Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 36

13/06/2020

Pindi tu Enzi ya Ufalme ilipoanza, Mungu alianza kuachilia Maneno Yote. Katika siku za baadaye, maneno haya yataendelea kutimizwa, na katika wakati huo, mwanadamu atakua katika uzima. Matumizi ya neno na Mungu kufichua tabia potovu ya mwanadamu ni ya kweli zaidi, na ni ya lazima zaidi, na Hatumii chochote ila neno kufanya kazi Yake ili kuifanya imani ya mwanadamu iwe kamili, kwani leo ni Enzi ya Neno, na inahitaji imani, uamuzi na ushirikiano wa mwanadamu. Kazi ya Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutumia neno Lake kutumikia na kukimu. Ni baada tu ya Mungu katika mwili kumaliza kuongea maneno Yake ndipo yatakapoanza kutimika. Wakati Anapoongea, maneno Yake hayatimiliki, kwani Anapokuwa katika hatua ya mwili, maneno Yake hayawezi kutimika, na hii ni ili mwanadamu aweze kuona kuwa Mungu ni mwili na sio Roho, ili mwanadamu aweze kutazama hali halisi ya Mungu kwa macho yake Mwenyewe. Katika ile siku ambayo kazi Yake imekamilika, wakati ambao maneno yote yanayopaswa kunenwa na Yeye duniani yamemenenwa, maneno Yake yataanza kutimika. Sasa sio enzi ya utimizaji, kwa kuwaHajamaliza kuongea maneno Yake. Kwa hivyo ukiona kuwa Mungu bado Ananena maneno yake duniani, usingoje utimizo wa maneno Yake; Mungu Anapokoma kunena maneno Yake, na wakati kazi Yake duniani imekamilika, huo ndio utakuwa wakati ambao maneno Yake yanaanza kutimika. Katika maneno Anayozungumza duniani, kunayo, katika mtazamo mmoja, utoaji wa uzima, na katika mtazamo mwingine, kuna unabii—unabii wa vitu vitakavyokuja, wa vitu vitakavyofanywa, na vya vitu ambavyo bado havijatimizwa. Kulikuwa pia na unabii katika maneno ya Yesu. Katika mtazamo mmoja, Alitoa uzima, na katika mtazamo mwingine Alinena unabii. Leo, hakuna mazungumzo ya kutekeleza maneno na uhakika kwa wakati mmoja, kwani tofauti kati ya yale yanayoweza kuonekana na macho ya mwanadamu na yale yanayotendwa na Mungu ni kubwa mno. Inaweza kusemwa tu kwamba, mara kazi ya Mungu inapokamilika, maneno Yake yatatimika, na mambo ya hakika yatakuja baada ya maneno. Duniani, Mungu katika mwili wa siku za mwisho anafanya huduma ya neno, na kwa kufanya huduma ya neno, Anazungumza maneno pekee, na hajali kuhusu mambo mengine. Mara kazi ya Mungu itakapobadilika, maneno Yake yataanza kutimika. Leo, maneno yanatumiwa kwanza kukufanya mkamilifu; Atakapopokea utukufu katika ulimwengu mzima, utakuwa wakati ambao kazi Yake imekamilika, wakati maneno yote ambayo yanapaswa kuzungumzwa yatakuwa yamezungumzwa, na maneno yote yamekuwa ukweli. Mungu amekuja duniani wakati wa siku za mwisho ili kutekeleza huduma ya neno ili mwanadamu amtambue, na ili mwanadamu aone kile Alicho, na aone hekima Yake na matendo Yake yote ya maajabu kutoka kwa neno Lake. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno kimsingi kushinda watu wote. Baadaye neno Lake litakuja katika kila dini, kikundi, taifa na madhehebu; Mungu hutumia neno kushinda, kuwafanya wanadamu wote waone kuwa neno Lake lina mamlaka na nguvu—na kwa hivyo leo, mnakumbana tu neno la Mungu.

Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Bibilia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapunziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaifanyikia Misiri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp