Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 35
13/06/2020
Mungu Amekuja ulimwenguni hasa kuzungumza maneno Yake; unachoshiriki nacho ni neno la Mungu, uonacho ni neno la Mungu, usikiacho ni neno la Mungu, unachokaa nacho ni neno la Mungu, unachopitia ni neno la Mungu, na Mungu aliyepata mwili huyu kimsingi hutumia neno kumfanya mwanadamu kamili. Yeye haonyeshi ishara na maajabu, na hasa hafanyi kazi ambayo Yesu Alifanya hapo awali. Ingawa wao ni Mungu, na wote ni mwili, huduma Zao sio sawa. Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, kuleta ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, “Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba.” Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvu, na kumfanya aweze kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa. Leo ni kazi gani ambayo Mungu katika mwili atakamilisha? Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya “Neno kuonekana katika mwili,” kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe kuwa kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. Kuna wakati ambapo watu wengine humpinga Mungu. Mungu hasababishi ukosefu mkubwa wa starehe kwako, mwili wako hauadibiwi wala wewe kupitia ugumu—lakini pindi tu neno Lake linapokuja juu yako, na kukutakasa, hutaweza kuvumilia. Je si hivyo ndivyo ilivyo? Wakati wa “watendaji huduma” Mungu Alisema mwanadamu atupwe katika shimo lisilo na mwisho. Mwanadamu aliweza kufika kwenye shimo lisilo na mwisho? Kupitia kwa maneno tu kumtakasa mwanadamu, mwanadamu aliingia kwenye shimo lisilo na mwisho. Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. Kazi ya Mungu nyingi katika wakati huu wote imekuwa kutoa, ufunuo, na kushughulika. Hatoi laana kwa mwanadamu kijuu juu, na hata Akifanya hivyo, ni kupitia kwa neno. Na hivyo, katika enzi hii ya Mungu kuwa mwili, usijaribu kuona Mungu akiponya wagonjwa na kufukuza mapepo tena, usijaribu kila mara kuona ishara—hakuna haja! Ishara hizo haziwezi kumfanya mwanadamu kamili! Kuongea wazi: Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama ukweli huu wa kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia. Badala ya kulenga vitu vilivyo vibaya, mnapaswa tu kulenga yale yaliyo mazuri—hivyo ni kusema, bila kujali kama maneno ya Mungu yamekamilika au la, ama iwapo kuna majilio ya ukweli ama haupo, Mungu anamfanya mwanadamu kupata uzima kutoka kwa maneno Yake, na hii ndiyo ishara kuu kushinda zote, na hata zaidi, ni ukweli usiopingika. Huu ndio ushahidi bora wa kupata ufahamu kumhusu Mungu, na ni ishara hata kuu kushinda ishara. Maneno haya pekee yanaweza kumfanya mwanadamu kamili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video