193 Kristo wa Siku za Mwisho Analeta Njia ya Uzima wa Milele

1

Mungu mwenyewe ni uzima na ukweli, na maisha Yake na ukweli vimeungana.

Wale wasiopata ukweli Wake, hawapati uzima.

Bila kupokea uongozi na usaidizi wa ukweli Wake,

mwanadamu anaachwa na barua tu na mafundisho, mwanadamu anaachwa na kifo.

Uzima wa Mungu na ukweli vimesokotana na vipo kila wakati.

Kama hujui chanzo cha ukweli, hupokei uboreshaji wa maisha.

Kristo wa siku za mwisho Analeta uzima na Anabeba uvumilivu na ukweli wa milele.

Ukweli huu ni njia ambayo mwanadamu lazima atembee ili apate uzima.

Ni njia pekee ya kumjua Mungu na kupokea kibali Chake.

2

Kupuuza njia ya uzima inayoletwa na Kristo wa siku za mwisho

ni kutelekeza kibali cha Yesu,

na kujigeuza kutoka kwa ufalme wa mbinguni.

Unakuwa kikaragosi na mfungwa wa historia.

Usipopata toleo la maisha, hakika huna ukweli.

Wewe tu ni mwili mbovu, fikira tupu na mawazo yasiyo na mazao.

Kristo wa siku za mwisho Analeta uzima na Anabeba uvumilivu na ukweli wa milele.

Ukweli huu ni njia ambayo mwanadamu lazima atembee ili apate uzima.

Ni njia pekee ya kumjua Mungu na kupokea kibali Chake.

Maneno yaliyo katika vitabu sio uzima, rekodi za historia sio ukweli,

njia nzee za kale sio rekodi za maneno ambayo Mungu ananena leo.

Ukweli unaonyeshwa na Mungu pekee duniani na Mungu kati ya mwanadamu.

Anaonyesha mapenzi ya Mungu na njia Yake ya kufanya kazi.

3

Watu ambao wamefungwa na pingu za historia na kufungwa na minyororo ya kanuni, kufungwa na maagizo,

hawatapata uzima kamwe ama njia ya uzima wa milele.

Kile walicho nacho ni historia na kanuni tu za maelfu kadhaa ya miaka.

kama vidimbwi vya giza vilivyotuama,

ambayo sio maji ya uzima kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu.

Na wale wasiokunywa kutoka kwa maji haya watajikokota kama maiti milele,

kama watumwa wa Shetani, kama wana wa jahanamu.

Kristo wa siku za mwisho Analeta uzima na Anabeba uvumilivu na ukweli wa milele.

Ukweli huu ni njia ambayo mwanadamu lazima atembee ili apate uzima.

Ni njia pekee ya kumjua Mungu na kupokea kibali Chake.

Kristo wa siku za mwisho Analeta njia ya uzima wa milele.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 192 Kiini cha Kristo Ni Mungu

Inayofuata: 194 Utambulisho wa Mungu ni Mungu Mwenyewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki