50 Jina la Mwenyezi Mungu Lashuhudiwa katika Mataifa Yote ya Dunia

1 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

2 Lugha za mataifa mbalimbali ni tofauti na kila nyingine lakini kuna Roho mmoja tu. Huyu Roho huunganisha makanisa kote ulimwenguni na ni mmoja na Mungu, bila tofauti hata kidogo, na hili ni jambo ambalo halina shaka kabisa. Roho Mtakatifu sasa anawapaazia sauti na sauti Yake yawaamsha. Hii ni sauti ya huruma ya Mungu. Wanaliita kwa sauti jina takatifu la Mwenyezi Mungu! Wao pia wanatoa sifa na kuimba. Hakuwezi kuwa na mkengeuko wowote katika kazi ya Roho Mtakatifu, na watu hawa hufanya linalowezekana ili kuendelea kwenye njia sahihi, huwa hawajitoi na maajabu yake hulundikana juu ya maajabu. Ni kitu ambacho watu huona ugumu kufikiria na kisichowezekana kukikisia.

3 Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme wa maisha katika ulimwengu! Yeye huketi juu ya kiti kitukufu cha enzi na huihukumu dunia, huwatawala wote, huyaongoza mataifa yote; watu wote hupiga magoti Kwake, humwomba, huja karibu naye na kuwasiliana na Yeye. Bila kujali muda gani mmemwamini Mungu, jinsi hadhi yenu ilivyo ya juu au jinsi ukubwa wenu wa vyeo ulivyo, kama nyinyi humpinga Mungu katika mioyo yenu basi ni lazima mhukumiwe na lazima msujudu mbele Yake, mkitoa sauti chungu ya kusihi kwenu; huku kweli ni kuvuna matunda ya matendo yenu wenyewe. Sauti hii ya kupiga mayowe ni sauti ya kuteswa katika ziwa la moto na kiberiti, na ni kilio cha kuadibiwa na fimbo ya chuma ya Mungu; hii ndiyo hukumu mbele ya kiti cha Kristo.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 8” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 49 Dunia Yote Itashangalia na Kumsifu Mungu

Inayofuata: 51 Binadamu na Mungu Washiriki katika Furaha Kamili ya Muungano

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp