Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Sikiliza Sauti ya Mungu Tazama Kuonekana kwa Mungu

A. Mungu Mwenye Mwili wa Siku za Mwisho Akionekana na Kufanya Kazi kama Mwana wa Adamu

Madondoo ya Ziada ya Mahubiri na Ushirika

1Swali la 1: Unashuhudia kwamba Mungu amepata mwili na kuwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, lakini wachungaji na wazee wengi wa dini wameamua kwamba wakati ambapo Bwana atarudi Atashuka juu ya wingu. Hili kimsingi ni kulingana na maandiko haya: “Huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye” (Ufunuo 1:7). Aidha, wachungaji na wazee wa dini pia wametufundisha kwamba Bwana Yesu yeyote ambaye hashuki juu ya wingu ni wa uongo na anapaswa kukataliwa. Hatujui kama dhana hii inalingana na Biblia au la. Je, kweli huu ni ufahamu sahihi?
2Swali la 2: Ingawa wale wanaomwamini Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, watu wachache sana wanaelewa ukweli wa kupata mwili. Wakati ambapo Bwana atarudi, Akionekana tu kama Bwana Yesu alivyofanya, akiwa Mwana wa Adamu na kufanya kazi, watu kweli hawatakuwa na njia ya kumtambua Bwana Yesu na kukaribisha kurudi Kwake. Kwa hiyo kupata mwili kweli ni nini? Ni nini kiini cha kupata mwili?
3Swali la 3: Mbona Mungu amepata mwili katika siku za mwisho, akiwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu? Ni nini tofauti ya kweli kati ya mwili wa roho wa Bwana Yesu kufufuliwa kutoka kwa kifo na Mwana wa Adamu mwenye mwili? Hili ni suala ambalo hatulielewi—tafadhali shiriki ushirika kuhusu hili.
4Swali la 4: Katika Enzi ya Sheria, Mungu alimtumia Musa kutenda kazi Yake, hivyo kwa nini Mungu hamtumi mtu kutekeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini Mungu mwenye mwili Mwenyewe lazima aifanye?
5Swali la 5: Kwa nini inasemwa kwamba wanadamu potovu lazima waokolewe na Mungu mwenye mwili? Hili ni jambo ambalo watu wengi sana hawalielewi—tafadhali shiriki ushirika kuhusu hili.
6Swali la 6: Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na alitumika kama dhabihu ya dhambi kwa ajili ya wanadamu, akiwakomboa kutoka kwa dhambi. Mungu amepata mwili tena katika siku za mwisho na ametamka ukweli na kufanya kazi ya hukumu, akiwatakasa kikamilifu na kuwaokoa wanadamu. Kwa nini Mungu anahitaji kupata mwili mara mbili ili kufanya kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu? Ni nini umuhimu wa kweli wa Mungu kujipatia mwili Mwenyewe mara mbili?
7Swali la 7: Miili miwili ya Mungu ilishuhudia kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Tunapaswaje kuelewa Kristo kuwa ukweli, njia na uzima?
8Swali la 8: Unashuhudia kwamba Mungu kujipatia mwili Mwenyewe katika siku za mwisho kumeanza Enzi ya Ufalme, kuimaliza enzi nzee ya utawala wa Shetani. Tunachotaka kuuliza ni, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imemaliza vipi enzi ya giza ya imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini, na ya utawala wa Shetani? Tafadhali shiriki ushirika wenye maelezo.

B. Mpango wa Usimamizi wa Mungu wa Kuwaokoa Binadamu—Hatua Tatu za Kazi