Have You Been Raptured? | "Kutamani Sana" | Swahili Christian Movie

25/08/2018

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi Wake: "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Kwa sababu ya hili, vizazi vya waumini vimeendelea kujawa na tumaini na kushikilia maombi kwa ajili ya kutimizwa kwa ahadi ya Bwana, na kutumaini na kuomba kwamba wanyakuliwe hadi kwenye mbingu ili kukutana na Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni wakati Bwana atakapokuja. Huu pia unamfafanua mhusika mkuu wa filamu, Chen Xiangguang. Ni mtafutaji mwenye shauku kubwa, anaieneza injili, na kumshuhudia Bwana ili kukaribisha kurudi kwa Bwana. Licha ya kuachishwa kazi shuleni na kushindwa kupata huruma kutoka kwa familia yake, katu hakati tamaa moyoni mwake. Siku moja akiwa kwenye kikao, Chen Xiangguang anakamatwa na kutiwa gerezani na serikali ya Kikomunisti ya Kichina. Kupitia kwa utawala na mipangilio ya ajabu ya Mungu, anakutana na Zhao Zhiming, Mkristo kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Zhao Zhiming anamtolea ushuhuda kuhusu kuonekana kwa Mungu na kazi katika siku za mwisho na kumtatulia miaka yake ya mawazo na fikira kwa kutumaini na kuomba kwa ajili ya kurudi kwa Bwana. Baada ya kutoka gerezani, Chen Xiangguang anawaongoza kaka na dada zake katika kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kila mtu hatimaye anafahamu maana ya kunyakuliwa hadi kwenye ufalme wa mbinguni, haijalishi kama ufalme umo hasa ulimwenguni au mbinguni, na namna ambavyo watu wanafaa kukaribisha kurudi kwa Bwana …

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp