kwanza ya kazi ya sheria inatofautiana sana na kiini cha kazi ya usimamizi; ilikuwa tu ina mwonekano wa mbali wa kazi ya wokovu, na haikuwa mwanzo wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanywa na Roho kwa sababu, chini ya sheria, mwanadamu alijua tu kuzishika sheria, na hakuwa na ukweli zaidi, na kwa sababu kazi katika Enzi ya Sheria haikujihusisha na kubadilisha silika ya mwanadamu, wala haikuwa inajihusisha na kazi ya jinsi ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Roho wa Mungu alikamilisha hatua hii rahisi ya kazi ambayo haikujihusisha na silika iliyopotoka ya mwanadamu. Hatua hii ya kazi ilikuwa na uhusiano mdogo na kiini cha usimamizi na haikuwa na uhusiano mkubwa na kazi rasmi ya wokovu wa mwanadamu, na kwa hivyo haikumhitaji Mungu ili aweze kuifanya kazi yake. Kazi inayofanywa na Roho ni mdokezo na haifahamiki, na ya kuogopesha na isiyofikiwa kwa mwanadamu; Roho hafai kikamilifu kwa ajili ya kufanya kazi ya wokovu moja kwa moja, na hafai kikamilifu kwa ajili ya kumpatia mwanadamu uzima moja kwa moja. Kinachomfaa zaidi mwanadamu ni kubadilisha kazi ya Roho na kuwa katika hali ambayo inaendana kwa ukaribu na mwanadamu, kile kinachomfaa mwanadamu zaidi ni Mungu kuwa mtu wa kawaida ili kufanya kazi Yake. Hii inahitaji Mungu apate mwili ili kuchukua kazi ya Roho, na kwa mwanadamu, hakuna njia inayofaa zaidi ya Mungu kufanya kazi. Kati ya hatua tatu hizi za kazi, hatua mbili zinafanywa na mwili, na hatua mbili hizi ni awamu muhimu ya kazi ya usimamizi. Hatua mbili hizi zinakamilishana na zinaafikiana. Hatua ya kwanza ya Mungu mwenye mwili iliweka msingi kwa ajili ya hatua ya pili, na tunaweza kusema kwamba hatua mbili hizo zinaunda Mungu mwenye mwili mmoja, na zote hazina ulinganifu. Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisia wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi yake, na umuhimu wa kazi. Unapokuja umuhimu wa kazi hii, kwa misingi ya mbinu ya kutumia—kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, au kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili, au kazi inayofanywa kupitia mwanadamu—ya kwanza kuondolewa ni kazi inayofanywa kupitia mwanadamu, na kulingana na asili ya kazi, na asili ya kazi ya Roho dhidi ya ile ya mwili, hatimaye inaamuliwa kwamba kazi inayofanywa na mwili ni ya manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na inakuwa na manufaa zaidi. Hili ni wazo la Mungu wakati wa kuamua ama kazi ifanywe na Roho au ifanywe na mwili. Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi bila mantiki; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli nyuma ya kazi zote za Mungu. Kwa umahususi, kuna mpango wa Mungu zaidi katika kazi kubwa kama hiyo kwa kuwa Mungu mwenye mwili akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Na kwa hivyo, hekima ya Mungu na uungu Wake wote unaakisiwa katika kila tendo lake, fikra, na wazo katika kufanya kazi; huu ndio uungu wa Mungu ambao uko imara na wenye mpangilio. Fikra hizi na mawazo pembuzi ni ngumu kwa mwanadamu kuwaza, na mambo magumu kwa mwanadamu kuamini, aidha, magumu kwa mwanadamu kuyafahamu. Kazi inayofanywa na mwanadamu ni kulingana na kanuni ya ujumla, ambayo, kwa mwanadamu, ni ya kuridhisha sana. Lakini ukilinganisha na kazi ya Mungu, kuna tofauti kubwa sana; ingawa matendo ya Mungu ni makuu na kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu sana, nyuma yake kuna mipango na mipangilio midogo ya uhakika ambayo haiwezi kufikirika kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi yake sio kulingana na kanuni tu, lakini pia inajumuisha vitu vingi ambavyo haviwezi kusemwa kwa lugha ya kibinadamu, na haya ni mambo ambayo hayaonekani kwa mwanadamu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda lake la nje) katika kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine Abadilishe utambulisho wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na anayeteswa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp